Muungano: Dkt. Mpango na Waziri wa Afya, hili si la Muungano. Msiliingize kinyemela!

WAHAMIAJI HARAMU KUTOKA TANZANIA BARA KWENDA ZANZIBAR (II)
KATIBU MKUU ABEIDA ''ATHIBITISHA'' KAULI ZA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS MASOUD OTHMAN


Hapo juu tumeeleza kisa cha Watoto 66 '' Wahamiaji haramu'' kutoka Bara kwenda Zanzibar
Ni habari liyozizima mitandaoni kwa mshtuko kwamba tuna tofauti za mipaka na Uhamiaji.

Uhamiaji ni idara katika Wizara ya mambo ya ndani. Mwaka 2024 Uhamiaji ilikamilisha ujenzi wa jengo Zanzibar.
Watumishi wa Uhamiaji wanafunzwa katika Chuo cha Uhamiaji Tanga na Moshi kwa gharama za JMT

Rais SSH aliagiza Watumishi wa Zanzibar wabadilishane na wa Bara kuimarisha utendaji

Gazeti la Mwananchi ( Rejea bandiko#38) lilimkariri makamu wa Rais Mh Othman Masoud Othman akisema Uhamiaj imeondolewa katika Muungano bila kueleza lini na kwa utaratibu gani, ilikuwa ni SIRI

Gharama za uendeshaji ni jukumu la JMT ambaybajeti ni kutoka Tanganyika.
Kilichoondolewa Uhamiaji ni uwezo wa kukusanya mapato kama JMT na sasa SMZ inakusanya .

Gharama za uendeshaji wa idara ya Uhamiaji zikiwemo mishahara, majengo n.k. zinalipwa kutoka bajeti ya JMT ambayo ni ya Tanganyika. Bajeti ya SMZ 2024/2025 haina kipengele cha Uhamiaji.

Kauli ya Katibu mkuu Bi Abeida Rashid kuhusu 'Watoto wahamiaji haramu' inashabihiana na ile ya makamu wa wa Rais Mh OMO kwamba Uhamiaji imeondolewa kinyemela kama ilivyo ondolewa gesi/mafuta . Bandari n.k. ingawa gharama za uendeshaji idara ya Uhamiaji Zanzibar ni za JMT au Tanganyika.

Haiwezekani kukawa na watoto wahamiaji haramu kama sisi ni Nchi moja.
Mtoto akitoka Mbeya kwenda Tanga hawezi kuwa mhamiaji haramu, iweje wa Tanganyika kwenda Zanzibar awe hivyo? Je watoto wa Wazanzibar wanaoishi Tanganyika nao ni 'Wahamiaji haramu'' ?

Hoja inayojengwa ni kwamba Watoto wa Wazanzibar wanaoishi Tanganyika ni ''Watanzania'' kwasababu kila Mzanzibar ni Mtanzania lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar.

Ni kwa mintaarafu hiyo Watoto wa Wazanzibar wanaoishi Tanganyika wanahaki na kila fursa kama Watanzania, lakini Watoto wa Tanzania Bara wanaokwenda Zanzibar wanapoteza Utanzania na kuwa Watanganyika na hapo hupachikwa jina la Wahamiaji haramu. Mbunge aliyetaka Watanganyika waende Zanzibar kwa passport alikuwa na hoja kama ya Bi Rashid na Makamu wa Rais OMO. Mbunge aliyeukana Utanzania alikuwa na hoja kama ya Bi Rashid.

Kauli ya Bi Abeida Rashid inapaswa kukemewa. Ni kauli inayoleta hisia na chuki

Bi Abeida Rashid amewadhalilisha Watanganyika!

Ikiwa Uhamiaji si jambo la Muungano kama wanavyodai Wazanzibar, mipaka iwekwe na hoja ya passport irudi mezani ili Watanganyika waende kwa passport na Wazanzibar nao waishi Tanganyika kama Wageni!
 
ZANZIBAR INAONEWA, IPEWE NAFASI YA KUKOPA
OMO ATAKA ''FULL AUTONOMY''
MANSOUR ATAKA ' FULL AUTHORITY'

Taarifa ni kwa hisani na shukrani kwa gazeti la The Citizen

Ziara ya viongozi wa ACT Kkisiwani Pemba inatuelezamengi. Ukifuatilia kauli za kiongozi Othman Masoud Othman (OMO) katika mikutano utabaini jipya kuhusu muungano.

OMO amemsifia Rais mstaafu Karume kwa kuongoza mageuzi ya katiba tunayojua yalikiuka taratibu na katiba ya JMT. Ni mageuzi yaliyoondoa Zanzibar katika Muungano kiaina ingawa katika ''mafao'' bado ipo.

Kwa wanaosema ACT wanataka Muungano uvunjike wanawaonea! CCM ni washirika pia

Tofauti ya ACT na CCM ni kutoaminiana kutokana na tofauti za kihistoria na kinasaba. Kwamba nje ya Muungano nini kitafuata!!!. CCM wana hofu ya historia wakiwa na mtazamo mmoja wa kutotaka Muungano.

Katika mkutano OMO anasema Wazanzibar wanataka '' Full autonomy''. Kwa tafsiri isiyo rasmi '' huru na inayojitegemea'' , Zanzibar isiyofungamana na Tanganyika Kiulinzi na Usalama, Uchumi, kijaamii na Utamaduni. OMO anachosema ni Zanzibar nje ya Muungano

Kiongozi, Mansour Himid aliyekuwa CCM anasema '' Zanzibar inataka Full authority'' akimaanisha Zanzibar yenye mamlaka kamili yaliyo na mipaka! kwamba kuna mambo itahitaji kushirikiana au kuhusisha Tanganyika.

Mansour Himid anaamini katika 'mapinduzi daima' na full authority. OMO haamini 'mapinduzi' anataka 'full autonomy'. Hizi ndizo tofauti tulizoleza mwanzoni za ACT na CCM zikijengwa katika kutoaminiana

Suala lingine aliloongea ni Mikopo. OMO anasema Zanzibar haiendelei kiuchumi kwasababu haina uwezo wa kukopa ikifungwa mikono na JMT au Tanganyika.

Kwa utaratibu, SMZ inakopa kwa kudhaminiwa na JMT na kuna mikopo ya Zanzibar inayolipwa na JMT

Hoja ya OMO ina mantiki. Hakuna sababu za kuzuia Zanzibar isikope.
Ikiwa watakopa na kulipa deni ni 'KERO' kuwaweka katika udhamini wa Tanganyika.

Kuna kila sababu za kuiacha Zanzibar au kuisaidia bila udhamini ikope matrilioni ya fedha kokote duniani ili mradi tu ukopaji huo hautamhusisha Mtanganyika.

OMO anapaswa kulieleza hilo wazi na pia atamke kwamba Zanzibar haihitaji udhamini wa Tanganyika na katika hili Tanganyika imuunge mkono OMO na ACT
 
KITUKO KINGINE CHA MUUNGANO WA ''TANZANIA NA ZANZIBAR''
MAKUBALIANO (MoU) KATI YA NCHI YA ''TANZANIA NA NCHI YA ZANZIBAR'' KUHUSU USAFIRI MAJINI


Mabandiko yaiyopita tulieza tukio la makubaliano '' memorandum of understanding' au 'MoU' kati ya Nchi ya ''Tanzania na Nchi ya Zanzibar'' katika Nishati. Makubaliano hayo yalisainiwa

Hakuna kumbumbu za kuonyesha liliwahi kufanyika huko na hata kama lilifanyika ilikuwa ni makubaliano tu ya uendeshaji. Tofauti na sasa , MoU ni tukio kubwa kama yale yanayohusisha mataifa.

Kwa hisaini ya Gazeti la Mwananchi

kuna maafikiano ya Wakala wa meli wa JMT (TASAC) na Mamlaka ya usafiri ya nchi ya Zanzibar (ZMA)
Maafikiano yataleta Makubaliano (MoU) katika wiki zijazo kati ya '' Nchi ya Tanzania na Nchi ya Zanzibar'' .

