Atomu zijazo hai
Mpaka wakati huu, tumezungumza kuhusu atomu na jinsi maada (matter) inavyoumbwa pasipo na chochote. Tulisema kuwa atomu ni matofali yanayojengea kila kitu ama chenye uhai au kisichokuwa na uhai. Ni muhimu kufahamu kuwa atomus hujenga vitu vyote vilivyo na visivyo uhai. Kwa sababu atomu ni chembechembe isiyo hazina uhai, inashangaza jinsi zinavyoweza kuwa matofali ya kujengea miili yenye uhai. Hili ndilo jambo ambalo ni vigumu kuelezeka.
Kama ilivyo vigumu kufikiria jinsi vipande vya mawe kuwepo pamoja na kusababisha uhai wa viumbe, vile vile ni vigumu kuelewa jinsi ambavyo atomu zisizo na uhai zinavyoweza kusababisha uhai. Fikiria lundo la jabali na kipepeo ambapo moja haina uhai na nyingine ina uhai. Bado, tunapofikiri vyanzo vyake, tunaona zote zinatokana na chembechembe hizi ndogo za atomus.
Mfano ufuatao unaweza kuwa na maelezo zaidi kuhusu kutokuwezekana kwa maada isiyo hai kujigeuza baadaye kuwa na uhai.
Je, Aluminium itaweza kuruka? Jibu ni hapana. Tukichanganya aluminium na plastiki na petroli je itaweza kuruka? Jibu ni hapana. Pale tu tunapoviweka vitu hivi pamoja na kujenga ndege ya Aeroplane ndipo inapoweza kuruka.
Kwa hiyo ndege yenye mbawa, injini na rubani wa kuiendesha huweza kuruka. Haziwezi kuruka pekee bila ya mwendeshaji. Kwa hakika zote, ndege huwa ni michoro na uhakiki madhubuti ikifuatiwa na ujenzi wa uhakika wa ndege ndio baadaye huweza kuruka.
Vitu vyenye uhai navyo si tafauti sana. Cell yenye uhai hufanyika kwa mpangilio maalum wa atomu katika matengenezo madhubuti sana. Uwezo wa chembe chembe hizi za uhai (Cell) kama kukua, kuzaliana na vinginevyo ni matokeo ya mpango mahsusi zaidi kuliko tu kuwa ni tabia ya molekuli. Mpango huu tunaouona hapa ni wa Allah (s.w.) kaumba maisha kutoka kwenye vitu visivyo na maisha:
Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji (mwoteshaji) wa mbegu na kokwa (zikawa miti). Hutoa nzima katika maiti, naye (pia) ndiye mtoaji maiti katika mzima. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi mnageuzwa wapi?
Surat Al-Anam: 95
Ni Mwenyezi Mungu (s.w.) Mwenye nguvu na mwenye busara anayeweza kuvipa maisha vitu visivyo na uhai, hivyo kuumba viumbe hai. Mtandao wa maisha huwa katika muundo wa ajabu sana ambao huwa taabu kuelezea hasa pamoja na kuwepo kwa teknolojia ya hali ya juu kabisa ulimwenguni leo hii. Hata hivyo, kuna ukweli wa namna fulani unaotuwezesha sisi kufahamu maendeleo haya kwa msaada wa sayansi na teknolojia ya kisasa katika karne hii ya 21.
Maisha ya viumbe ni kitu ambacho kuwepo kwake ni kwa namna ya ajabu sana isiyo ya kawaida. Wakati maelezo ya Evolution yalipotolewa katika karne ya 19, utafiti uliofanywa kisayansi kupitia vikuza vitu (Microscope) vya hali ya chini sana vilionyesha kuwa Cell ni kama tu mkusanyiko wa maada (matter) .
Katika karne ya 20, uchunguzi na utafiti uliofanyika kwa kutumia vifaa bora zaidi kama Electron Microscope ulionyesha Cell ambazo ni kama matofali ya kujengea maisha, ambayo ilikuwa na umbile la ajabu kabisa ambalo lingeweza kuwepo kwa mpango ambao si wa kawaida kwa mwanadamu.
Muhimu zaidi ni kuwa, utafiti ulionesha kuwa Cell hizo haziwezi kuwa zimetokeza tu kwa kubahatisha kutokana na visivyo hai. Chanzo cha maisha na maisha pekee. Ukweli huu umedhihiri kwa majaribio [38].
Hili ndilo tatizo ambalo nadharia ya Evolution imeshindwa kupata ufumbuzi. Tatizo hili limewafanya wanasayansi wa Evolution kushindwa kutoa ukweli wa kisayansi na badala yake kueleza hadithi ambazo hazisemi chochote zaidi ya michapo ya mtu anayetazama dirishani na kujaribu kuelezea anayoyaona. Zinaweka mbele yote yasiyo na busara na hazina ushahidi wa kisayansi kuwa maada zina akili, uwezo, na matakwa ya namna yake. Hata hivyo vile vile hadithi hizo nazo hawaziamini na mwisho wake wanakiri kuwa maswali makubwa hayawezi kujibika kisayansi:
Kuna wakati mmoja kabla ya maisha yetu, wakati dunia ilikuwa jangwa kiasi cha kuhuzunisha. Dunia yetu leo hii imeshamiri maisha. Je, hii ilitokeaje? Vipi bila maisha, molekuli za Organik ziliweza kutokea? Je, ilikuwaje kutokea kwa maisha ya mwanzo? Ilikuwaje kwa vitu hai kujitengeneza katika namna hii ya ajabu na kwa chanzo kipi? [39].
