Muswada wakosa wachangiaji

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
6,997
Reaction score
1,172
Katika hali ya kushangaza, muswada unaohusu hali bora za wanyama, uliowasilishwa hivi punde na magufuli umekosa wachangiaji. Waliokuwa wamejiandikisha kuchangia ni wawili tu-Job Ndugai na mbunge mmoja wa Chadema viti maalum (jina limenitoka) na wote hawakuwepo bungeni wakati ulipofika wa kuchangia!
hali hii ilimfanya spika Sitaa achanganyikiwe hadi Ibrahim sanya (Mji Mkongwe0CUF) alipoibuka ghafla na kusema kuwa atachangia. Hivi ndio sanya anazungumza na Spika anaamini kuwa watajitokeza wengine kuendelea kuchangia!
 
Sanya jamani....
Anasema alitokea mjinga mmoja huko Tarime wakati wa kampeni, akachukua Bendera ya CCM akamvalisha mbwa. Anasisitiza huyo ni mjinga tu, awe wa chama chochote kwa sababu huwezi kutumia mbwa kutafuta umaarufu wa chama.
Anaendelea....
Akatokea mjinga mwingine mkuzwa zaidi akamuua yule mbwa!!!
 

Maneno ya hekima na busara.Namvulia kofia Sanya na wewe ndugu yangu Mpita Njia kwa kunipa hii habari nzuri.
 
Suzan Lyimo naye ameitaka serikali itoe maelezo ya kina kuhusiana na tukio la mbwa kuuawa kwenye kampeni huko tarime.
Pia ameulizia kuna mpango gani wa kuanzisha migahawa na saluni kwa ajili ya wanyama?
 
habib Mnyaa anataka sheria izisuie mchezo wa kupiganisha kuku kwa sababu hata kupiganisha binadamu kunaruhusiwa! Sita anamwambia kwua wanapopiganishwa binadamu kunakuwa na kaununi, lakini kwenye kuku hakuna kanuni na wanaweza kuuawa!
 
very interesting! kwani ni nini kilisababisha (motivation) ya mswada huo? inawezekana magufuli hakushirikisha wadau kabla ya kuuwasilisha bungeni ndo maana kila Mbunge yupo kimya au si wakati wake. Wakati huu ungepwlekwa mswada juu ya kuwasamehe mafisadi wa EPA.
 
Inaonekana wabunge hawapo interested na muswada huo. Ukiachia wachangiaji mandatory, wabunge wa kawaida waliochangia ni wanne tu. Hivi sasa magufuli ndio anajibu hoja zao na kufunga mjadala. nadhani huu utakuwa ni moja ya miswada ambayo imechukua muda mfupi sana kujadiliwa Bungeni
 

I second you,
nadhani hata wabunge wamekuwa demoralized kwa kuona mkuu wao anageuka mtetezi wa wezi, kila mtu angependa kuona usawa na haki kwa binadamu raia wa Tanzania ndilo linalo pewa kipa umbele badala ya haki za wanyama,

Kwa mantiki hiyo wanona ni upuuzi kujadili eti wanyama wawe na haki, wakati hata binadamu wenyewe haki hamna! wezi wa mabilioni hawashitakiwi, ila sheria na magereza zipo kwa ajili ya wezi wakuku na walal hoi tu!
 
Mkuu Mpita Nj....., duh aisee yaani nasoma michango ya waheshimiwa mpaka jamaa hapa pemeni yangu ameshituka manake duh... Hoja za waheshimiwa kwenye huu mswada ni kaazi kwelikweli.... Haya twende tutafika tu...
 
Kwa wenzetu huo muswada ni wa muhimu sana. Huko Netherlands kuna chama kinaitwa Party for Animals kina mbunge mmoja. Huko hata kuchinja na kunyonyoa na kukata kata kuku kwa kutumia mashine ni issue. Huko kuna vegetarians wengi tu, mswada kama huo ungejadiliwa muda mrefu. Hayo ni mageni kwetu kwa sasa lakini kuna siku yatakuja!

......ndiyohiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…