Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Wanasiasa wa Africa ni vigumu sana kuelewa biashara. Kinachosababisha madini yasichakatwe katika nchi nyingi za Africa ni mazingira ya biashara kuanzia miondombinu, usalama,nishati, utaalamu, sera mpaka tozo na kodi.
Hapo anachokifanya Museveni ni kuitumbukiza nchi kwenye shida tu. Wazungu wana syndicate ya kufa mtu juu ya haya madini.
Aende Kuzimu akamuulize Magufuli. Alipojenga ukuta kule Mererani na kuzuia wazungu kujinunulia tanzanite watakavyo thamani yake ilishuka kwa 90% ikaanza kutumika kama kete za kuchezea mchezo wa bao.
Alipowakataza kununua korosho watakavyo, korosho ikaonekana kama samadi.
Museveni yeye amekula chumvi nyingi hana cha kupoteza. Anasubiria parapanda tu.