SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Pamoja na kwamba Camara ni golikipa mzuri nilishasema zaidi ya mara moja kuwa Lakred asiachwe.
Itakuwa ni kosa kubwa sana na matumizi mabaya ya rasilimali za klabu kumuacha Ayoub Lakred. Simba ndiyo timu pekee duniani ambayo mchezaji akiumia tu anaachwa. Kwa staili hiyo, hauwezi kamwe kujenga timu imara ambayo wachezaji wanacheza kwa moyo wote.
Katika dirisha dogo, Simba iachane na Manula halafu imbakishe Lakred hadi mwishoni mwa msimu kama inawezekana. Kuna dalili fulani za washkaji zake Manula pale nyuma wanaweza kuchomesha ili kumharibia Camara ili jamaa yao arudi langoni.
Simba haimhitaji tena Manula.