Muuaji wa afisa wa TANAPA Arusha akamatwa


Weledi wa polisi bado una shida kidogo.
Walipoteza ushahidi mzuri sana wa alama za vidole na DNA kwa kulivuta hilo gari.
Sasa tumebakia na maneno ya house boy aliyekiri kumuua boss wake.
Hii inanikumbusha habari ya mkenye aliyejisalimisha baada ya kutekwa kwa ulimboka.
Yaani stori imelembwa ili kusiwe na kinachofuatia.
 
Kuna lingine hapo ''polisi walimwomba mama funguo ya Akiba''!!INA maana alikwenda NATO kituoni?! Magari yetu haya ya mtumba kwanza ni nadra sana kuwa na funguo mbili!!



Ukijumlisha hutakaa upate jibu lenye akili. .
Habari za mjini ni kwamba, mke alikuwa ametengana na mumewe kwa muda mrefu.
 

Nashangaa pamoja na wewe.
Hivi hawa watu hawaangaliagi movies za upelelezi? Waige japo machache. ..
 
Nissan Mazda ndio gari gani.!?
 
Ukijumlisha hutakaa upate jibu lenye akili. .
Habari za mjini ni kwamba, mke alikuwa ametengana na mumewe kwa muda mrefu.

Kungineee....hivi kweli huyu mama alikuwa na mapenzi Kwa mumewe kiasi hicho hadi kwenda kuripoti polisi Sikh hiyo hiyo!?!polisi watazame mawasiliano ya nyuma ya huyo mama kama kweli alikuwa anawasiliana na mumewe Mara Kwa mara,ratiba za mumewe pia ziangaliwe...Nina imani Kwa MTU Wa intelijinsia hana ratiba maalum na anaweza kutooneka Kwa muda bila taarifa hata Kwa mkewe!why siku hiyo I we ajabu!!
 
Ni mmasai wa mjini (mwarusha)
 

Wameamua kufoji na taarifa !
 

mi mwenyewe sijawaelewa polisi wetu katika suala hili

mnavuta gari tu, kirahisirahisi namna hiyo? bado tuko mbali sana
 
Sijui kwa nini nina mashaka na maelezo ya polisi...
1. Huyo kijana alijuwaje kama ndani ya nyumba kuna hizo 5M..?? Ni utaratibu wao kumweleza kiasi cha hela cha nyumbani..??
2. Muda unaotajwa kuwa ni wa tukio, mke alikuwa wapi..??
3. jamaa aweze kuosha gari halafu ashindwe kuosha panga mpaka linakutwa na damu..??
4. Jamaa kakamatiwa wapi..?? Alikimbia au walimkuta nyumbani..??
5. Kwenye hiyo familia kuna house girl..?? watoto..??
6. Hilo panga alikatwa mara moja tu na jamaa jamaa akafa..?? hakukuwa na purukushani..??
7. Ni mara ya kwanza kuwepo hela humo ndani hadi muuaji apatwe na tamaa siku hiyo tu tangu awepo hapo jyumbani...??
8. Kama amekiri, kwa nini wanawashikilia hao wengine.?? kawataja au..??
 

mashaka ni mengi kuliko kawaida
 

Kijana amekiri ameua kwa ajili ya mil 5, sasa wengine wanang'ang'aniwa kwa ajili gani ?
 
Lakini akaendelea kushika funguo za gari

Wakwanza kutolewa taarifa kuwa anashikiliwa na Polisi ni mke wa marehemu ! ........ walihisi nini wakati yeye alikuwa anamtafuta mumewe !?
 
Kuku ukinchinja damu inaruka mnooo...sembuse binadamu!!?? Halafu tena alikuwa anakunywa uji...possibly alikuwa kwenye kochi!!(kama kweli)..huo usafi Wa kusafisha hiyo damu na kuondoa harufu ya damu hata ukiwaita cleaners Wa manispaa Kwa siku moja hawawezi
 

Hilo ni DRAFT huyo jamaa ni kete ya sadaka ambayo haina faida, kajitaja vipi kirahisi hivyo, wajanja wamegundua kuwa huyo mtuhumiwa ni mbuzi wa sadaka
 
Kwahiyo mtuhumiwa alikuwa na shida ya 5m tu, zile pesa alizokutwa nazo marehem kwenye gari pamoja na simu, laptop hakuwa na shida nazo?
 
Kwahiyo mtuhumiwa alikuwa na shida ya 5m tu, zile pesa alizokutwa nazo marehem kwenye gari pamoja na simu, laptop hakuwa na shida nazo?

Hawa jamaa wametuvuruga badala ya kutusaidia !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…