Kufahamu maajabu ya kuumbwa ni majibu ya chanzo cha maada, jinsi ilivyotokea katika dunia na ulimwengu wetu huu na kwa nini itokane na molekuli hai kwa namna ya ajabu. [40]
Kwa jinsi wanamapinduzi wa kisayansi wanavyokiri, malengo ya msingi ya nadharia ya Evolution ni Mwenyezi Mungu (s.w.) aliyemuumba wa vyote vilivyo hai na visivyohai. Ijapokuwa, ukweli wa uumbaji umewekwa wazi katika mtizamo wote wa ulimwengu na yote yaliyomo unaonesha dhahiri kuwa kila unapotafuta undani unakuta unatokana na mpango madhubuti sana. Umadhubuti ambao akili ya binadamu haiwezi kufanya maumbile haya na vile vile haiwezi kuwa umetokea tu kwa kubahatisha. Nadharia hii inajitahidi kutumia akili ya kibinadamu kujichanganya changanya. Mwenyezi Mungu (sw) anatueleza kwenye Qurn:
Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu, akakuhuisheni, kisha atakufisheni, kisha atakuhuisheni, kisha kwake mtarejeshwa (atakapokufufueni).
Al-Baqara:28
Badala ya kuamini ukweli, wanasayansi wa Evolution hupendelea kuongea kuhusu uwezo wa maada na jinsi vitu visivyo na uhai vinavyoweza kujibadilisha kuwa vile vyenye uhai. Wakati wanafumba macho kwenye ukweli, wanasayansi hawa wanajiweka mahali ambapo huweza wakapata aibu. Ni wazi kuwa shutuma za kuwa atomu zina namna fulani ya uwezo na hutumia uwezo huo kujibadilisha kuwa kwenye vitu hai haina uhusiano na namna yetu ya kutafakari mambo.
Baada ya kusoma mfano tutaounukuu, nawe utaamua upendavyo kuhusu hekaya hizi zisizo na ukweli za Evolution. Hapa ndipo mahala wana Evolution hudai kuwa mabadiliko ya visivyo na uhai kuwa vyenye uhai, na muhimu zaidi kuwa watu wenye uwezo wa juu wa akili na ufahamu.
Baada ya mlipuko mkubwa unaoitwa Big Bang atomu zilizo na nguvu kubwa zenye uwiano madhubuti, kwa namna fulani zimejileta kwa kuwepo kwake. Wakati baadhi ya atomu zenye kujitosheleza kwa idadi kufanya ulimwengu mzima, zimeifanya nyota na sayari mbalimbali, na vile vile dunia yetu hii.
Baadhi ya atomu zilizofanya dunia, mwanzo zilifanya ardhi na baadaye, haraka kufanya viumbe hai! Atomu hizi zilijibadilisha kuwa Cells kwa umbile la hali ya ajabu kabisa na kutoa Cells nyingi zilizogawanyika mara mbili na baadaye kuanza kuzungumza na kusikia.
Hivyo hivyo, atomus hizi zikajigeuza kuwa Maprofesa katika vyuo vikuu, vikijitizama kwenye vikuza umbile (electron microscope) na kujinadi kuwa zimejitokeza kwa bahati mbaya. Baadhi ya atomu zikajifanya wahandisi wa ujenzi na kuanza kujenga madaraja na maghorofa makubwa. Wengine wakajenga vyombo vya angani na atomu zingine kujigeuza kuwa wataalamu wa fizikia, kemia na bailojia.
Atomu kama zile za Carbon, Magnesium, Phosphorns, Potassium na Iron zikaungana badala ya kuunda bonge kubwa la kitu cheusi ikaunda ubongo madhubuti na wa ajabu, ambao siri yake mpaka sasa haijajulikana kwa ukamilifu.
Ubongo ukawa unaona vitu kwa daimensheni-3 katika namna ya usahihi kabisa ambayo teknolojia tuliyonayo sasa hivi haijaifikia. Baadhi ya atomu zikafanya vichekesho na zikatuchekesha. Na baadhi yake kutengeneza muziki ambao watu hufurahia kusikiliza.
Inawezekana kurefusha aina hii ya simulizi, lakini ni vizuri tuishie hapa na tutengeneze majaribio (experiment) kuonesha kuwa simulizi hizi sio za kweli na haikubaliki. Tuwaachie wana Evolution wachukue atomu nyingi wazipendazo kwenye pipa, kwa elementi zote wapendazo zinazosababisha maisha. Tuwaachie wachanganye na waongeze chochote kilicho hapa ulimwenguni katika atomu hizi na halafu wasubiri. Wasubiri kwa miaka 100, 100 na ikiwa lazima miaka 100 milioni kuona kama kuna mtoto yeyote atakayezaliwa. Au tuseme kama kuna Profesa atakayetokea hapo.
Ni wazi kuwa haitatokea, kwa muda wowote watakaosubiri. Si hivyo tu bali hakutatokea, maisha kama ndege, samaki, vipepeo, nyani, tembo, mauwaridi, michungwa, nyuki, mbu wala kitu chochote chenye maisha.