Musukuma ataka machinga wasibugudhiwe. Asema Serikali imechuma Bilioni 43 kwenye Vitambulisho

Musukuma ataka machinga wasibugudhiwe. Asema Serikali imechuma Bilioni 43 kwenye Vitambulisho

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
BUNGENI: Mbunge Joseph Kasheku Musukuma amesema Machinga anaposumbuliwa na kuharibiwa Biashara, Taasisi za Kifedha nazo zinaharibiwa.

Amesema, "Kuna watu wako pale wana mikopo, wamekopeshwa wana marejesho. Tuna shida gani tukisema magari yasiingie Kariakoo ili iwe kitovu cha Biashara? Watu wafanye kwa uhuru wasibugudhiwe"
 
Amos Makalla ameshindwa kuwatoa machangudoa alafu eti anataka apambane na machinga wanaojipatia kipato halali na kodi wanalipa!!!

Ngoja tumuone mwisho wake
 
Amos Makalla ameshindwa kuwatoa machangudoa alafu eti anataka apambane na machinga wanaojipatia kipato halali na kodi wanalipa!!!

Ngoja tumuone mwisho wake
Akili za kimwendazake hizi, very primitive creatures
 
Eti magari yasiingie Kariakoo ili machinga watumie barabara kufanya biashara????
Hizi bangi sio poa. Ambulance, fire, Polisi, Kirikuu za kubeba mizigo, gari za abiria zote zisiingie??? Hili bunge lina vituko sana.
 
BUNGENI: Mbunge Joseph Kasheku Musukuma amesema Machinga anaposumbuliwa na kuharibiwa Biashara, Taasisi za Kifedha nazo zinaharibiwa.

Amesema, "Kuna watu wako pale wana mikopo, wamekopeshwa wana marejesho. Tuna shida gani tukisema magari yasiingie Kariakoo ili iwe kitovu cha Biashara? Watu wafanye kwa uhuru wasibugudhiwe"
Wangeendelea tu kukaa kambi za kusafisha barabara na reli. Biashara inataka mpangilio si ya kuweka kila mahali inaonyesha jinsi tulivyo na wabunge wa ovyo. Aeleweshwe juu ya mipango miji
 
Kama vipi ndani ya Kariakoo itengwe mitaa mikubwa 2 kwaajili ya machinga tuu.

Kwingine wasiruhusiwe.
 
Round hii Machinga kazi wanayo daaah, JAH awasaidie tyuuh kwa kweli.
 
Kwa hiyo sababu wameingiza hizo bilioni kadhaa ndio wasibugudhiwe? Basi na akina manji walipakodi wakubwa nao wasibughudhiwe ili twende sawa.

Hatuwezi kuwa na lawless nation yani watu wajiamulie tu, basi na wafanyakazi nao wataomba wasibughudhiwe maana Kodi inayokatwa kwenye PAYE ni maradufu ya hao machinga, pia na wakulima sasa sijui tutakuwa na nchi ya aina gani🤷
 
binafsi kwa uelewa wangu sijawahi kubali na sitokubali ile hali ya kuruhusu machinga anamwaga nguo na vitu vingine chini mbele ya duka ambalo linauza vitu ka hivyo. Machinga kariakoo wametapakaa kila mtaa kila mbele ya duka yani sijui nani atalipa kodi ya TRA na PANGO LA NYUMA, hayo yalikuwa mawazo mabaya sana ya kurasimisha machinga pale kariakoo,
Machinga waende Machinga complex maana pale palitengenezwa kwaajili yao. Watu wameshindwa kusimamia hilo yale majengo ya machinga complex yanaenda kuwa magofu sasa
 
Back
Top Bottom