Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
The road to hell is paved with good intention.Mussa Zungu, Mbunge wa Ilala amesema haya
Hoja kuhusu viwango vya tozo za miamala ziko juu ni kweli yaani Laki moja inatafutwa kwa mbinde halafu ada inakatwa mara tatu, ndio maana Rais Samia ametoa maagizo kwamba litizamwe wapi tulipokosea.
Hii kodi tumeiweka kwa ajili ya wenye uwezo, kati ya Watu Mil. 50 wanaomiliki line za simu, Watu Mil. 20 tumewatoa hawalipi hii kodi, wanaolipa ni Mil. 30 ambao tunaamini wana uwezo kiasi na tunajuaje wana uwezo ni kwa kupitia TCRA.
Tukisema Tshs. 50 kwa Watu Mil. 30 (wanaolipa tozo za simu) tunapata Bil. 540. Tukiweka Tshs 100 tunapata Tril. Moja na Bil. 80 haya ni mapato ambayo yatasaidia kuchochea maendeleo ya Nchi yetu.
Kuwa na ada ya simu ni uzalendo leo hatuandiki barua, hatuna gharama ya stempu, leo Mtu yupo Mwanza anauliza Soko la Pugu ni shilingi ngapi, anauliza soko la samaki ni shilingi ngapi, hii ni nafasi nzuri tuwe na kodi ya uzalendo.
My Take
Kwa wabunge kama hawa ilikuwa sahihi Magufuli kuwa analishauri bunge badala ya bunge kumshauri yeye. Hatuna bunge
Binafsi nipo kwenye sekta ya utalii, lakini sijawahi kumsikia mgeni akilalamika kwanini kusiwe na one price as entrance fees to all parks and attractions. Kumbuka, cost nzima sio entrance tu, hapo wanachoweka cha juu sana ni ma tour operator na hotel anayokaa ndani ya mbuga. Hakuna mgeni aliekuja TZ kutembea mbugani akashindwa $100 entrance to have a lifetime experience.Kunasiku nilisema utalii ukitumika vizuri utaikwamua nchi, mfano kwa sasa hivi gharama za utalii nikubwa na zinapelekea kupata mapato kiduchu
Suluhisho ni kuwa na package moja tu mfano Dolla 500 ambayo mtalii akiilipia ndani ya wiki mbili anaweza tembelea kivutio chochote kile kilichopo Tanzania na Zanzibar akitaka kuongeza siku baada ya siku 21 analipia Tena dolla 500
Tozo zikiwa ndogo watalii watakuja wengi sababu Kuna unafuuu lakin Kilimanjaro bei yake, ngorongo bei yake, Serengeti bei yake, Zanzibar bei yake angalia huu usumbufu watalii wanaoupata ni wazi viongozi wa ccm sio wabunifu hata kidogo
Kama kawaida sisi tunasugua magoti kumlilia Mungu. Wao wana mitutu ya bunduki sisi tuna MunguView attachment 1878384
Kwa kweli hatuna wabunge wala wataalamu wa kufikiria nje ya box jinsi ya kutafuta vyanzo vya mapato kwa serikali..Mussa Zungu, Mbunge wa Ilala amesema haya
Hoja kuhusu viwango vya tozo za miamala ziko juu ni kweli yaani Laki moja inatafutwa kwa mbinde halafu ada inakatwa mara tatu, ndio maana Rais Samia ametoa maagizo kwamba litizamwe wapi tulipokosea.
Hii kodi tumeiweka kwa ajili ya wenye uwezo, kati ya Watu Mil. 50 wanaomiliki line za simu, Watu Mil. 20 tumewatoa hawalipi hii kodi, wanaolipa ni Mil. 30 ambao tunaamini wana uwezo kiasi na tunajuaje wana uwezo ni kwa kupitia TCRA.
Tukisema Tshs. 50 kwa Watu Mil. 30 (wanaolipa tozo za simu) tunapata Bil. 540. Tukiweka Tshs 100 tunapata Tril. Moja na Bil. 80 haya ni mapato ambayo yatasaidia kuchochea maendeleo ya Nchi yetu.
Kuwa na ada ya simu ni uzalendo leo hatuandiki barua, hatuna gharama ya stempu, leo Mtu yupo Mwanza anauliza Soko la Pugu ni shilingi ngapi, anauliza soko la samaki ni shilingi ngapi, hii ni nafasi nzuri tuwe na kodi ya uzalendo.
My Take
Kwa wabunge kama hawa ilikuwa sahihi Magufuli kuwa analishauri bunge badala ya bunge kumshauri yeye. Hatuna bunge
Natural resource curseHuyu jamaa ni wa ovyo sana tena sana...
Yani nchi hii ni minerals zote tulizo nazo, na vivutio vya utalii tumeshindwa kujenga nchi hii mpaka watukamue. Kuna nchi zina deposite ya madini aina moja tu, lakini watu wanasoma bure, huduma ya afya bora sisi tuna kila aina ya madini lakini serikali ya CCM kwa miaka zaidi ya 50 haijui ifanye nini ili tuendeleee.
Kila awamu wanatudanganya oooh gas asilia ipaisha uchumi, oooh inabidi tukatwe kodi ya uzalendo.