Museveni: Nitaondoka tu iwapo kuna mtu wa maana nitakayeona naweza kumuachia Uganda

Museveni: Nitaondoka tu iwapo kuna mtu wa maana nitakayeona naweza kumuachia Uganda

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye anawania muhula wa sita madarakani, amesema kwamba hajaona mtu mwenye uwezo wa kuongoza Uganda kwa sasa, na hivyo ataendelea kuwa madarakani kwa sababu wapiga kura nchini humo bado wanamhitaji kuendelea kuongoza taifa hilo.

Akihutubia viongozi wa chama chake cha National Resistance Movement (NRM) katika wilaya ya Lukungiri, ambayo ni ngome ya kisiasa ya aliyekuwa mpinzani wake mkuu mara nne Dr. Kiiza Besigye, Museveni amesema kwamba wapinzani wake ni watu wazembe wanaotaka kusukumwa kama mkokoteni.

“Wanajua lengo langu katika siasa lakini wanataka kunishawishi niache msimamo wangu. Wanapiga kelele kwamba nastahili kuondoka madarakani utadhani sina pa kwenda,” amesema Museveni akitumia mojawapo ya lugha zinazozungumzwa magharibi mwa Uganda.

Akiwataja watatu hao ambao walikuwa marafiki wake wa muda mrefu na mmoja alikuwa daktari wake binafsi (Dr. Kiiza Besigye), kuwa watu “wasiokuwa na maana yoyote na ambao sasa wanataka aondoke madarakani.”

Amesema kwamba "huwa nakasirika sana ninaposikia watu wakiniambia kwamba niondoke madarakani, lakini huwa najaribu sana kujizuia na kuwa mtulivu.”

“Kama ulishindwa kufanya nilichokuambia, usilete vurugu kwa kuniambia kwamba niondoke madarakani. Wapiga kura ndio wanaoamua,” amesema Museveni akiongezea kwamba “hata nikiondoka nani hao wasiokuwa na maana yoyote ambao wanataka kusukumwa kama mkokoteni wanaotaka kuongoza nchi hii.

Muniache niendelee kuongoza kwa sababu raia wa Uganda wananihitaji niwepo. Nitaondoka tu iwapo kuna mtu wa maana nitakayeona naweza kumuachia Uganda. Nataka niwe na uhakika mahali naiacha Uganda”
 
Huyo mtu wamaana atamuona lini na sisi tutajuaje kuwa ni mtu wamaana. Huyu atakuja kuuwawa huyu anatafuta risasi tu sasa.
Labda risasi za huku JF, hapo sawa. Taamali kirefu cha chama chake cha NRM labda utapata fununu kidogo.
 
Kwa upande wa nani wakumuachia Nchi kwa wakati huu na kwa wagombea waliopo nchini Uganda ,Naungana na Mh Dikteta kwani kama unaakili timamu huwezi ukamkabidhi Taifa kubwa kama Uganda mvaa milegezo Bob Wine. Never!! Nasema bob kwa sababu ndiye anayejisema ndo mpinzani wa Mh Dikteta.

Waganda wamemuogopa mh dikteta kiasi kwamba waakawachia kina Bob wine watimize wajibu.Hilo ni kosa la waganda na litawagharim.

Walikosa mtu sahihi wa kumpambanisha na Dikteta huyu? Shame on u Waganda.

Yani wanazidiwa mpaka na wana Ufipa? Ufipa walikuwa sahihi kumuweka lissu sababu "angalau"anaonekana kuwa presidential material ,sio Bob. Hivi Bob na sugu wana tofauti

#Kwa uoga,ujinga na ushamba wa waganda kwa kushindwa kusimamisha mtu sahihi, acha Best friend wake na Mh Jiwe atawale Milele.
 
Rubbish and you don't deserve to be here. Mawazo ya Kuburuzwa na Kutawaliwa kama Kondoo bila Kuoji na kutojitambua kifikira. Safari bado ni Ndefu kama taifa litakuwa na Mawazo haya Mgando. Daaah! sijui hata wewe ni wa jinsia gani! Fikiria kama Mwanaume Unayetamani hata siku moja na wewe ufike alipo hoyo Dictator.
 
Yani wagombea wa Uganda hadi kero,mwingine nae ndo kwanza anamiaka 34 , hatakuoa hajaoa halafu umpe nchi?

Yani nina uhakika kama Mseveni angekuwa huku kwa wajuaji wa Ufipa wanaoijua siasa ya maji machafu, wallah safari hii angepata kura yake na mke wake ovaa. Sioni tofauti kati ya Mseveni na idd amini. Lakin kwakua Ug hazimo, acha mzee wa watu afie Ikulu
 
#GENTAMYCINE katika rubish uliyoongea ndo nmekudharau kabsa heshima yako uliyoijenga kwa muda mrefu humu jukwaani leo umeishusha kwa maandishi machache, umepatwa na nini mkuu au umelazimishwa?,.au simu yako imeibiwa maana sijawahi kuwaza utakuja kuongea pumba kiasi hiki.

Kwahyo waganda wote hawana akili? Ya kujiongoza? Vipi mseveni akifa Taifa halitoendelea? Litakufa nalo? Umepatwa na nini mpaka umekuwa na mawazo mgando kiasi hcho mkuu ebu kaa kunywa maji kdogo then FIKIRIA upya.
 
Bila Chuma hakitaeleweka hapo.
Chuma kufanikisha Haiwezekani kwa Uganda ya mwaka huu, labda kuwe na mkono wa mataifa makubwa.

Chuma hata kwa Kagame naona Haiwezekani sasa itakuwa jembe hilo la msituni.
 
Kakaa madarakani miaka 34 na hajaweza kutengeneza mazingira ya kupatikana watu (sio mtu) wa kuweza kuongoza Uganda! Hii peke yake ni sababu tosha ya kumfanya aondoke madarakani. Kuna kufeli zaidi ya huko? Sifa mojawapo ya kiongozi mzuri ni uwezo wa kutengeneza watu wanaoweza kuja kumrithi.
 
Chuma kufanikisha Haiwezekani kwa Uganda ya mwaka huu ,labda kuwe na mkono wa mataifa makubwa

Chuma hata kwa Kagame naona Haiwezekani sasa itakuwa jembe hilo la msituni
Hao wote wawili bila chuma either ni kwa support kutoka nje/ndani hakuna anayeng'oka ng'oo.
 
Back
Top Bottom