MUST WATENGENEZA KIFAA CHA AJABU: MAMA AKIWA KIJIJINI DAKTARI ANAMUONA MOJA KWA MOJA - WAZIRI MKENDA ASHANGAA!

focaltz

Member
Joined
Aug 26, 2026
Posts
6
Reaction score
1
MBEYA - Bunifu mpya kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) inatarajiwa kuleta mapinduzi katika huduma za afya ya uzazi nchini, baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda kuupongeza na kuuita mfumo utakaokosha Taifa.

Akizungumza alipotembelea bunifu za wanafunzi wa MUST tarehe 09/10/2026, Prof. Mkenda alishuhudia maonesho ya kifaa kinachoitwa MAMA-SAFELIFE ambapo inajumuisha kifaa na mfumo wa ufatiliaje wa afya ya mama na mtoto, kilichobuniwa na mwanafunzi wa Biomedical Engineering, Gibons Jack Mwasabwite.
KIFAA NI NINI?

Mfumo huo unaunganishwa na mtandao wa GPRS kutuma taarifa moja kwa moja hospitalini, una mfumo wa kuchaji kwa nishati ya jua (SOLAR) na kitufe cha dharura cha SOS kinachotuma ujumbe na eneo la mama alipo (GPS) anapohitaji msaada wa haraka.

"Kifaa hiki kimebuniwa kwa ajili ya mama aliyeko mjini na kijijini Tunduma, Sumbawanga au Mtwara ambaye yuko mbali na hospitali dharula inapotokea tahadhari. Daktari anaweza kumuona akiwa live akiwa Dar es Salaam," alisema Mwasabwite.

Waziri Mkenda amesema wizara yake itaendelea kuunga mkono bunifu kama hizo ambazo zinagusa maisha ya wananchi moja kwa moja, huku akiwataka wadau kuunga mkono juhudi

Instagram%20-%201791556973173(JPG).jpeg
Bunifu%20zinazofanywa%20na%20wanafunzi%20na%20watafiti%20wa%20Chuo%20Kikuu%20cha%20Sayansi%20...jpeg
Instagram%20-%201791556973181(JPG).jpeg
 
MBEYA - Bunifu mpya kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) inatarajiwa kuleta mapinduzi katika huduma za afya ya uzazi nchini, baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda kuupongeza na kuuita mfumo utakaokosha Taifa.
Akizungumza alipotembelea bunifu za wanafunzi wa MUST tarehe 09/10/2026, Prof. Mkenda alishuhudia maonesho ya kifaa kinachoitwa MAMA-SAFELIFE ambapo inajumuisha kifaa na mfumo wa ufatiliaje wa afya ya mama na mtoto, kilichobuniwa na mwanafunzi wa Biomedical Engineering, Gibons Jack Mwasabwite.
KIFAA NI NINI?

Mfumo huo unaunganishwa na mtandao wa GPRS kutuma taarifa moja kwa moja hospitalini, una mfumo wa kuchaji kwa nishati ya jua (SOLAR) na kitufe cha dharura cha SOS kinachotuma ujumbe na eneo la mama alipo (GPS) anapohitaji msaada wa haraka.

"Kifaa hiki kimebuniwa kwa ajili ya mama aliyeko mjini na kijijini Tunduma, Sumbawanga au Mtwara ambaye yuko mbali na hospitali dharula inapotokea tahadhari. Daktari anaweza kumuona akiwa live akiwa Dar es Salaam," alisema Mwasabwite.

Waziri Mkenda amesema wizara yake itaendelea kuunga mkono bunifu kama hizo ambazo zinagusa maisha ya wananchi moja kwa moja, huku akiwataka wadau kuunga mkono juhudi
well done G.K.Mwasabwite 💪
 
well done G.K.Mwasabwite 💪

Tlaatlaah Asante sana mkuu kwa ku-share na kwa support. 🙏

Ndugu zangu JamiiForums, asanteni kwa support. MAMA-SAFELIFE ni kwa ajili yetu sote. Hakuna mama anastahili kufaa kwakukosa msaada wa ufatiliaji
 
Back
Top Bottom