tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Subiri kwanza, bado mapema. Cyprian Musiba Majura Muingereza popote alipo anaweza akawa anachekelea kuwa Membe kafariki, hivyo amenusurika kulipa mabilioni aliyokuwa anadaiwa. Anajidanganya sana. Hii ni sawa na kuchekelea kuruka majivu halafu ukatua motoni. Hii ngoma bado mbichi sana!
Hukumu ya kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa na aliyekuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe dhidi ya Cyprian Musiba anayejitambulisha kama mwanaharakati huru, inafikisha jumla ya fidia anazotakiwa kulipa kuwa takriban Sh 18.58 bilioni.
Kiasi hicho anachotakiwa kuwalipa watu aliowakashfu kupitia vyombo vyake vya habari ndani ya miaka sita iliyopita kinamweka katika hatari ya kufungwa jela iwapo atashindwa kukilipa, mawakili wamesema.
Mahakama Kuu ilimwamuru Musiba kumlipa Membe jumla ya Sh 6 bilioni baada ya kumshinda katika kesi ya madai ya kashfa aliyomfungulia.
Mbali na Membe, wakili maarufu nchini, Fatma Karume (aka Shangazi) alisema Mahakama Kuu Zanzibar ilimwamuru Musiba amlipe Sh 12.5 bilioni kwenye kesi yake ya madai ya kashfa aliyomfungulia.
Vilevile, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilishamwamuru Musiba kumlipa waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka fidia ya Sh 80 milioni kutokana na kashfa alizozitoa dhidi yake.
Baadhi ya mawakili walisema endapo Musiba atashindwa kulipa fidia hiyo na hatakuwa na mali za kupigwa mnada kufidia kiasi hicho basi wanaomdai wanaweza kuomba mahakama imfunge kama mfungwa wa madai.
Akitoa maoni kuhusu hukumu hiyo, Wakili Fulgence Massawe alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Madai (CPC), wanaomdai wanaweza kuiomba mahakama impeleke jela.
MAONI YANGU
Musiba aache kusherekea kifo cha Membe badala yake aendelee kulia kwani bado hajapata unafuu wowote. Kwanza kiasi cha fedha anachodaiwa na Shangazi ni kikubwa kuliko alichokuwa anadaiwa na Membe. Na hapo hapo bado hajamlipa mama wa hela ya mboga (Profesa Tibaijuka). Patamu hapo! Akae atulie atie kichwa maji asubiri kunyolewa bila shuruti.