Muugizaji nguli Will Smith akiwa Serengeti

Muugizaji nguli Will Smith akiwa Serengeti

Ila hawa jirani zetu huwa hawana aibu ngoma si yao wanaivalia kibwaya.
 
Mkuu nakwambia tena, labda wangetumia ujanja wa kumpa mchango diamond au king kiba , ajifanye kaenda kutalii yuko mbugani ,kisha abruptly wakutane na kupeana gwala, kisha domo arushe kwa page zake za kijamii mfano fb, inst, YouTube, n.k kisha waandishi wa kwenye blogs wazichukue na kuzisambaza kwa mitandao zako, hapo ungeona habari ya ujio wake ime hit the point of target. Ni mtizamo tu lakini mkuu.
kwakweli..... diamond angefaa kutengeneza hio scenario
 
Atakayekutana na Will aniombee number ya Ash, au chicktionary yake alipokuwa Bel Air, I'm sure Carlton hakuitendea haki.
 
ukimuweka Will Smith kwenye tangazo lenu utamlipa sh.ngapi labda kwa mfano??

please toeni ushauri wizara wawe wabunifu sio kudandia kiki ya mteja aliyekuja kutumia pesa yake.
mbona kwenye fb page tanapa wamemuweka
 
Naweza nikaamini yupo Tz

Maana kila nchi ina mg'ang'ania si kenya ,Uganda
Yupo Tanzania huyo jamaa aliyepiga nae picha ni pilot wa serenget balloon. Hapo ni serenget sehemu ballon zinapo land then wanapata breakfast. Sio Kenya
 
Wizara Yetu imenisikitisha sana. Will Smith ni muigizaji nguli kutoka marekani. Hakika ni muigizaji ambae ana watu wengi wanaemfatilia. Nilidhani kufika kwake hapa nchini pangepewa kipaumbele. Kuna watu huko ulaya na Amerka hawakujui Tanzania kabisa.
Kufika kwake hapa ni fursa ya kutangaza mlima Kilimanjaro na mbuga Yetu ya Serengeti kwamba vipo Tanzania na sio Kenya. Ni fursa nzuri ya kutangaza mbuga zetu nyingine pia na Tanzanite Yetu.
Haya mambo hayaendi hivyo... kabla ya kusikitishwa na wizara ulitakiwa kwanza kufahamu Willy amekuja kuja vp Tanzania!!!

Hawezi kuja kivya vyake au kwa niaba ya kampuni fulani halafu wizara idandie treni!! Kuna wengine wanakuja na ku-demand privacy... no camera; no media, no nothing!!

Hicho unachokitaka wewe kinapaswa kufanywa na wizara from the grassroot! Kwamba, ni wizara wenyewe wanamleta mtu wa kariba ya Willy na kuwekeana hizo conditions!!!
 
Nadhan huu ilikua wakati muafaka kwa wizara ya maliasili na utalii kutumia ziara ya nguli huyu kutangaza malisili zetu yani mbuga na mlima Kilimanjaro hata Tanzanite zetu.
View attachment 478147
Hawa jamaa vipi huyo porini kavaa Tai? na huyo Punda Milia si sawa Watu wa haki za Wanyama wako wapi? imagine Punda Milia wamuone Willy Kafanana nao kuanzia kiunoni na juu binadamu Punda watakuwa wanaowaogopa Binadamu Mr. Smith omba radhi haraka
 
Kisuruali chake hicho isitoshe kauziwa milioni nane, mgeni njoo faru john apone
 
Wizara Yetu imenisikitisha sana. Will Smith ni muigizaji nguli kutoka marekani. Hakika ni muigizaji ambae ana watu wengi wanaemfatilia. Nilidhani kufika kwake hapa nchini pangepewa kipaumbele. Kuna watu huko ulaya na Amerka hawakujui Tanzania kabisa.
Kufika kwake hapa ni fursa ya kutangaza mlima Kilimanjaro na mbuga Yetu ya Serengeti kwamba vipo Tanzania na sio Kenya. Ni fursa nzuri ya kutangaza mbuga zetu nyingine pia na Tanzanite Yetu.

Usije shangaa kukuta asilimia kubwa ya walioko kwenye board ya utalii hata hawamjui Will Smith. Movie stars wanaowajua ni akina Ray, JB, marehemu Kanumba na wale wa Nollywood, na pengine wafilipino na wakorea kidogo.
 
Kisuruali chake hicho isitoshe kauziwa milioni nane, mgeni njoo faru john apone
Bingwa hiyo troused ya will Smith ni Dolce and Gabbana zebra trousers price tag yake ni us dollars 995 , google kwa uwakika zaidi pesa ndefu kibongo bongo
 
Mependa body lake tu kifua kidogo kiuno nacho si haba
 
Elimu kitu muhimu sana, yaani Will Smith kaenda Serengeti watu wameanza kuilaumu serikali. Maajabu haya!
 
Usije shangaa kukuta asilimia kubwa ya walioko kwenye board ya utalii hata hawamjui Will Smith. Movie stars wanaowajua ni akina Ray, JB, marehemu Kanumba na wale wa Nollywood, na pengine wafilipino na wakorea kidogo.
Ha ha ha ha ha ha[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Inamaana mtu kuja kula good time yake. Mnataka afanye na matangazo pesa ya kumlipa mnayo au mnamkopa? [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom