Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nilishangazwa Sana na taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gershon Msigwa, kuwa Serikali imeshindwa kuupeleka Bungeni katika kikao kinachoendelea hivi sasa, muswada wa marekebisho ya Sheria ya huduma za Habari, kwa madai kuwa Bunge hilo limekosa muda wa kuujadili muswada huo!
Hivi huyu Gershon Msigwa, anatufanya watanzania wote ni wajinga?
Nimuulize Mheshimiwa Msigwa, hivi miswada mingapi ya Sheria ilikuwa inapelekea Bungeni kwa kile kinachoitwa hati ya dharula na kupitishwa "fasta fasta" ukiwemo huo muswada wa huduma za Habari, ambao ulipelekwa Bungeni wakati wa utawala wa awamu ya 5, licha ya wabunge "kugomea" kuwa muda waliopewa kuujadili ulikuwa mfupi Sana.
Hata hivyo kauli hiyo ya wabunge walio wengi ikapuuzwa na Serikali na kulazimisha muswada huo ujadiliwe Bungeni na kupitishww Kwa nguvu!
Ingawa najua Serikali hii ya awamu ya 6 imeonyesha nia yake ya kuzirekebisha Sheria zote za ukandamizaji, ikiwemo hii ya huduma za Habari, zilizopitishwa wakati ule wa utawala wa awamu ya 5, lakini naona Bado Kuna "mabaki" ya utawala wa Mwendazake, ambao wanafanya Kila wawezalo kukwamisha juhudi hizi nzuri na zenye maslahi mapana Kwa Taifa hili.
Mungu ibariki Tanzania