Mustafa Mkolo amuombe radhi Zitto Kabwe

Mustafa Mkolo amuombe radhi Zitto Kabwe

Hapo kwenye RED, mi nafikiri kwa sasa mawaziri wote wa JK wamezishindwa wizara zao, sio Mkulo tu. Inahitajika total reformation ya Serikali nzima kuanzia kwa Pinda mpaka kwa Hawa Fujo (a.k.a Hawa Ghasia).

Umekosea. Si mawaziri tu, kuanzia Rais na Baraza lake la mawaziri lote limeshindwa kazi. Nawashauri wajiuzulu tufanye uchaguzi mwingine haraka iwezekanavyo.
 
kufilisika kwa nchi nilazima waziri wa fedha, gavana kamishena wa tra kitily wajiuzur maana wanaandaa bajeti tata.
 
Watanzania woote tana haki ya kuombwa radhi na Mkulo. MAGAMBA ndio wajue wenzao wa CDM wanaona mbali kabla ya wao kupata tatizo tayari Mh Zitto alishaliona hilo. Vijana tunaweza.
 
Serikali yetu haiwezi kukiri udhaifu wake hata siku moja, kwa hiyo hata mkulo hawezi kuomba radhi kwa sababu hana tendency. Yeye kila kitu anasema Zitto ni muongo bila kujua kuwa yeye ndio anaoneka muongo mbele ya wananchi
zitto kwenye UKWELI hasubiri ruhusa kuusema,Alimlipua karamagi akafukuzwa bungeni mwishowe ikabainika mkataba wa buzwagi ulisainiwa hotelini,aliwaambia chadema kutokumtambua jk sio sahihi as tutakwama kuendesha siasa akazongwa mwishoni wamekubali kimya kimya,alisema kisheria kuvunja mkataba wa DOWANS ni makosa KISHERIA wakabisha wanasheria uchwara mishowe tumeshindwa kwenye kesi ngazi ya kitaifa na kimataifa,alitangaza serikali ni muflis wakabisha mwishoni sasa wanakubali,alianzisha rasmi mjadala wa kupinga posho ya makalio sasa tumefikia sehemu kila mtu anamtupia zigo mwingine,alikanusha rais kusign posho gugumaji NKAMIA akaja juu sasa kaumbuka,tangu amekuwa MWENYEKITI WA KAMATI MUHIMU YA bunge hata maadui zake wamekubali dogo jembe,anapigwa vita na watu wa CCM na CDM but dogo bado yupo juu,Said kubenea kwenye kipeperushi chake juzi kaacha kuandika mgomo wa madaktari,nyongeza ya posho anakwenda kuandika habari isiyo na maslahi kwa chama chake wala TAIFA kisa ZITTO achafuke.ZITTO kaza buti tumia muda mwingi kwenye tafiti zako badala ya kuiga wenzako wanaoshinda kwenye vibaraza vya wanahabari kuuza mafuvu yao!!!
 
Tanzania kwa sasa hatuna viongozi,ila tuna viranja tu,taifa la Tanzania linaongozwa na MUNGU, viranja vilivyowekwa ni vibaka.
 
ZITTO KABWE ni noma jana kuna radio moja uku mkoani ninapoishi walikua wanachambua ishu ya posho hasa migogoro iliyopo kati ya MAKINDA,PINDA,na JK...Walisema hao waliokua wana host kipindi plus na wachangiaji kua inawezekana vipi MAKINDA na PINDA wanasema RAIS kabariki posho kwa kuzisaini bungeni baadae ZITTO akasimama akasema kwa taarifa alizonazo RAIS hajasaini baada ya muda IKULU ikawaua kabisaaaa wakina PINDA,MAKINDA kua RAIS hajasaini wala hajaidhinisha hizo posho....wachangiaji wengi walisema inamana ZITTO anajua taarifa za serikali kuliko ata waziri mkuu na spika wa bunge?
 
Hawezi coz atasema kuwa serikali parse haijatamka kuwa imefilisika!

Nasasa Mh. Rais amekwishatamka kuwa serikali yake imefilisika, kama kiongozi mkuu wa serikali hiyo ni statement ya serikali. Hivyo ni budi Mh. Mustafa Mkulo amuombe radhi Zitto Kabwe kwa kumdhalilisha kutu,ia dhamana yake serikalini. La sivyo, sitakaa niamini chochote ndani ya serikali hii tata.
 
Back
Top Bottom