Muuguzi aliyempiga Mjamzito vibao akutwa na hatia na kuondolewa kwenye baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania

Bro hujui kusoma au 😳😳😳
Halijamfuta Kazi Limemnyang'anya vyeti vya certification ya professional yake.

#YNWA
Acha kukurupuka wewe. Umeukuta uzi upo baada ya muda. Mwanzoni heading ilikuwa inasema baraza la uuguzi limemfuta kazi.
 
Kweli mnathubutu kumtetea nesi aliyemwacha mama mjamzito mwenyewe (angeweza kupoteza maisha yake na ya mtoto!); na kana kwamba hiyo haitoshi, anathubutu kumchapa vibao??? Huyo angefukuzwwa na kifungo juu! Sijui mnatetea nini hapa! Kama mapapa wanafanya makosa, nao wachukuliwe hatua stahiki! Kazi ya unesi/udaktari inahitaji moyo wa huruma kwa mgonjwa, hata kama hali ya kazi ni ngumu!
 
Aisee pole Sana Dada Muuguzi;

Wakati mwingine shetani huwa anazunguka zunguka kumtafuta wa kwenda naye huwa ni busara Sana kuepuka ugomvi na mtu yeyote.

Wengine tumejifunza hapa, life goes on.
 


Picha yake tafadhali ili tukikutana naye tumpishe mbali kama Masudi
 
Kumbe baraza la wauguzi lina mamlaka ya kufuta kazi mwajiriwa?
Kunyang'anywa leseni ya kazi ni sawasawa na kufukuzwa kazi. Moja kwa moja hapo muajiri hawezi kuendelea na mkataba na mtu ambae amethibitika kwenda kinyume cha maadili ya kiapo chake
 
The best way was kuhamisha badala ya kumfutia usajili na hatimaye kukosa sifa ya kufanya huduma nchini
Ili aendelee na ukatili? Watanzania mbona hatujipendi,!!! hatujihurumii?!!! Huyu Anaonekana anachojali ni mshahara na sio huduma takatifu anayotakiwa kuitoa kwa umma. Kwa tabia hiyo unadhani vifo vya kizembe na madhara yatokanayo na utendaji mbaya wa watu wa kaliba yake vitakwisha? Tujihurumie,kuna field hazihitilaji ujanja ujanja. Akafanye shughuli nyingine hata kilimo.
 
Vp
Hivi aliyechapwa vibao angelikuwa mkeo au mama yako Au mwanao ungeliandika ujinga huu?
km aliyefukuzwa angekuwa mama yako au mkeo?
Ni kweli alifanya kitendo kibaya na hakikubaliki lakini adhabu aliyopewa ni kali mno.
Wangeweza hata kumkata mshara kwa miezi kadhaa wampe fidia aliyepigwa
 
Hasira hasara akauze vitumbua apeleke hasira huko Ili abakie na vitumbua vyake
 
kama hana akiba ya kueleweka na vitega uchumi atateseka sana na atajuta siku zote..... Hata kama una hasira ni vizuri kukishusha muda mwingine na kuacha baadhi ya votu vipite tu....tusiache hasira zituongoze
Hasira ukaa moyoni mwa mtu mjinga na mpumbavu
 
Kumbe baraza la wauguzi lina mamlaka ya kufuta kazi mwajiriwa?
Baraza halikufuti kazi isipokuwa unafutiwa usajili. Ukishafutiwa usajili basi mojo kwa moja unakosa sifa ya kuajiriwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…