Museveni: Sitaki Kuwa Sehemu ya Wasaliti wa Afrika. Apiga Marufuku Kuuza Madini ghafi ya Uganda, Tanzania tuna la Kujifunza

Wanasiasa wa Africa ni vigumu sana kuelewa biashara. Kinachosababisha madini yasichakatwe katika nchi nyingi za Africa ni mazingira ya biashara kuanzia miondombinu, usalama,nishati, utaalamu, sera mpaka tozo na kodi.
 
Bobi wyne yupo wapi siku hizi ,alimtesa sana mseveni
 
Wanasiasa wa Africa ni vigumu sana kuelewa biashara. Kinachosababisha madini yasichakatwe katika nchi nyingi za Africa ni mazingira ya biashara kuanzia miondombinu, usalama,nishati, utaalamu, sera mpaka tozo na kodi.
Umenena vema ndugu. Ukichakata hapa Africa halafu unataka kwenda kuwauzia uliowazuia kuyachakata na ndiyo wapanga bei na hao hao ndiyo wenye vipimo vya ubora na viwango lazima wakukandamize tu.

Tukubali tu kwamba wazungu wanaiendesha hii dunia jinsi watakavyo.
 
Hili halina ubishi japo linaumiza sana..
 
Sio kweli. Ama huna taarifa au unapotosha makusudi. Tafuta taarifa.

Kujengwa kwa ukuta wa mererani kuliongeza mapato ya serikali na kufikia bilioni 2.17 mwaka 2020 kutoka millioni 165 mwaka 2016 kabla ya ukuta.

Huku kwenye korosho napo hujui kitu. Ni Magufuli ndio aliongeza thamani ya korosho baada ya serikali yake kuingilia kati kumuokoa mkulima kwa kuondoa watu wa kati waliokuwa wanashirikiana na vyama vya ushirika chini ya bodi ya korosho.

Mfano ukiangalia rekodi kwa 2015 kurudi nyuma bei elekezi ilikuwa haizidi 1200 na kuanzia 2016 bei elekezi ikafika hadi tzs 3810 kwa kilo moja ya korosho.

Na wakulima walilipwa kwa wakati yaani wiki pesa inaingia wakati miaka ya nyuma ilikuwa inachukua hadi miezi mitatu au sita.
 
Acha kutumia takwimu feki za Magufuli aliyekuwa analiongopea taofa kila uchwao:
*Tanzanite ilishuka bei kutoka shilingi 1,300,000/= kwa ounce Hadi sh 300,000/= kwa ounce moja. Kama hauko kwenye hii sekta kaa kwa kutuliia.

-Korosho ni kweli alizinunua yeye lkn serikali haikuweza kuziuza nje. Na msimu uliofuata seriakli yake ilibaki imetoa macho tu isijue cha kufanya. Wakulima wakalia kilio vha mbwa mwtu.

Na ndiyo maana mpk leo biashara ya korosho Mtwara imedoda. Kwasabb Magufuli aliharibu mfumo wa biashara hiyo na haujarejea tena. Kama haujihusishi na kilimo endelea kulipwa buku 7.
 
Kwa hiyo?
 
Hii umekoti wapi au mawazo yako
 
Wazungu washakwambia Hadi kwenye dollar wameandika We believe in GOD.
G-Gold
O-Oil
D-Diamond
Halafu uje kuwazingua tafuta historia ya kiongozi yeyote aliyewahi kuwasumbua katika hizo herufi tatu uone kama yupo hai.
 
Sioni Chakujifunza yoweri mseveni.....,
Kwa maana hamekalia madini hayo 45yrs. Then Leo ndio aje na sera ya kutaka kuongea thamani
Hata ivyo Uganda hakuna madini zaida ya wanayo waibia kabila Kongo...
 


Huna information ya kutosha juu ya unachokiongelea.
 
Hatujali sisi hayo! Museven kaleta amani Uganda sana kuliko wooote!! apewe heshima! hata akitawala millele!! nitamlipia ulinzi bure mie km akistaafu...nampenda sana huyu mzee! akae tu!

wengi hata wasomi kumpita walishindwa kurejesha amani Uganda, leo ndg/majirani zetu wametulia, eti tumnange huyu mzee No! ningekuwa na uwezo ningempa hata ardhi kubwa tu hapo Musoma!

Waganda walilia wakamwaga damu mpaka ardhi ikaitika abeee!...leo hayo mmesahau??? mnamnanga yesu wa Uganda kweli?? hakikak mwanadamu lazima achomwe moto tu!

km mnamdharau mseveni aliye leta amani waliyoshindwa wengi! mtamuheshimu nani?? je jiulize waweza kumuheshimu Mungu ambaye hujawahi kumuona??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…