Mimi bado nina mashaka na tume iliyoundwa ya kukusanya maoni ya katiba, imetawaliwa na udini sanaaa, hivyo tayari maoni yetu yameanza kuchakachuliwa hatuna imani na matokeo yake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mimi naenda moja kwa moja kwenye mfumo wa serikali tatu kwa kweli serikali ya tanzania ndio serikari inayoendeshwa kwa gharama kubwa sana kwani kuna rais makamu wa rais na waziri mkuu kwa upande wa bara na zanzibar kuna rais makamu wa rais na makamu wa pili wa rais huu mfumo ni mfumoa wa ghali sana sana sana!!!! Tunaomba katiba mpya ifute kipengele cha serikari tatu kwani ni mzigo mkubwa sanaa kwa walipa kodi wanyonge. Nchi hii ni nchi maskini iweje iwe na serikali tatu??? Au itategemea fedha za wafadhili kujiendesha?? Ambapo bajeti yetu kwa 40% hutoka kwa wafadhili je??? Serikari 3 hiyo bajeti itaatosha?? Nawaomba viongozi wetu wananchi hawatki serikari tatu wananchi wanataka huduma bora za jamii kama mashule hospitali ,miundombinu bora, pembejeo za kilimo, maji naswala mengi ya msingi. Napendekeza hivi kuwepo na majimbo mawili tuu tanzania 1-tanganyika litambulike kama jimbo litawaliwe na gavana aishi pale ikulu magogoni 2- zanzabar liatambulike kama jimbo litawaliwe na gavana. Rais awe mmoja tuu na ahamie dodoma kwa makazi ya kudumu hakika huu muungano utakuwa wa bei rahisi sana na kero zote za muungano zitabaki historia kwa ulalamishi wa zanzibari utafika kikomo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.