PreGE2025 Musukuma: Wanaharakati wa Kenya na Uganda mliwarudisha wa nini? Wangepelekwa kulima mashambani

PreGE2025 Musukuma: Wanaharakati wa Kenya na Uganda mliwarudisha wa nini? Wangepelekwa kulima mashambani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyu mbunge alichachaguliwa na watu au alijichagua mwenyewe
ni aibu anaongea ujinga mtupu!
 
Ukikosa ELIMU basi uwe na Akili sasa msukuma Hana vyote ndio maana tunasema KATIBA NI MUHIMU ili kuondokana na MBUZI KAMA hawa akina Msukuma.
Inasikitisha sanaa na kushangaza sijaona baya lolote alilo zungumza ASKOFU GWAJIMA.

Siku mtoto wa msukuma akitobolewa macho ndipo atayakumbuka haya maneno ya GWAJIMA

Kama Kuna mtu ana access na watoto wa msukuma tunaomba asogezewe hiyo HUDUMA then arud Tena kuongea ALICHO kiongea.

GWAJIMA katoka data za watu kuumizwa/ kutekwa na hata kupotezwa MSUKUMA YEYE ANAONGEA KI CHAWA YAANI ANATETEA TUMBO LAKE..
 
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Musukuma ameshangaa Mamlaka ya Uhamiaji kuwarudisha Wanaharakati wa Kenya na Uganga nchini kwao, amedai wangepelekwa kulima masmbani.

Musukuma amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kuwashughulikia wanaharakati wa Kenya wanaokuja nchini kufanya majaribio ya kuvuruga amani.

Akichangia hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi bungeni jijini Dodoma, Mei 26, 2025 amesema wanasiasa nchini hawapaswi kuingilia maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimtaja Mbunge wa Kawe Askofu Joseph Gwajima kuingilia maamuzi ya Rais Samia kwa kutumia upole wake, kwani ni kuvuka mipaka na kuingilia mamlaka na kuliomba Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua wote wanaoingilia mamlaka.


Sijajua ni kwa nini vilaza wanajiamini sana kuliko werevu!
 
Back
Top Bottom