TASAC ni wakala wa usimamizi wa usalama, biashara, na usafirishaji wa majini ''Nchini Tanzania''.
TASAC ilianzishwa 2018 kwa sheria ya Bunge ya Wakala wa meli no. 415 na ilianza majukumu Feb 23 2018

Uanzishwaji TASAC ulijadiliwa Bungeni wakiwemo Wabunge kutoka Zanzibar. Sheria iliridhiwa na Rais wa JMT kama chombo cha JMT chenye mamlaka ya usalama, biashara, usafirishaji na uwakala wa Meli

Katika mazingira ya utata wa Muungano zama hizi, Zanzibar wameanzisha chombo chao ZMA.

kwa mantiki kwamba kuna mipaka ya bahari kati ya 'Tanzania na Zanzibar''.
Si tatizo Zanzibar kuwa na taasisi,si mara ya kwanza, na hakuna! mamlaka/taasisi isiyo na mbadala Zanzibar.

Ni haki kusema TASAC si chombo cha Muungano, ni cha Tanganyika lakini kwa jina la Tanzania.
Sheria zinazotekelezwa na TASAC zimetaja ''Tanzania Bara'', nchi isiyokuwepo na wala haijawahi kuwepo

Jina Tanzania linawanyima Watanganyika fursa ya chombo chao kama ilivyo kwa Wazanzibar.

TASAC ipo chini ya Wizara ya Uchukuzi isiyo ya Muungano. Na hapa ndipo tatizo linapoanza.

1. Kwa muundo wa TASAC , Rais wa JMT anaweza kumteua yoyote midhali ni Mtanzania kuwa Waziri wa Uchukuzi.
Hili linawahusu Wazanzibar kwasababu '' Kila Mzanzibar ni Mtanzania, lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar''
2. Mkurugenzi wa TASAC anaweza kutoka Zanzibar kwasababu zile zile, ni Mtanzania.
3. Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC anaweza kutoka Zanzibar kwasababu zile zile, ni Mtanzania
4. Wajumbe wote wa Bodi wanaweza kutoka Zanzibar kwasababu zile zile, ni Watanzania.
5. Watumishi wote wanaweza kutoka Zanzibar kwasababu zile zile ni Watanzania

Mantiki ni kwamba, TASAC ni ya Tanganyika kisheria,, lakini, inaweza kumilikiwa na kuendeshwa na Wazanzibar kwa 100%, kwasababu nao ni Watanzania. Hakuna Mtanganyika anayeweza kutumikia ZMA kwa nafasi yoyote! kwasababu si Mzanzibar!

Kwa namba 1-5 hapo juu hakuna sheria itakayovunjwa. Wazanzibar ni Watanzania, ingawa TASAC ni chombo cha Tanzania japo hakifanyika kazi Zanzibar.

Hapa ndipo hoja ya Tanganyika kukasimu madaraka yake katika muungano inapojitokeza'.

Wazanzibar wana haki katika TASAC walishiriki sheria ya kuanzishwa kwake Bungeni
Maswali ya kujiuliza, kwanini chombo cha Tanganyika kitungiwe sheria, Wazanzibar wakishiriki?

Kwanini chombo kilichotungiwa sheria na Wazanzibar hakitambuliwi Zanzibar lakini kinaitwa cha Muungano?

Na kwanini chombo kinachofanya kazi kwa kuzingatia mipaka ya Tanzania kina mipaka ndani ya Tanzania?
Ikiwa Zanzibar si Tanzania, Tanzania inayotajwa na sheria iliyoanzisha TASAC ipo wapi?

Kwanini tunaita vyombo au taasisi za Tanganyika kwa jina la Tanzania ikiwa hazitambuliwi na Wazanzibar?

Yote haya yanatokea kwasababu vyombo na taasisi za Tanganyika hazina usimamizi na mwenyewe.
Je, kuna sababu ya kujiuliza tena iwapo Tanganyika inahitajika?

Kuwa na taasisi Tanganyika tukizificha kwa jina la Tanzania hakusaidii.
Turejee katika Rasimu ya Warioba, mambo 7 tu! na kama haiwezekani tusijidanganye tuna muungano!
 
ZANZIBAR ILIPOJITOA LIGI KUU YA TANZANIA
Ligi kuu ya soka Tanganyika ni 'moto'


Kwa hisani ya gazeti la The Citizen

Chama cha zamani cha Mpira wa miguu Tanzania (FAT)kilikuwa na ligi ya mpira (Soka) ikizikutanisha timu za Tanganyika yote na Zanzibar (Pemba na Unguja).

