Muumini Mwijuma sasa anaimba taarabu

Muumini Mwijuma sasa anaimba taarabu

SOCIOLOGISTTZ

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
2,615
Reaction score
927
Baada ya kutamba sana kwenye miziki ya bendi za dansi hapa nchini, Muumini mwijuma amehamia kwenye taarabu. Ikumbukwe kuwa Mwijuma muumini alianza kujulikana sana akiwa na Nchinga sound mpaka akajipachika jina la kocha wa dunia, baada ya hapo akachuliwa na bendi ya African Revolution iliyokuwa inatumia mtindo wa chumvi chumvi na akaubadilisha ukaitwa Tamtam. Tamtam ambayo ni kati ya bendi za kampuni ya ASET inayoongozwa na Asha Baraka ikavuma sana. Baadaye akaanzisha bendi yake mwenyewe aliyoiita Double M Sound. Akiwa Double M sound alisafiri na bend hadi tanga na alifanikiwa kuoa mwana dada anayeitwa Sadah Salehe. na alimtungia nyimbo wimbo....kuwa mtoto wa chumbageni ameumbika, (ikumbukwe kuwa alimuacha mke aliyepewa na baba yake kabla ya kumuoa Sada)

Vituko ndani ya ndoa vikaanza na Muumin Mwijuma akaanza kumuimba mke wake kuwa ni Call Box yaani kila anyetaka kupiga simu anapiga. wimbo huu uliwahuzunisha sana wanawake wakawa wamesusa kwenda kwenye maonyesho ya bend yake. Bend mwishowe ikafa.

Muumini kwa vile alivyokuwa anapenda kuimba mipasho kwenye bendi nadhani sasa ameenda mahali patakapomfaa, kwani anapenda sana mipasho na vijembe.
 
hii sio mahali pake .....Punguza uchizi na Viroba .....kunywa kwa wastani
 
shwain yupo kwenye kundi gani la taarabu be specific.
 
Huwa tunamcheka Mr.Nice kwa kupoteza umaarufu wake gafla ila huyu nadhani kupotea kwake kamzidi hata Mr.Nice
 
Juzi nilisikia,kaifufua tena ile bendi yake ya double m sound...
 
shwain yupo kwenye kundi gani la taarabu be specific.
Haitwi shwain anaitwa mwijuma Muumin au kocha wa dunia, nimemsikia akiimba taarabu kwenye radio, sikujua yupo bendi gani ila alikuwa anasema sasa kocha wa dunia kahamia huku.....Mtamsikia tu wenyewe
 
Huyu jamaa enzi zake wakati alikuja kuimba pale ilipokua Hotel ya 77 hapa Arusha nilikosa tiketi yakumuona, kama ni kweli Kocha wa Dunia kakimbilia taarabu basi mwisho wake atakimbilia kuimba Kwaya japokua sio Mkristo mwenzangu.
 
Back
Top Bottom