real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,299
Watu kutoka ndani wameliambia gazeti la Nation kwamba hatua ya watatu hao kutoshiriki tukio hilo, na ambalo Musyoka alielezea Jumanne, ilikuwa kuweka hai matumaini ya kuingia Ikulu mwaka 2022.
Kuhusu ikiwa alikuwa na wasiwasi kila chama kujipanga kwa uchaguzi wa mwaka 2022 kwa gharama ya umoja, Wetang'ula alisema: "Hapa niliposimama, na nilipoketi, sitaki kuvutwa na masuala kama hayo."
Naibu kiongozi wa chama cha Ford-Kenya Boni Khalwale, ambaye ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya kuratibu shughuli za Nasa, alikuwa wazi zaidi, akichelea kidogo tu kusema umoja umekufa.
Shutuma za usaliti kwa kushindwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Raila Odinga na matamanio ya urais mwaka 2022 yanatishia kuvunja muungano wa upinzani wa National Super Alliance (Nasa) ikiwa ni mwaka mmoja tangu ulipoanzishwa.
Na hatua ya chama tawala cha Jubilee – kilichojiapiza kwamba Machi 2018 kiusambaratishe upinzani kwa kuwashawishi kujiunga au kutumia mbinu za gawa uwatawale – kumezidisha hali kuwa mbaya zaidi huku chama cha Odinga cha Orange Democratic Movement (ODM) kikilaumiwa kuwa ni mnufaika mkubwa katika nafasi za bungeni.
Viongozi wakuu Kalonzo Musyoka wa Wiper, Musalia Mudavadi wa ANC, na Moses Wetang'ula wa Ford-Kenya hawakuhudhuria tukio la Odinga kujiapisha kwenye viwanja wa Uhuru Park, kitendo kilichofunua mfululizo wa shutuma na mashambulizi yanayotishia kutoboa jahazi la upinzani.

"Sitaki kulizungumzia suala hilo, hata kidogo, hata kidogo. Niacheni, "Wetang'ula aliiambia Nation alipoulizwa kuhusu hali ya muungano, jibu ambalo si la kawaida kwa mtu ambaye wiki moja iliyopita alikuwa akitoa majibu ya kujiamini juu ya umoja wa muungano.

"Sisi (Ford-Kenya) tumefungua milango kwa mazungumzo mapya na vyama vya siasa ndani ya Nasa na, popote pale fursa ikipatikana hata nje ya umoja huo," alisema Khalwale, seneta wa zamani wa Kakamega.
Bila kusema kuwa watatoka nje ya Nasa, Dk. Khalwale alisisitiza kuwa Ford-Kenya sasa inajihusisha na masuala ya kujiunda upya na kushinikiza mageuzi katika mfumo wa uchaguzi na mahakama ili kuhakikisha kuwa mbio za mwaka 2022 zinakuwa huru na haki.
Mwananchi