Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MUSOMA VIJIJINI WAENDELEA KUTATUA MATATIZO YANAYOWAKABILI WANAFUNZI WA SEKONDARI ZA KATA
* Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374
* Jimbo lina Sekondari za Kata 25 na 2 za Binafsi. Kwa sasa ujenzi wa sekondari mpya 4 unaendelea kwenye Vijiji vya Nyasaungu, Muhoji, Wanyere na Kisiwani Rukuba.
Jana, Mbunge wa Jimbo hilo, Prof Sospeter Muhongo, alitembelea Kijiji cha Muhoji kwa malengo mawili: (i) kusikiliza na kutatua kero za wanakijiji, na (ii) kukagua ujenzi wa sekondari mpya iliyopangwa kufunguliwa mwakani, Januari 2024.
Tafadhali sikiliza VIDEO/CLIP zilizowekwa hapa - Wananchi wa Kijiji cha Muhoji, Kata ya Bungwema, wenye furaha tele wameanza ujenzi wa Sekondari ya pili ndani ya Kata yao
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumanne, 6.6.2023