Mchaka Mchaka
JF-Expert Member
- Jul 20, 2010
- 4,517
- 1,407
Na hao wananchi wapigwe tu, maana tumeshachoka...M.P.K.PINDA(MB) - 2013
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wana bodi,
Naamini wengi mnapajua Dumila. Mji huu upo katka wilaya ya Kilosa, jimbo linaloongozwa na Mustapha Mkulo.
Leo hii takriban saa moja lililopita Mhe. Mkulo amelazimika kukimbia kabisaaa (Namaanisha kukimbia) pale wananchi wa mji huu walipoanza kupaza sauti za kumzomea baada ya kutoa majibu mabaya juu ya mradi wa maji ambao yeye aliahidi kutoa Tsh 5,000,000 toka katika Mfuko wa Jimbo tangu mwaka 2011 lakin hadi leo hajatoa na aliwahi kunukuliwa akisema hatatoa kwa madai kwamba alitukanwa na katibu wa CCM wa wilaya.
Majibu yake kwamba "... sitoi hela mpaka katibu aniombe msamaha kwa maandishi..." ndo yakaibua hasira za wananchi ambao mwaka huo wa 2011 walilazimishwa kwa vipigo kutoa kila mtu Sh 3500 tofauti na makubaliano ya kuchangia sh 2000 kwa kaya... pesa ambazo nazo zimeliwa.
Mkulo kadandia gari yake aina ya Range Rover Vogue na kutimka.
Nikiweza ntaleta picha
Huo ni uongo kabisa. Hata ukimdanganya Mtoto aliyetumboni mwa mama yake ataukataa na ataanza kucheza tumboni mwa mama yake kupinga uongo kama huo. Sijui kama unasema uongo kiasi hicho watoto wako wanajifunza nini kutoka kwako. Kwanza haiingii akilini uongo wako huo kugeuka ukweli.
Bila kumtaja Dr. Slaa hupati raha hehhh!!!!
Huo ni uongo. Si kweli.