Tatizo la nchi hii ni kuwa wafanyakazi wa serikali wanaobuni Sheria hizi na kuzipeleka bungeni zipitishwe kwanza ni maskini wa mali na roho na pili hawajawahi kushiriki shughuli wanazozibunia Sheria kama kilimo, ufugaji, biashara nk. Hivyo mara zote hubuni Sheria kandamizi.
Ndiyo sababu watumishi hawa wakistaafu hawawezi kuendeleza shughuli au kazi za taaluma zao. Mfano ofisa wa TRA akistaafu hawezi kufanya biashara kwa kuwa kodi alizozibuni hawezi kuzilipa kutokana na biashara yake. Vivyo hivyo kwa taaluma nyingine.