Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitaifa kwenye nchi moja.
Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu ...... Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.
Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!
Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!
Mwanakijiji,
..mimi nataka serikali moja, serikali ya Tanganyika.
Sisi sio wa bara; ni WATANGANYIKA!
Yeah, hata Lukuvi alitamka hivyo bungeni. I prefer a single country, single govt
Hatutaki serikali Tanganyika ni mzigo kwa Tanganyika.
Serikali moja, na ni sisi watanganyika ndiyo tunavyotaka.
Mzee Mwanakijiji
Unatushauri watanzania(wabara aka watanganyika) sote tujiunge na CCM?
Sera ya CCM kutoka serikali mbili kuelekea moja imebadilika lini?
Lini CCM walibadilisha hii kutoka mbili kuelekea moja? Umesema CCM wanataka serikali tatu?
Hata hivyo wazo lako ni zuri tu, sasa uwashawishi CHADEMA na wanaCHADEMA waunge mkono wazo lako.
CHADEMA wana sera ya serikali tatu.Halafu pia uwashawishi CUF na wanachama wake wabadili sera yao ya muungano, serikali tatu.
Lissu ametonesha kidonda bungeni kwa kusema Tanganyika na serikali ya Tanganyika irudi.
Na mwazilishi wa Muungano, Mwalimu alisema ikifufuliwa EAC basi ni vyema Tanzania iwe na serikali mbili, ya Tanganyika na ya Zanzibar. Bofya hapa
lissu
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar(Tanzania) kwa miaka 48 umekosa kuvutia nchi nyengine kujiunga nasi,zimekuwepo kelele na mayowe ya wazanzibari kutaka waachiwe wapumue kwa miongo kadhaa sasa. Kweli mkuu unategemea kupata serikali moja, nchi moja na Taifa moja?
Kwa maneno mengine, unasema kuwa tuimeze Zanzibar? Au ndio kampeni ya "Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye muungano"?
Unasema,
Hatutaki serikali Tanganyika ni mzigo kwa Tanganyika.
Tukishawasaidia Zanzibar kutoka katika Muungano, tutabaki na serikali ipi?
Serikali ya Tanganyika huitaki, je unaitaka Tanganyika? Unataka Tanganyika isiyo na serikali?
Ni imani yangu kuwa wengi tutamuunga mkono Lissu katika kupeleka hoja ya kufufuliwa kwa Tanganyika na serikali yake, ili tukutane na Zanzibar huko EAC na kwenye shirikisho la EAC(muungano wa nchi nyingi).Huu wetu ambao umeshindwa kutatua kero za muungano na kuvutia wanachama wepya uachwe ufe bila kuleta vifo vya ziada na vilema wa ziada, na mihanga mengine katika kuulinda/ kulazimisha uwepo.