Muungano uruhusu wawakilishi toka Tanganyika katika Bunge la Zanzibar

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
40,051
Reaction score
51,217
Ni Muda sasa wabunge toka baraza la wawakilishi huwa pia na fursa ya kuingia Bunge la Muungano.

Sio vibaya kama wabunge toka bara baadhi yao nao wakiwa wanahudhuria vikao vya baraza la wawakilishi.

Uwekwe utaratibu maalum ambao utawafanya wabunge hao kushiriki vikao bila kuathiri maamuzi ya ndani ya Zanzibar.
 
Wabunge wakafanye Nini Baraza la wawakilishi? Wawakilishi watano huchaguliwa kutoka Baraza la wawakilishi kuwakilisha ZNZ katika masuala ya muungano na maslahi ya ZNZ. Hao wabunge kutoka Tanganyika wanaenda kuwakilisha Nini ZNZ.
 
Wabunge 50 wanaingia bungeni kutoka Zanzibar. Hivi hawatoshi kuiwakilisha Zanzibar hadi waongezwe watano kutoka Baraza la wawakilishi?
 
Wanakwenda kuwa wawakilishi wa Tanganyika huko visiwani.
 
Hao 50 wanaenda kuwakilisha majimbo yao binafsi , 5 huteuliwa kwenda kuwakilisha ZNZ katika masuala ya muungano.
 
Wanakwenda kuwa wawakilishi wa Tanganyika huko visiwani.
Wabunge kutoka ZNZ wanawakilisha ZNZ Kwa sababu znz ni sehemu ya Tanzania , hao wabunge wa Tanganyika wanakwenda kuwakilisha Nini wakati wao sio wazanzibari? Baraza la wawakilishi hujadili mambo ya znz tu ambayo Tanganyika haihusiki. Nadhani ni muda sasa Tanganyika wajitafute.
 
Wabunge wakafanye Nini Baraza la wawakilishi? Wawakilishi watano huchaguliwa kutoka Baraza la wawakilishi kuwakilisha ZNZ katika masuala ya muungano na maslahi ya ZNZ. Hao wabunge kutoka Tanganyika wanaenda kuwakilisha Nini ZNZ.
Na nyinyi mnafata nini huku?
 
Huu Muungano wetu, ukiufikiria vizuri kuna vitu unatakiwa uviache tu kama vile unasoma biblia na kuamini kuwa kila kitu kipo sawa.....
Muda wa kunyamaza/kufunika kombe, umepita! Tulipendekeza muungano wa serikali 3 kwenye Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba! Wahafidhina ndani ya ccm wakaleta figisu zao!

Hata sasa tumeendelea kubakia na huu muungano wa kipuuzi, na ambao unainufaisha zaidi Zanzibar huku Tanganyika ikigeuzwa kuwa shamba la bibi na Wazanzibari. Hili jambo halikubaliki. Leo hii Lissu ambaye ni mtetezi wa Tanganyika, ananyanyaswa na Mzanzibari aliyeshinda uchaguzi wa Tanganyika kwa hila! Kwa hali hii ni kwa nini chuki zisiongezeke baina ya hizi nchi mbili?
 
Wabunge kutoka ZNZ wanawakilisha ZNZ Kwa sababu znz ni sehemu ya Tanzania , hao wabunge wa Tanganyika wanakwenda kuwakilisha Nini wakati wao sio wazanzibari? Baraza la wawakilishi hujadili mambo ya znz tu ambayo Tanganyika haihusiki. Nadhani ni muda sasa Tanganyika wajitafute.
Wanakuwa watazamaji tu bila kuathiri mambo ya Zanzibar.
 
Zenji ni ka Taiwan ketu. Kametukalia pabaya twende kwa step.
Hadi hapo nyakati zitakapofika tukawa na nchi halisi ya TANZANIA yenye rais 1, Bunge 1 na Mahakama 1. Chini yake ni mikoa na wilaya.
Hatuna namna ya kuutenganisha tena udongo wa Mwl na Karume. Sisi ni udongo mmoja!
 
Hao watumie rasilimali zetu mara ya mwisho mwisho.
Tunashida nao.

Haiwezekani ukawa unaishi nchi moja alafu mikoa mingine hauruhusiwi kumiliki ardhi.
 
Back
Top Bottom