Timu za Tanganyika ziliongozwa na miamba ya soka Simba na Yanga, nyingine zilizosikika ni Tumbaku Morogoro, CDA-Dodoma, Pamba-Mwanza, Costal Union na African Sports za Tanga, Bandari-Mtwara, Maji Maji-Songea, Pan Africa, Nyota Nyekundu, Mwadui-Shinyanga, Balimi-Bukoba kwa uchache.

Timu kutoka Zanzibar zilizosikika zilikuwa Navy (KMKM) Miembeni, Jamhuri, Small Simba, Mwembeladu.

Ushindani wa Ligi ulikuwa mkubwa kiasi cha Timu kama Miembeni, Small Simba na KMKM kuwakilisha Tanzania katika michezo ya Kimataifa. Timu hizo zilikuwa changamoto kwa timu za Dar es Salaam

Katika miaka ya karibuni iliundwa shirikisho la soka TFF likirithi mikoba ya FAT.
Choko choko za ''Muungano'' zilianza zikiongozwa na Waandishi wawili wa habari , mmoja wao akiwa Mbunge wa ACT kwa sasa wakidai kuiondoa Zanzibar katika Ligi Kuu ya Tanzania.

Hoja ya Wazanzibar ni kunyimwa misaada inayokuja kwa jina la FAT au TFF, wakidai hilo linalemeza soka la Zanzibar, wakijitoa Zanzibar itapata mafanikio.

Choko choko za kujitenga kutoka Muungano zilipamba moto, busara ikanena Wazanzibar waachwe wawe na ligi yao na ushiriki wao kimataifa katika mambo ya soka.

Tangu kuvunjika kwa ligi ya Tanzania, Watu wa Tanganyika hawaelewi nini kinachoendelea Visiwani.
Ni ngumu atakayekueleza soka la Zanzibar lipo wapi. Kuna wakati kiongozi wa CAF aliwahi kushangaa ligi ya Zanzibar, kwa uchache aliiponda

Kinyume cha hayo, timu za Tanganyika kama Simba , Yanga, Azam, na nyingine zimetengeneza ligi kubwa Afrika (soma link hapo juu), ikiwa ni ya 5 Afrika na 57 Duniani ikizipiku ligi za South Africa, Nigeria, Ghana n.k.

Timu za Tanganyika zimefanya vema katika mashindano ya Afrika na ni Vilabu vinavyotazamwa kwa jicho la tahadhari na manguli wa soka kutoka kona zote za Afrika. Ni kielelezo cha kukua kwa soka.

Timu za Tanganyika zimekuwa maarufu Zanzibar zilikojizolea mashabiki na Wapenzi zikitumia viwanja vya Zanzibar kwa mashindano na hata mazoezi na si kushindana katika Ligi Kuu kama ilivyokuwa zamani

Wachezaji wa Vilabu vikubwa wanatoka Zanzibar kutokana na fursa za kiuchumi na kukua kisoka. Mathalani, kuchezea Yanga, Simba au Azam kunamweka mchezaji kwenye ramani ya Afrika na Dunia.
Ni rahisi kufikiwa na ''scouts' kwasababu wanaonekana.

Vilabu vya Tanganyika vinachukua ''advantage' ya Muungano kwa kuwapata Wachezaji kama vile wanatoka Tanga au Mwanza.
Kwa Zanzibar Wachezaji wa Tanganyika ni maruku au kuwekewa kodi, tozo na kila aina ya hujuma.

Kwa mtazamo hapo juu, kuna maswali ya kujiuliza.
Je, ni kweli Tanganyika iliinyonya Zanzibar? Je, Zanzibar imefaidika na misaada baada ya kujitoa!

Nje ya Muungano wa soka Tanganyika imepoteza nini? Nje ya Muungano Zanzibar imefaidika na nini?
 
MKOPO WA SHUGHULI ZISIZO ZA MUUNGANO KWA ZANZIBAR
UJENZI UGHARAMIWE NA TANESCO, MAKUSANYO YAFANYWE NA ZECO

Kwa hisani ya gazeti la Mwananchi

Tumefafanua mara kadhaa kuhusu 'mvurugano' wa mambo ya Muungano hasa taasisi zake.
Kila Taasisi inayoitwa ya Muungano kuna upande wa pili kule Zanzibar.

