Mushi alikuwa mu-LAWI

Mushi alikuwa mu-LAWI

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
34,181
Reaction score
41,563
Utangulizi - Mambo ya nyakati ni nini?

Kitabu cha Kwanza cha Mambo ya Nyakati kinatueleza kuhusu ibada katika hekalu na kinatupa habari zaidi kuhusu ukoo wa Masihi. Kikiwa sehemu ya Neno la Mungu lililoongozwa kwa roho, ujumbe wake unaimarisha imani yetu na kuboresha uelewaji wetu wa Biblia

Mbali na rekodi za ukoo, Kitabu cha Kwanza cha Mambo ya Nyakati kinasimulia matukio ya kipindi cha miaka 40 hivi, tangu kifo cha Mfalme Sauli mpaka kifo cha Mfalme Daudi. Inaaminika kwamba kuhani Ezra ndiye aliyeandika kitabu hicho mwaka wa 460 K.W.K

Baada ya utangulizi huo sasa fungua Biblia yako Mambo ya Nyakati 1 sura ya 6 mstari wa 19 unasema

"Wana wa Merari walikuwa Mali na Mushi. Na hizi ndizo zilizokuwa familia za Walawi kulingana na mababu zao":

Lawi au walawi ni watu gani katika historia ya biblia?
Wametoka katika ukoo wa Aroni (au Haruni), aliyekuwa wa kabila la Lawi. Kitabu cha mambo ya walawi kinaelezea amri na maagizo ya Mungu kwa Wanaisraeli hasa sheria za ibada zenye kulenga utakatifu wa makuhani na wa sadaka.


Tujadiliane:
Tunaambiwa katika miaka hiyo ya uhamisho wa babilon Mushi na wana ukoo wake alikuja na kuishi katika mlima kilimanjaro; walizaliana sana sana wengine wakawa upande wa pili wa milima yaani Kenya hawa ndiyo wakikuyu na wengine wakawa upande huu wa Mlima yaani Tanzania hawa ndiyo wa-Mushi.


Je kuna ukweli hapa? hebu angalia makabla 12 ya wana wa Islaeli je Lawi anaonekana ambaye ndiye Mushi?

Kabila 12 za Israel: Je Lawi yumo?

Makabila hayo yalitokana na wana wa kiume 12 wa babu Yakobo, bin Isaka na mjukuu wa Abrahamu. Ni Yakobo aliyepewa kwanza jina la Israeli.

Ibrahim alimzaa Isaka, Isaka akamzaa Yakobo, Yakobo naye akazaa watoto 12 ambayo ndiyo makabila 12 ya Israel. Kwenye mabano ni maana ya jina:

1. Reubeni (Ona)
2. Simeoni. (Sikia)
3. Lawi. (Ungana)
4. Yuda. (Sifu)
5. Dani. (Haki)
6. Naftali. (Mashindano)
7. Gadi. (Bahati Njema)
8. Asheri. (Heri, Furaha)
9. Isakari. (Ujira, Zawadi)
10. Zabuloni. (Zawadi ya Thamani sana)
11.Yusufu (Ongeza)
12. Benjamini (Mwana wa mkono wa kulia)


Sasa unaona kwamba LAWI kumbe ni mtoto wa tatu wa Yakobo, maana ya jina lake ni Ungana - na ndiyo maana wa-islaeli wakicheza ngoma ya kwao wanaunganisha mikono yao hali kadhaika wachaga ni vivyo hivyo.

Tujadili, yawezekana wenzetu hawa ni WALAWI; wanatokana na mtoto Lawi katika ukoo wa Ibrahimu; Yakobo baba yetu.
 
Last edited:
HOJA ni kwama je wachanga (MUSHI) ni moja na makabila 12 ya wana wa Israeli?
 
Inawezekana maana wachaga tamaduni zao zinaendana na hao walawi
 
Mushi au Kushi? Sijaelewa mkuu
huu ukoo ulikuwa kusini kwa misri ya kale; ndiyo hao hao akina Mushi.

Jina "kusini" laaminiwa limetokana na neno lenye asili ya Misri ya Kale kwa ajili ya nchi ya Kushi iliyokuwepo upande wa kusini wa Misri katika Nubia (au Sudani ya leo) pamoja na Uarabuni ya Kusini.

Jina la Kushi lapatikana pia katika masimulizi ya Biblia likimtaja mmoja wa wana wa Hamu katika kitabu cha Mwanzo 10:16 kama baba wa watu wa Kushi.

Kwa ufafanuzi zaidi kwamba wakushi ni wana wa Israeli basi soma Amosi 9 mstari wa 7

"Je! Ninyi si kama wana wa Wakushi kwangu mimi, enyi wana wa Israeli, asema Bwana? Je! Mimi sikuwapandisha Israeli toka nchi ya Misri, na Wafilisti toka Kaftori, na Washami toka Kiri?"
 
Mbona kuna watu wanaitwa, Benjamin, Israel, Reuben, Naftal ,Yuda nk hawa nao ni waisrael? Sio kila kitu cha kufananishwa
 
Mbona kuna watu wanaitwa, Benjamin, Israel, Reuben, Naftal ,Yuda nk hawa nao ni waisrael? Sio kila kitu cha kufananishwa
hayo ni majina ambayo baba ama mama wa mtoto anaweza kumpatia mwanae; sisi hapa tunaongelea wana wa Lawi ambao Mushi ni mmoja wao. Lawi ni kabila moja kati ya 12 ya wana wa Islaeli.
 
Wachaga kwa kiki siyo mchezo! Naskia pia Bob Marley na Peter Tesha aka Tosh ni wachaga!!! Hahaah
 
Sorry, unamaanisha Mushi ... Huyu wa kibosho ????? Au sijakuelewa vizuri ?
ha ha ha

Mushi ni ukoo mkubwa ulikuwepo karne nyingi nyuma, inasemekana babu yao alikuwa Mlawi wa Kushi, ali-migrate toka Misri ya kale na kuja kuweka makazi yake kilimanjaro; uoto wa asili na hali ya hewa ndiyo vilivyomvutia.

Haya si maneno yangu bali soma vitabu vitakatifu juu ya makabila & koo zilizobarikiwa na Mwenyezi Mungu.
 
hayo ni majina ambayo baba ama mama wa mtoto anaweza kumpatia mwanae; sisi hapa tunaongelea wana wa Lawi ambao Mushi ni mmoja wao. Lawi ni kabila moja kati ya 12 ya wana wa Islaeli.
Hata hilo mushi lilitajwa tu mkuu
 
Back
Top Bottom