Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Mwaka 2022 unasomwa kwa mara ya pili Bungeni

Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Mwaka 2022 unasomwa kwa mara ya pili Bungeni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Muswada huu unasomwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye



Lengo la kutunga sheria hii ni kuweka kiwango cha chini cha masharti ya matakwa ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi, kuanzishwa tume ya ulinzi wa taarifa binafsi, kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi wa vyombo vya serikali na vyombo binafsi na maswala mengine yanayohusiana na hayo.

Muswada huu umegawanyika katika Sehemu tisa. Sehemu ya Kwanza yenye vifungu 1 hadi 5 inahusu masharti ya utangulizi yanayojumuisha jina la Muswada, tarehe ya kuanza kutumika kwa Sheria, matumizi, tafsiri, malengo ya Sheria na misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Sehemu ya Pili ya Muswada yenye vifungu vya 6 hadi 13 inahusu masharti ya uanzishwaji na muundo wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na uteuzi wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Tume. Kifungu cha 7 cha Muswada kinaainisha majukumu ya Tume.

Sehemu ya Tatu ya Muswada yenye vifungu vya 14 hadi 21 inahusu masharti ya usajili wa wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi. Aidha, ili kuiwezesha Tume kuwatambua watu wote wanaohusika na ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi, usajili utatofautiana kati ya Taasisi za Umma na Taasisi binafsi kwani kwa mujibu wa kifungu cha 21 cha Sheria.

Sehemu ya Nne yenye vifungu kuanzia 22 hadi 30 inaainisha masharti kuhusu utaratibu wa ukusanyaji, utumiaji na uhifadhi wa taarifa binafsi. Aidha, Sehemu hii inaainisha mazingira ambapo taarifa binafsi zinaweza kufichuliwa. Masharti ya Sehemu hii pia yanazuia uchakataji wa taarifa binafsi nyeti bila ridhaa ya maandishi kutoka kwa mhusika wa taarifa. Taarifa binafsi nyeti zinazorejewa katika Sehemu hii ni pamoja na taarifa zinazohusu watoto, taarifa za kibayometriki, taarifa za kiitikadi za kisiasa na taarifa za kiafya.

Sehemu ya Tano yenye vifungu 31 na 32 vya Muswada inahusu masharti ya usafirishaji wa taarifa binafsi nje ya nchi ambapo dhana ya utoshelevu itatumika kama kigezo kwa nchi ambazo zinaweza kupokea taarifa binafsi kutoka nchini.

Sehemu ya Sita yenye vifungu 33 hadi 38 inaainisha haki za mhusika wa taarifa binafsi ikijumuisha haki ya kupata taarifa zake, kusahihisha taarifa hizo na kuzuia uchakataji.

Sehemu ya Saba yenye vifungu 39 hadi 50 inahusu masharti ya kushughulikia malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa misingi ya ulinzi wa taarifa binafsi kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa kisheria. Inapendekezwa Tume ipewe mamlaka ya kupokea malalamiko, kuyachunguza, kuyatolea maamuzi, na kutoa adhabu ya faini za kiutawala. Aidha, inaweka masharti yanayowezesha muathirika wa vitendo vinavyotokana na ukiukwaji wa Sheria hii kulipwa fidia. Vile vile inatoa pia fursa ya rufaa kwa mtu ambaye hataridhika na uamuzi wa Tume.

Sehemu ya Nane yenye vifungu 51 hadi 57 inaweka masharti ya fedha. Masharti hayo ni pamoja na vyanzo vya mapato ya Tume na utaratibu wa ukaguzi wa hesabu za Tume.

Sehemu ya Tisa yenye vifungu 58 hadi 65 ya Muswada inahusu masharti mengineyo ambayo ni pamoja na masharti kuhusu mazingira yanayopendekezwa kuondolewa katika mawanda ya Sheria.

Muswada huu unapendekeza Sheria tarajiwa kuwa na Jedwali moja ambalo limeandaliwa chini ya kifungu cha 8(6) cha Muswada. Jedwali linaainisha masuala mbalimbali kuhusu Bodi ya Tume ikiwemo muda wa wajumbe kushika nafasi, ukomo wa wajumbe, shughuli za Bodi kutobatilishwa kwasababu ya kasoro, vikao vya Bodi, mgongano wa maslahi, mwaliko wa mtaalamu, akidi, muhtasari wa vikao, uamuzi wa Bodi, na malipo ya wajumbe.

Maoni na Ushauri wa kamati-
  • Serikali iweke wazi vyanzo vya fedha vitakavyotumika kuendesha shughuli za Tume katika kusimamia mambo ya ulinzi wa Taarifa Binafsi.
  • Kwa kuzingatia kwamba, kanuni ni nyenzo muhimu inayofafanua utekelezaji wa masharti ya sheria inayohusika, Serikali isimamie vyema utungaji wa Kanuni za Sheria hii ili zisipishane na dhamira ya Bunge na zisikose uhalisia.
  • Haki ya wahusika wa Taarifa (data subjects) walioachana na taarifa zilizokusanywa kuendelea kuhusishwa na taarifa hizo tofauti na utashi wao izingatiwe katika utekelezaji wa sheria inayopendekezwa. Aidha, Stahili ya Marehemu kuhusu ulinzi wa taarifa zake iwekewe utaratibu wa kuizingatia
  • Ili kuwezesha utekelezaji bora wa Sheria inayotungwa na Bunge, vigezo au sababu zinazoweza kutumiwa kufuta usajili wa Mkusanyaji au Mchakataji wa Taarifa Binafsi viwekwe wazi
  • Kwa madhumuni ya kuzingatia misingi ya utawala bora wakati wa utekelezaji wa Sheria hii, ni vizuri kuzingatia suala la jinsia katika uteuzi wa wajumbe wa bodi.
 
Kwamba mkutano wa bunge wa nne kwa mwaka huu meshaanza?
 
Back
Top Bottom