Hili ndilo swali la kujiuliza, ikiwa kuna Taasisi za JMT na Zanzibar, hii JMT ni kitu gan!?
Kwa jicho lisilohitaji certificate ya aina yoyote, Taasisi za JMT ni Taasisi za Tanganyika.

Mfano wa Taasisi hizo ni TANESCO na ZECO ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa gazeti hapo juu, kikao cha Makatibu wakuu wa Wizara za Nishati za '' pande' mbili za Muungano walikutana Zanzibar kwa kikao cha ushirikiano.

Kituko kinaanzia hapo, kwamba, Wizara ya nishati si suala la Muungano, kwahiyo, kikao ni baina ya Katibu Wizara ya Nishati ya Tanganyika kwa jina la Tanzania au JMT na Wizara ya nishati ya Zanzibar

Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati Zanzibar '''Bwana J. Kilangi kwa mujibu wa gazeti'' alisema sekta ya Utalii inategemea umeme, kupungua kwa umeme ni kutokana na ongezezeko la mahitaji Zanzibar na njia za kebo za baharini kutokukidhi. Kilangi akasema umeme wa joto ardhi wa megawati 5000 Mtwara utaifaidisha Zanzibar pia

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Tanganyika au Tanzania Bara au JMT Bw. F. Mramba akasema kikao kitajadili kuweka kebo mpya ya umeme kutoka Tanga kwenda Pemba, Uchambuzi yakinifu umeshaanza.

Mazungumzo ya kupata fedha za mkopo kati ya TANESCO na Benki ya Maendeleo ya Afrika yanaendelea.

Katibu Mkuu F. Mramba anamaanisha TANESCO ya Tanganyika au Tanzania Bara au JMT ndiyo inakopa pesa za kuweka kebo ya Umeme kwenda Zanzibar ambako kuna shirika la Umeme la ZECO

Wakati TANESCO inayoendeshwa na kodi za Tanganyika inakopa pesa za kuweka kebo kwenza Zanzibar, ZECO inafanya kazi moja, kukusanya mapato ya umeme Zanzibar na kuweka bei elekezi

Soma hapa chini kwa hisani ya gazeti la Mwananchi

Kutokana na hayo hapo juu kuna hoja zinajitokeza
1. Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Tanzania ''ni wa Muungano'' kwasababu anateuliwa na kuagizwa na Rais wa JMT kupitia Wizara ya Nishati ya JMT ingawa Nishati si jambo la Muungano.
Kikao cha Zanzibar ni kati ya JMT na SMZ!.
Ndani ya JMTm, Zanzibar ipo na imewakilishwa , swali nani alisimamia masilahi ya Tanganyika?

2. TANSECO si shirika la Muungano, kazi zake zinaishia Mbweni ''kebo' za Baharini zinapoanzia kwenza Zbar

Wakati wa Rais Kikwete kifaa cha Umeme rasi kilomoni kiliharibika. Zanzibar hawakuwa na Umeme kwa miezi 3 hadi Waziri kiongozi Shamsha V alipomuomba Kikwete Bilioni 5 kulipa Norway ije ifanye ukarabati.

Kikwete alitambua TANESCO si suala la Muungano na Umeme ukivuka Bahari ni suala la SMZ na ZECO
Kwamba gharama za umeme Zanzibar chini ya SMZ na ZECO hazipaswi kulipwa na Tanganyika

Ni kwanini leo TANESCO ikope pesa Benki ya maendeleo Afrika kwa umeme usiotumika Tanganyika wala makusanyo ya umeme wa Zanzibar hayatavuka Bahari.

Kwanini mtumiaji umeme wa TANESCO abebe mzigo wa kulipia deni la kebo za Zanzibar wakati ZECO Zanzibar wanakusanya pesa bila kugharamia miundo mbinu ya umeme

3. Hoja ya kwamba mikopo ya Zanzibar inalipwa na kodi za Tanganyika jibu lake lipo hapa

Allen Kilewella
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…