Museveni: Sitaki Kuwa Sehemu ya Wasaliti wa Afrika. Apiga Marufuku Kuuza Madini ghafi ya Uganda, Tanzania tuna la Kujifunza

Museveni: Sitaki Kuwa Sehemu ya Wasaliti wa Afrika. Apiga Marufuku Kuuza Madini ghafi ya Uganda, Tanzania tuna la Kujifunza

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2022
Posts
9,436
Reaction score
10,944
Heri ya Christmas wadau.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amepiga marufuku Kuuza Madini ghafi yanayotoka Uganda akisema hataki kuwa sehemu ya Wasaliti wa Afrika..

Museveni amesema kuuza madini ghafi Ni kuwapelekea ajira watu wa Nje na hivyo Kutaka wanaotaka kuuza madini wahakikishe yameongezewa thamani..

My Take.

Tanzania hatujachelewa ,tuna la Kujifunza na ikibidi tuanze na Dhababu maana tayari tuna viwanda 3 vya kuchenjua dhahabu lakini Hakuna kinachofanyika..

20221225_115244.jpg
Screenshot_20221225-115121.png
 
Hata apige marufuku still madini sio mali zetu sisi ni walinzi tu. Madini yote duniani bila kujali mipaka yaani yapo nchi gani ni mali ya familia ya De Beers kizazi cha Kina Cecil Rhodes mtawala wa zamani wa kikoloni..
Wao ndio umiliki soko la madini duniani wao ndio ucontrol bei.
 
Hapo anachokifanya Museveni ni kuitumbukiza nchi kwenye shida tu. Wazungu wana syndicate ya kufa mtu juu ya haya madini.

Aende Kuzimu akamuulize Magufuli. Alipojenga ukuta kule Mererani na kuzuia wazungu kujinunulia tanzanite watakavyo thamani yake ilishuka kwa 90% ikaanza kutumika kama kete za kuchezea mchezo wa bao.

Alipowakataza kununua korosho watakavyo, korosho ikaonekana kama samadi.

Museveni yeye amekula chumvi nyingi hana cha kupoteza. Anasubiria parapanda tu.
 
Amekaa miaka 40 madarakani na Uganda ni mojawapo ya nchi maskini kabisa Africa.
Museveni ni kati ya viongozi wa Afrika wanaolitia bara hili aibu kwa kunajisi demokrasia kwa kuendesha chaguzi za maigizo na kukandamiza wapinzani.Yeye ndio msaliti namba moja wa bara tangu mwaka 1986 yuko madarakani kimagumashi
 
Hapo anachokifanya Museveni ni kuitumbukiza nchi kwenye shida tu. Wazungu wana syndicate ya kufa mtu juu ya haya madini.

Aende Kuzimu akamuulize Magufuli. Alipojenga ukuta kule Mererani na kuzuia wazungu kujinunulia tanzanite watakavyo thamani yake ilishuka kwa 90% ikaanza kutumika kama kete za kuchezea mchezo wa bao.

Alipowakataza kununua korosho watakavyo, korosho ikaonekana kama samadi.

Museveni yeye amekula chumvi nyingi hana cha kupoteza. Anasubiria parapanda tu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kete za kuchezea bao
 
Remind me amekaa hapo kwenye hiko kiti for how many years yet? Wananchi ni wavivu? Yeye kama kiongozi amefanya nini ? Au amewaacha wawe wavivu?
Ila kweli waganda ni wavivu sana. Kilimo tu ingewatoa bila hata madini. Ardhi yao yote ni rotuba
 
Back
Top Bottom