Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilikuwa wa kubadili jina la Tanganyika

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilikuwa wa kubadili jina la Tanganyika

Kwa maoni yangu,Msingi mkubwa wa Muungano Kwa fikra zangu ni suala la Usalama wa Tanzania Bara na Visiwani na hasa baada ya mapinduzi ..Kama ilivyo Taiwan Kwa China Mainland au Ukraine Kwa Russia..Zanzibar Ina umuhimu strategically Kwa Tanganyika vivyo hivyo Kwa Nchi Za Kiarabu..

Mizizi ya Waarabu wa Oman si ya kufutika leo wala kesho..mwarabu Ana kiu na uchu wa kuirudisha Zanzibar ktk mikono yake kuliko tunavyodhani Kwa sasa kikwazo kikubwa ni Tanganyika au Serikali ya Muungano…

Kwa historia,Utamaduni wa Kiarabu umetamalaki sana ZNZ..Ndugu Zangu wa asili ya Zanzibar ni watu wapole ktk maamuzi ,Wepesi wa kupokea,Wanapenda raha ,Hawana nongwa wakishiba..Hawana hiana wakiwa na raha zao..Wana moyo mizuri wakikirimiwa vema..Ndugu zangu wa Zanzibar wenye asili ya Uarabu wao wapo aggresive kiasi kibiashara na kiutawala (Wana ushawishi)..Japo lengo Lao kuu ni kurudisha utawala wa Kisultani..

Sasa Kwa kuwa Zanzibar ni mlango kwa kuingia bara,Zamani zile masuala ya ulinzi na usalama yalihusisha physical confrontation wakati nyakati hizi (Digital age)..Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia yameleta uvumbuzi na mapinduzi ya kiusalama na ulinzi (Air,Sea,Land,Cyber ) kuna cyber attacks,drones,UAV n.k..

On the other hand ,Sio kwamba Wazanzibar wana furaha na Muungano..Wanapenda kujitawala,kuwa na Dola kamili kuwa na uwezo wa kushiriki michakato ya kimataifa (Kisiasa,Kiutamaduni,Kiuchumi,N.K)..Refer michakato mbalimbali ya kujiunga OIC,FIFA,UN,AU,IMO,etc..

Ikitokea leo Kura ya maoni kwamba wachague kujitenga na muungano (JMT) ama Kwa hakika si chini ya asilimia 96 watakubali kujitenga..Though Kwa sasa Wapo kwenye neema kubwa ya kufaidi matunda ya Muungano.. Hivi juzi gawio la fedha (Misaada,Mikopo,Riziki) kwenda Zanzibar toka JMT limeongezwa toka 4.5% mpaka 9% kupitia jitihada Za Mh Rais Samia na Mh Rais Mwinyi..Hongera viongozi Kwa maamuzi thabiti..Neema juu ya Neema.

Hakuna ndoa isiokuwa na changamoto,yapo mazuri Kwa Pande zote lakini zipo changamoto..Penye nia pana njia.
 
Back
Top Bottom