Tetesi: Muswada fao la kukosa ajira

Tetesi: Muswada fao la kukosa ajira

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
854
Muswada wa Sheria ya Fao La Kukosa Ajira Huu Hapa

Ule mbadala wa fao la kujitoa ambao umekuwa ukisemwa na mamlaka ya udhibiti na uendeshaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini SSRA, na wakati fulani waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu (sera, uratibu na bunge), Jenista Mhagama sasa umepatikana.

Tarehe 12/Mei/2017, waziri huyo mwenye dhamana ya wizara inayohusika na masuala ya ajira na vijana--alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba fao la kujitoa kwa sasa limefutwa na badala yake kutakuwa na fao la kukosa ajira.

Mbali na waziri Mhagama, pia Rais John Pombe Magufuli naye alilizungumzia fao la kukosa ajira kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani zilizofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro, tarehe 1/Mei/2017. Katika kulizungumzia fao la kukosa ajira Rais Magufuli aliwatoa wasiwasi wafanyakazi akiahidi kwamba mambo yatakuwa mazuri.

Ufuatao ni muswada na utaratibu wa fao la kukosa ajira (unemployment benefits) kwa mifuko yote ya jamii nchini, ambayo inadhibitiwa na kusimamiwa na mamlaka ya SSRA.

Kwamba, iwapo mtu atapoteza ajira, kwa mujibu wa muswada huu ambao kama utatiwa saini na Rais ndiyo itakuwa sheria, ni kuwa mfuko husika mfano NSSF, PPF au LAPF unalazimika kumlipa mwanachama wake asilimia kumi na nane na nusu (18.5%) ya mshahara wake wa mwisho kwa kipindi cha miezi sita.

Ikitokea mwanachama huyo hajapata ajira baada ya kipindi hicho cha miezi sita tangu kupoteza ajira, basi mwanachama huyo atalipwa asilimia kumi na sita na nusu (16.5%) ya salio lililobaki kutokana na malipo ya asilimia kumi na nane na nusu (18.5%) yaliyofanyika kwa miezi sita.

Mfano unalipwa mshahara wa Tsh. 300,000/- (laki tatu), basi hesabu yake ni asilimia kumi na nane na nusu (18.5%) ya Tsh. 300,000/- (laki tatu) kwa kila mwezi kwa miezi sita.

Na ikitokea kwa bahati mbaya mwanachama hakupata ajira baada ya miezi 6, basi mfuko unamlipa mwanachama huyo asilimia kumi na sita na nusu (16.5%) ya kiasi kilichobaki baada ya malipo ya asilimia kumi na nane na nusu (18.5%) yaliyofanyika kwa miezi sita.

Mfano salio lako ni Tsh. 2,000,000/- (milioni mbili) baada ya kulipwa asilimia kumi na nane na nusu (18.5%) kwa miezi sita, basi asilimia kumi na sita na nusu (16.5%) ya hiyo milioni mbili iliyobaki, ndiyo mwanachama atapewa na kiasi kitakachobaki kitakuwa granted kwa mwanachama pale atakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiyari au lazima--miaka 55 ama--miaka 60; vinginevyo mwanachama aendeleze uanachama atakapopata ajira mpya au kujiajiri.

Kwa mujibu wa muswada huu, wale wanaoacha kazi wenyewe (resignation) watapewa asilimia kumi na nne tu (14%) ya michango yao kwa kipindi chote ambacho wamekuwa wakichangia mfuko; na kiasi kitakachobaki kitakuwa granted pale mwanachama atakapofikisha umri wa kustaafu.

Aidha, kwa wale ambao wamechangia mfuko chini ya miezi 18 (kumi na nane) ikitokea wamepoteza ajira kwa kufukuzwa au kupunguzwa kazini, wao watalipwa asilimia arobaini (40%) ya mafao yao na salio litakalobaki litatolewa kwa mwanachama pale atakapofikisha umri wa kustaafu aidha kwa lazima au kwa hiyari.

Muswada huu iwapo ukasainiwa na Rais na kuwa sheria, maana yake sheria hii mpya itakuwa imefuta sheria ya sasa ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo inamruhusu mtu kuchukua mafao yake pale anapopoteza ajira, licha ya kusemwa kuwa sheria hii ilishafutwa.

Kwa mujibu wa sheria ya hifadhi ya mifuko ya jamii ya mwaka 2002, kifungu na: 44 (1) imeainishwa kuwa, ikitokea mtu kapoteza ajira, basi michango yake yote pamoja na ile ambayo mwajiri alikuwa akichangia kwa mfuko kwa ajili ya mtu huyo, itatolewa kwa mtu huyo ambaye kapoteza ajira.

MKANGANYIKO:
Kabla ya muswada huu ambao umevuja, watu walipopoteza ajira na kuamua kufuatilia mafao yao, wamekuwa wakiambiwa kwamba…sheria ya fao la kujitoa imefutwa. Lakini wakati wakiambiwa hivyo, watu ambao wamekuwa wakipunguzwa makazini (redundancy) wao wamekuwa wakipewa mafao yao. Ila kwa wale waliopoteza ajira kwa misingi ya kufukuzwa na mwajiri, wamekuwa wakinyimwa mafao yao kwa sababu ambazo hazikuwa zikiwekwa wazi.

KIMAHESABAU:
Kutokana na ukokotoaji, hesabu zinaonesha kuwa; malipo ya miezi sita yatakayokuwa yakifanywa chini ya mpango huu, pamoja na malipo ya asilimia kumi na sita na nusu (16.5%) ni sawa na mshahara wa mtu kwa miezi miwili na nusu.

