Kamugy T
JF-Expert Member
- Sep 17, 2018
- 1,110
- 1,226
Ligi bora zote ulaya hazina huu mfumo ni zile farmers leagues tuuKwa kuutazama huu muondo wa sasa hauleti ushindani na una mianya mingi sana ya hizi timu kongwe kuendelea kutawala.
Ingependeza baada ya mzunguko kuisha, ichezwe ligi ndogo walau ya timu sita tu ili kumpata bingwa wa ligi kuu ya Tanzania.
Zile timu sita za juu ndizo ziingie kwenye ligi ndogo ambayo itapigwa kwa mechi moja. (Sio home & away).
Hapa TFF wanaweza chagua viwanja bora kabisa ndipo baadhi ya mechi zipiwe huko.
Mfano wa viwanja ni Kaitaba, Lupaso,uhuru na chamazi.
Hii itaongeza ushindani zaidi lakini pia kushuhudia mechi zenye mvuto kwa mashabiki na kupata timu bora.
Hii itasaidia pia hata kwa marefa kutokuwa na presha, wala misheni town za timu kuunda matokeo.
Watasubiria kiumane kwenye hatua ya fainali ya hizo timu sita.
Pia hata kwa azam media itakuwa na tija zaidi,achilia mbali mapato ya viingilio.
TFF naomba ibadiri mfumo huu wa sasa wa ligi.
Alamsiki Bin Nuruuuu.
Sent from my SM-A500H using JamiiForums mobile app