Mustafa Mkulo atoka mbio kukwepa ghadhabu ya wananchi Dumila

Mustafa Mkulo atoka mbio kukwepa ghadhabu ya wananchi Dumila

MPANDA Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2011
Posts
1,295
Reaction score
159
Wana bodi,

Naamini wengi mnapajua Dumila. Mji huu upo katka wilaya ya Kilosa, jimbo linaloongozwa na Mustapha Mkulo.
Leo hii takriban saa moja lililopita Mhe. Mkulo amelazimika kukimbia kabisaaa (Namaanisha kukimbia) pale wananchi wa mji huu walipoanza kupaza sauti za kumzomea baada ya kutoa majibu mabaya juu ya mradi wa maji ambao yeye aliahidi kutoa Tsh 5,000,000 toka katika Mfuko wa Jimbo tangu mwaka 2011 lakin hadi leo hajatoa na aliwahi kunukuliwa akisema hatatoa kwa madai kwamba alitukanwa na katibu wa CCM wa wilaya.

Majibu yake kwamba "... sitoi hela mpaka katibu aniombe msamaha kwa maandishi..." ndo yakaibua hasira za wananchi ambao mwaka huo wa 2011 walilazimishwa kwa vipigo kutoa kila mtu Sh 3500 tofauti na makubaliano ya kuchangia sh 2000 kwa kaya... pesa ambazo nazo zimeliwa.

Mkulo kadandia gari yake aina ya Range Rover Vogue na kutimka.

Nikiweza ntaleta picha
 
Nimependa sana ujasiri wa wananchi..iwe wembe huo huo utumike kwa wabunge wote wasio timiza ahadi zao.
 
Jamaa huyu alikuwa na majibu ya hovyo sana akiwajibu wananchi wa kilosa ni mpuuzi sana huyu.
 
kwani HAO WAPIGAKURAWAKE hawakuwa na mawe????
wangemsindikiza kwa mawe ingekuwa vizuri zaidi
Hawawanasiasa wanashindwa tambua kwamba jamii ya leo sio ile ya miaka ya 40
Akirudi bora mpige mawe kabisa
 
Aise..Watanzania wamechoka na ahadi hewa.
 
Yani ma ccm yanafanya maendeleo ya wananchi kama vile ni mambo ya nyumba ndogo!Katibu ccm anauhusiano gani na maji?M4c jimbo hilo lipo wazi
 
apigwe tu wananchi wamechoka sasa wameamua kutekeleza sera ya waziri mkuu aliyoitoa bungeni "tumechoka wapigwe tu" na bado mwaka huu wabunge wengi wa magamba watapigwa sana na wananchi kwa kushindwa kutekeleza ahadi walizozitoa wakati wa kampeni.
 
Wana bodi,

Naamini wengi mnapajua Dumila. Mji huu upo katka wilaya ya Kilosa, jimbo linaloongozwa na Mustapha Mkulo.
Leo hii takriban saa moja lililopita Mhe. Mkulo amelazimika kukimbia kabisaaa (Namaanisha kukimbia) pale wananchi wa mji huu walipoanza kupaza sauti za kumzomea baada ya kutoa majibu mabaya juu ya mradi wa maji ambao yeye aliahiti kutoa Tsh 5,000,000 toka katika Mfuko wa Jimbo tangu mwaka 2011 lakin hadi leo hajatoa na aliwahi kunukuliwa akisema hatatoa kwa madai kwamba alitukanwa na katibu wa CCM wa wilaya.

Majibu yake kwamba "... sitoi hela mpaka katibu aniombe msamaha kwa maandishi..." ndo yakaibua hasira za wananchi ambao mwaka huo wa 2011 walilazimishwa kwa vipigo kutoa kila mtu Sh 3500 tofauti na makubaliano ya kuchangia sh 2000 kwa kaya... pesa ambazo nazo zimeliwa.

Mkulo kadandia gari yake aina ya Range Rover Vogue na kutimka.

Nikiweza ntaleta picha
Aibu,..... mmechagua fisadi mnavuna ufisadi
 
Kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Sijui Ule uwaraza aliutia wigi ? maana ni aibu sana mwenye upara kutoka nduki .
 
Yaani huo mradi wa maji wanataka kuufisadi kama ule wa Karatu alivyoufisadi Dr. Slaa.

Maji ni UHAI...
 
Back
Top Bottom