Suala la fao la kujitoa lilileta mtafaruku mwishoni mwa mwaka jana hali iliyopelekea shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA chini ya katibu mkuu Nicolas Mgaya, kutamka wazi kuwa shirikisho hilo lingeitisha mgomo wa wafanyakazi nchi nzima, na kuiburuza serikali mahakamani iwapo ingefuta fao hilo la kujitoa ambalo limeonekana kuwa mkombozi kiuchumi kwa wafanyakazi kutokana na mazingira ya ajira nchini kutokuwa rafiki.

Hoja zilizotolewa na TUCTA kutaka fao la kujitoa lisifutwe zilizingatia mazingira ya ajira nchini kwamba, ajira hasa sekta binafsi si za uhakika, malipo kidogo ya mishahara kitu kinachopelekea watu washindwe kuweka akiba hivyo kulifuta fao hilo itakuwa ni kuumiza watu ambao fao la kujitoa hulitumia kujiendeleza kielimu, kujiajiri na hata kujikimu kimaisha.
 
Hivi hawa jamaa wanafikili kila mtu ni mwajiliwa wa serikali ambayo mkataba wake ni permanent &pensionable?? Walio wengi mikataba Hasa ya taasisi binafsi ni mwaka 1 mmoja au 2 miwili tu , na kila mwaka unapoisha mkataba wako una re new na inategemea na mahitaji ya mwajili, sasa mathalani nimemtumikia mwajili wangu miaka 8 afu anasitisha kunipa mkataba Mpya ina maana Pesa yangu ndo wanaanza kuifinyanga finyanga hivyo na hivyo Vip % vyao?

Aisee....kwa mtindo huu watu watazid kukopa uzalendo nchi hii mpaka mwisho wa dahari...
Maana wewe unategemea mtu kama huyo awaelewe Vip??aisee patachimbika
 
Hii mifuko ni chanzo kizuri cha kuwakamua waTanzania ili tujenge flyover zaidi, hii ya Tazara na Ubungo hazitoshi, ziongezwe Tabata, Mwenge, Morocco, Chang'ombe n.k. Serikali ikamue hawa ng'ombe mpaka watoe damu, na hata wakitoka damu iendelee tu kukamua, hakuna namna.
 
Huwa nikiona nyuzi za mifuko ya kijamii napatwa na jazba kama faru John, Naondokewa na uzalendo..


Nimeshajiapiza mwanasiasa yoyote aliefanya maamuzi ya sisi watumwa kunyimwa jasho letu Mungu na Shetani waondoe tofauti zao wawafanyie maajabu hapa hapa duniani.




Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Hiyo 18.5% inatolewa kwenye basic salary au net salary iliyokuwa ikipokelewa na mfanyakazi kipindi akiwa kazini?
 
Hiyo 18.5% inatolewa kwenye basic salary au net salary iliyokuwa ikipokelewa na mfanyakazi kipindi akiwa kazini?
haiko wazi hii, usikute ni net salary, maana hawa watu akili zao wanazijua wao wenyewe...maana mshahara wa mwisho ina maana pana sana bila ufafanuzi.

Senti Fromu Mai Nokia Kitochi.
 
Magufuli akisaini mswaada huu ndiyo nitajua Serikali yake sasa imehamia kwenye dhuluma ya wazi kwa wafanyakazi baada ya bomoabomoa, na wabunge inakuwaje hebu malizia
 
Daah,, sasa na kwa wale ambao wanafanya kazi kwa mda labda wa miaka miwili, harafu anaacha kazi, hicho kiasi kidogo tu cha mafao yake ndo kitagawanywa kingine apewe kingine kibaki Mpaka atakapositaafu!? Bora wangetuachia tu, ukiacha kazi unachukua chako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani hawa wanaharibu pesa ya mwananchama maana kwa style hiyo hata mtu hawezi fanya la maana.
Kinachinishangaz pesa yangu lakini matumuzi nipangiwe it does not make any sense
 
Magufuli akisaini mswaada huu ndiyo nitajua Serikali yake sasa imehamia kwenye dhuluma ya wazi kwa wafanyakazi baada ya bomoabomoa, na wabunge inakuwaje hebu malizia
Tumwombe Mungu 2020 tupate serikali itakayorudisha fao la kujitoa.
 
Magufuli akisaini mswaada huu ndiyo nitajua Serikali yake sasa imehamia kwenye dhuluma ya wazi kwa wafanyakazi baada ya bomoabomoa, na wabunge inakuwaje hebu malizia
Wakati unasubiri ufikishe miaka 55 upate mafao yako wanaamua kubomoa nyumba yako ili ufe mapema usije kusumbua hapo baadae.
 
Taasisi yetu ilifungwa mwezi uliopita,hivyo tukasitishiwa mkataba wa ajira.sasa kasheshe kwenye fao la kujitoa.ukienda NSSF hata form wanakwambia utapewa baada ya miezi 6.ukiwa mkali ndo unapewa form ila wanakwambia uzirudishe baada ya hio miezi 6.wenzetu wa PPF wameshapewa hela yao.NSSF ni mfuko mbovu kuliko yote nchi hii.
 
Ukisainiwa huu mswaada hata sisi wazalendo tutaondoa IMANI na Presidaa
 
Tatizo watanzania ni wajinga,...mambo kama haya ingekuwa nchi za watu pasingekalika sasaivi mtaani
 
Back
Top Bottom