Mkuu wangu hawa watu wanadanganywa sana na wanasiasa wao. Kila jambo liloongezwa ktk mktaba wetu wa muungano ni kwa matakwa ya serikali ya Mapinduzi kwa ajili yao na kwa nafasi ya Zanzibar ktk muungano huu lakini bado wanahitaji, wanahitaji hawachoki kutaka kilichobakia ni moja tujitenga nao. Hilo koti wanalosema linawatia joto mbona ndilo wanalitumia kila wanapoenda kuomba kazi wasivae misuri na kanzu?.
Hiyo serikali moja mnayoitaka, ndio itakuwa kutumia nguvu sasa, maana sii kitu wanachokiombea kabisa isipokuwa wale waliokuwa ktk jumuiya ya Pan African ambao kwa Zanzibar ya leo hawapo na kama wapo wameisha poteza tumaini. Hivyo serikali moja italeta mgogoro kubwa kuliko huu na mwisho wake tutauvunja Muungano, hivyo kwa nini kazi yote hii wakati tunaelewa mwisho wake? Hivi tunatafuta serikali zipi zinafaaa sii kutokana na malalamiko ya Wazanzibar?
LET ZNZ Goo ndio suluhisho tena nadhani tuwalazimishe wafanye referendum japokuwa utawasikia wakiitaka serikali ya muungano ndio igharamie. Tunajua fika waloingia ndoa hii hawataki talaka isipokuwa watoto wao na kwa kadhi haendi mtoto kuomba talaka bali mzazi.
Ha ha ha ha! ''Kadhi kaingia mjini watu hawataki kuomba talaka''
Mkuu Mkandara, miaka michache iliyopita waliamua kuwa na ZMA(Zanzibar maritime Agency) kwasababu SUMATRA inawabana wasifanye biashara. Imekuja julikana kuwa kumbe ZMA hailipi ada kule Internationa Maritime Organization.
ZMA ni chaka la viongozi kusajili meli kwa bendera za 'koti' na kulipiwa ada na fedha za 'koti' ili wafanye biashara na Iran
Mkuu,wabia wa ZMZ mmoja ni yule yule anayehubiri kuvunjika kwa muungano kwa njia ya uani. Sasa hivi hasemi kwasababu amesogezwa karibu na sania la ubwaba na kupewa wadhifa wa pili wa kugawa nyama.
Hawa mayahe wenzangu wanashabikia tu hawajui adha itakayowakuta, hawajiulizi kwanini kila kiongozi wa ZNZ ana makazi Tanganyika na anaishi Tanganyika
Tena tukiwauliza katika mambo 11 wanayodai Tanganyika inafaidika na nini hawana jibu.
Kimya chetu kiliwafanya waone kuwa wana hoja za maana sana. Siku hizi kimya, hoja zao zimevunjwa vunjwa na MZNZ mwenye akili na ufahamu amekaa kimya, lakini akina Yakhe wamebaki kudanganya kule mzalendo.
Mkuu Kibona, zaidi ya uliyosema Tanganyika ni soko kubwa sana la Zanzibar. Hilo halina ubishi hata wao wanajua.
Kuvunjika kwa muungano tena katika hali ya chuki walioijenga kutawaumiza sana.
Angalia mahusiano yetu na Zambia, Kongo, Burundi, Msumbiji, hakika huwezi kuona kama kuna tofauti ya nchi hizo. Wazambia wapo tu wengi Tanganyika kama walivyo Watanganyika Lusaka. Kwa vile tupo katika misingi ya kuheshimiana na kuthaminiana huwezi sikia kelele dhidi yao.
Kwa Zbar siku muungano ukivunja sijui nini kitatokea maana Watanganyika wana hasira sana si kwasababu wanawachukia WZNZ bali wamechukizwa na WZNZ.
Nafahamu ugumu utakaowasibu katika biashara na ajira, elimu na afya na hiyo itakuja kwasababu tu si huyu ni MZNZ! anayejiona bora sana sasa ni wakati wa kumtenda. It is coming just a matter of time. Huko maofisini siku hizi wanaonja joto ya jiwe, wanapewa 'live' ondoka rudi kwenye nchi ya neema yenye mito na maziwa ya asali
Hizo gharama za ulinzi ulizosema hazitaongezeka kwasababu hata sasa hivi gharama za jeshi ni za Mtanganyika asilimia 100. Kitakachotokea ni kuzihamishia gharama hizo zibaki Tanganyika kama ilivyo.
Lakini pia lazima tuelewe kuwa kuna mabilioni yanakwenda ZNZ bila hesabu. Juzi ofisi ya makamu wa Rais imepewa bilioni 32 kwa ajili ya ZNZ, yaani makamu akitaka kunywa chai na UAMSHO ofisini hizo ndizo gharama za usafiri nk.
Sasa hivi wapo kimya! tunasema hamkani si shwari LET ZNZ GO!
Sisi Tanganyika tuna uzoefu wa kusimama wenyewe.
Kenya walipotupiga bao mwaka 1977 tulisamama kidete na bado tunasonga mbele.
Hakuna serikali 3, mahusiano au mkataba
Ima serikali 1 ambayo hamtakubali na hapo tunasema LET ZANZIBAR GO! Nothing to lose!