Musukuma aitaka Serikali kufungua viwanda ilivyofunga

Musukuma aitaka Serikali kufungua viwanda ilivyofunga

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma ameitaka Serikali kufungua Viwanda ilivyofunga akisema wengine walionyang'anywa wana uwezo, na waliosababisha Viwanda vifungwe ni Serikali kushindwa kulinda Soko la Ndani

Amesema, "Nikuombe Waziri, dhambi hii ya kupora vitu vya watu isikuangukie mikononi mwako. Kama Serikali imeanza kufungua Akaunti, kaa na Katibu wako mfungue hivyo Viwanda. Wapeni muda mambo yaendelee"
Kwani wakati vinaporwa hakuwepo? Je yeye hakuwa miongoni mwa wacheza ile ngoma wakati wamiliki wakiporwa haki zao? Wanafiki sasa wanajianika...
 
K

Kila ninapopita nje ya kiwanda cha tumbaku Morogoro na kiwanda cha Mazava Msamvu, huwa nabubujikwa na machozi. Ifike mahali nchi ipitishe sera ya kuwapima watia nia wetu kama "they are upstairs ok"
Yaani inasikitisha...mie nakumbuka kile kiwanda cha kusindika nyama, kilichojengwa Shinyanga, kuwa karibu kabisa na ukanda wenye mifugo kilikuwa hata kabla ya kuanza.... nasikia sasa wamegeukia kuanzisha kipya cha wachina cha kuchinja punda.....haya bwana..na kazi iendelee.
 
K

Kila ninapopita nje ya kiwanda cha tumbaku Morogoro na kiwanda cha Mazava Msamvu, huwa nabubujikwa na machozi. Ifike mahali nchi ipitishe sera ya kuwapima watia nia wetu kama "they are upstairs ok"
Wakulima wa malighafi wahamasishwe, waanze kulima tena, watu walishaacha kulima, ilionekana haina wateja wala faida.
Makampuni mengi yanayochakataa tumbaku yalienda nchi jirani.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kila ninapopita nje ya kiwanda cha tumbaku Morogoro na kiwanda cha Mazava Msamvu, huwa nabubujikwa na machozi.
Kumbe nacho kilifungwa kwa hila, nikajua kilifungwa kwa ajili ya corona kama walivyosema wanasiasa
 
Mbona sielewi serikali ya viwanda imefungia viwanda ?

Si tulikuwa tunafungua viwanda vingi na kutengeneza ajira kwa wingi ?
 
Viwanda vyote vilishauzwa! Sasa Serikali ifufue viwanda gani? Na nyumba za Serikali zilishauzwa na Serikali ikajipatia pesa, tatizo liko wapi!!! Haya mambo ya maendeleo ya NCHI yanahitaji uzalendo wa KWELI. Rais anakuwa madarakani zaidi ya miaka 20, anajenga mashule nchi mzima na wanafunzi wote hadi Chuo Kikuu wanasoma BURE. Anajenga mahospitali na wananchi wanatibiwa BURE. Katika mkakati wa create employment anajenga viwanda, makanpuni, mahotel, barabara, miundombinu ya umeme, e.t.c kwa UZALENDO wa hali ya juu hadi anasahau kujenga nyumba yake ya kuishi baada ya kustaafu. Huyo ndio Rais mwajiliwa wa wananchi. Leo kila anayekuja anastsili yake. Huyu nawajengea marais wenzake nyumba za kifahari utadhani hawana nyumba hizo. Mwengine....., wakati hali ya NCHI inahitaji mambo mengi ya maendeleo hasa kwa kwa ajili ya vivazi vijavyo. WABUNGE TUJISAHIHISHE WAKATI TUNAO.
 
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma ameitaka Serikali kufungua Viwanda ilivyofunga akisema wengine walionyang'anywa wana uwezo, na waliosababisha Viwanda vifungwe ni Serikali kushindwa kulinda Soko la Ndani

Amesema, "Nikuombe Waziri, dhambi hii ya kupora vitu vya watu isikuangukie mikononi mwako. Kama Serikali imeanza kufungua Akaunti, kaa na Katibu wako mfungue hivyo Viwanda. Wapeni muda mambo yaendelee"
Naunga mkono hoja ya Msukuma lakini wakati huohuo nahoji credibility ya bunge letu.
-Je, hawakujua wakati wote kuwa viwanda hivyo vilifungwa kwa uonevu?
- Ili wabunge waongee ukweli unaowaumiza wananchi ni mpaka raisi aondoke madarakani au afariki wakati tunaaminishwa kuwa bunge ni chombo huru?
 
Mkuu kwa Bunge gani? Hili la lililoingia kwa kimbunga cha Tsunami? Lenye wabunge ambao hawana chama, wabunge wa kuteiliwa na Spika wa Bunge. UTAJICHELEWESHA
 
Back
Top Bottom