Musonda atunukiwa medali na mtoto wa miaka 8

Musonda atunukiwa medali na mtoto wa miaka 8

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Mchezaji wa Yanga Kennedy Musonda leo ametunukiwa medali aliyopewa na mtoto wa kutoka huko Spain aitwaye Lucas Gomez. Medali hiyo ilikabidhiwa kwa Musonda na Balozi wa Spain kwa niaba ya mtoto huyo.

20230313_130953.jpg

Musonda alipata zawadi hiyo kutokana na kuwa man of the match wakati akichezea club yake ya zamani ya Power Dynamos ya Zambia, ila cha ajabu club yake ya sasa ya Yanga Afulika ikateka shughuli hiyo ili kujitafutia kiki.

Haijajulikana huyo mtoto wa miaka 8 ni nani hasa au ana matatizo gani hadi medali yake kuwepa uzito kiasi hicho ila inaonyesha alipendezwa na uchezaji wa Musonda hadi akamchagua kuwa man of the match wakati anacheza huko Zambia na hivyo kumtumia medali hiyo.
 
Leo asubuhi mchezaji wetu Musonda Jr amepata nafasi ya kupokea zawadi ya medali kutoka kwa mtoto Lucas Gomez Usoz kutoka Spain.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 8 anayeishi mjini Madrid nchini Spain alituma Medali hiyo kupitia ubalozi wa Spain (TZ) na kukabidhiwa rasmi leo na Balozi Jorge Moragas mbele ya Rais wa Klabu yetu Hersi Ally Said kama sehemu ya kuvutiwa na uchezaji wa Musonda baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi akiwa anaitumikia klabu yake ya zamani ya Power Dynamos FC ya nchini Zambia.

Hafla hii fupi iliyoandaliwa na balozi ilifanyika kwenye makazi yake eneo la Oyster bay, jijini Dar es salaam.

Source page ya wananchi yanga.
1678702614304.jpg
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]sa hii ndo nini? Haya medali fc
 
Leo asubuhi mchezaji wetu Musonda Jr amepata nafasi ya kupokea zawadi ya medali kutoka kwa mtoto Lucas Gomez Usoz kutoka Spain.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 8 anayeishi mjini Madrid nchini Spain alituma Medali hiyo kupitia ubalozi wa Spain (TZ) na kukabidhiwa rasmi leo na Balozi Jorge Moragas mbele ya Rais wa Klabu yetu Hersi Ally Said kama sehemu ya kuvutiwa na uchezaji wa Musonda baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi akiwa anaitumikia klabu yake ya zamani ya Power Dynamos FC ya nchini Zambia.

Hafla hii fupi iliyoandaliwa na balozi ilifanyika kwenye makazi yake eneo la Oyster bay, jijini Dar es salaam.

Source page ya wananchi yanga.View attachment 2548790
Ila hii timu ina mambo ya kujua wenyewe tu.
 
Kuna mashabiki wa upande wa pili watanuna eti! Huku wakiwa hawana hata sababu ya msingi.
 
ila cha ajabu club yake ya sasa ya Yanga Afulika ikateka shughuli hiyo ili kujitafutia kiki.

Nimeielewa hapo😁🙌
 
Makolo wamechukia eti, walitamani awe mchezaji wao chama mguu mfupi au baleke macho kumchuzi.
 
Aya mambo ni yakawaida, Kuna mwaka kati ya 1987-1992 aliyekua Kiungo wa Yanga na timu ya Taifa Issa Athumani Mgaya aliwahi kupewa tuzo ya uchezaji Bora na Ubalozi wa Urusi apa Tanzania.
 
ila cha ajabu club yake ya sasa ya Yanga Afulika ikateka shughuli hiyo ili kujitafutia kiki.

Nimeielewa hapo😁🙌
Halafu sijaiona hata jezi ya Power Dynamos hapo. Yule dogo hata hajui kama aliuzwa ndiyo maana imechukua muda mrefu zawadi kumfikia.
 
Aya mambo ni yakawaida, Kuna mwaka kati ya 1987-1992 aliyekua Kiungo wa Yanga na timu ya Taifa Issa Athumani Mgaya aliwahi kupewa tuzo ya uchezaji Bora na Ubalozi wa Urusi apa Tanzania.
Hii ya mtoto wa miaka 8 kweli, kabisa hadi Rais wa Club akaacha shughuli zake kuhudhuria? Wachezaji wangekuwa wanaitisha press conference kila wakiandikiwa barua na kupewa zawadi na mashabiki wao, wasingepata hata muda wa kucheza.
 
Back
Top Bottom