Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Mwanaharakati huru kama anavyojiita, Cyprian Musiba amesema kama mtanzania ameumia sana na matukio ya utekaji na kupotezwa kwa watu hususan tukio la hivi karibuni la kuuawa kwa Ali Mohammed Kibao. Hata hivyo, amesema kama mtanzania anapinga kutumia matukio kama haya kuanza kushambulia watu baadhi ambao hawana makosa yoyote huku akishauri kusubiri ripoti kutoka kwa Vyombo vya Usalama na si kutumia matukio haya kisiasa na kuingiza chuki sababu ya watu binafsi.
Amesema "Ripoti haijatoka hajapelekewa Rais, tayari watu wameshaanza fukuza huyu, fukuza huyu, haiwezekani. Wanachosahau Vyama vya Siasa wanadhani wana Serikali yao na Wananchi wao. Ninachoweza kuwaambia ni kwamba hata ninyi mpo uchi, unaweza kuilaumu Serikali kuwa imefanya jambo fulani kumbe hata ninyi ndio mmefanya. Ninachoshauri tu mkileta tuhuma na kutengenza vipeperushi kuwa fukuza huyu, fukuza huyu hata ninyin mpo uchi. Hata ninyi huko ndani kwenye vyama vyenu kuna kamera zinawaona, mawasiliano yenu wanayaona watu. Mnaweza mkatuhumu watu, hizo tuhuma zikageuka. Mie nawatahadharisha na kuwashauri tu."

Aidha, kuhusiana na tukio la Mzee Ali Mohammed Kibao amesema anashauri yeye kama yeye kuwa kwenye uchunguzi mmoja wa Watu wanaotakiwa kusaidia Polisi ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika kwa sababu yeye ndio alikuwa mtu wa kwanza kutoa taarifa na kuzisambaza.
Amehoji "Nani aliyempa taarifa kuwa huyo jamaa kuwa kuna watu wanamteka? Huyu aliyempa taarifa Katibu Mkuu naya anaweza akasaidia Vyombo vyetu. Huyo aliyotea taarifa kuwa Mzee Kibao ameuawa naye anaweza akasaidia "
Ameongeza kuwa uchunguzi sio kwasababu ya Serikali tu, kwani inaangaliwa nani ameanza kutoa taarifa, kwenye basi kulikuwa na nani?, aliyewasiliana na Mnyika akiwa kwenye basi ni nani? Amesema hayo ni mambo ya msingi sana ya kuzingatia kwa sababu Katibu wa Chama amaeanza kutoa taarifa hivyo asaidie.
Amemalizia "Mimi nashauri hapa si kwa nia mbaya, maana mtaanza kunitukana hapa na kunidhalilisha hapa ila ni kwa nia njema"
Amesisitiza "Lazima tulinde hadhi ya Urais, sio kila Mtu anaweza kuongea ongea tu, unamtukana Rais. Nafuatilia rafiki yangu mmoja yupo CHADEMA, siwezi kumtaja jina yeye kila akiamka ni kumtukana Rais tu, anamtukana tu. Na yupo tu wala hakuna mtu anayemjali. Kwenye page yake yeye ni kumtukana tu lakini la kumshukuru Mungu hakuna anayemjali maana inawezekana anataka akamatwe ila watu wamemwacha hakuna naye mjali na sasa ameanza kuchoka. Sio kila kitu anahusika Rais"