Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Ustadh Mwiba mata nyingi hupinga mawazo yako. Kumradhi yakhe (Ndo demokrasia). Lakini kwa haya mengine nakuunga mkono uelezayo ni sahihi. Hiyo kunyamaza na kupiga makofi tu japo yanaenda mrama imewakosesha mengi Wazanzibari. Endelea na msimamo wako Mwiba elezea uelezayo. Mwakyembe amefurunda -yeye.
Unajua hapa tulipo kwa kweli Tanzania imechafuka ,japo hali haionekani kwa uwazi ,lakini tunaweza kusema kuna machafuko ndani ya Tanzania ,na machafuko haya sio hali ya Zanzibar ni nchi au si Nchi lakini ujumla serikali ya Mheshimiwa Kikwete ipo mashakani ,kuanzia T/bara hadi T/Visiwani ,tunasema nchi inayumba ,uchumi wa Nchi upo katika hali mbaya sana ,jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa manung'uniko kutoka kila pembe,ndani ya serikali viongozi hawaelewani ndani ya Chama Tawala hawaelewani wala hawajui wanafanya nini maana kila wanapoziba kunatoboka kwengine ,wapinzani nao wamekuta wananchi wana uelewa mdogo hawajui wawafahamishe vipi hadi wawashawishi kuwapa kura zao ,na hata wakiwapa kura bado vyombo vya dola vipo nyuma kulinda chama cha mafisadi inakuwa ni shagala bagala tupu,ni fujo tu.
Ukiangalia viongozi tulionao ndio hao kina Mwakiembe na Mwakipapai ,woga ,wanaogopa ,kuogopa kwao kunawafanya na wao wawatishe wengine.Kila siku tunasikia mawasilisho ya mawaziri yamejaa utata lakini kwa kuogopa na kukosa adabu ,wabunge wa kundi la akina mwakiyembe wameshindwa kusitisha hata bajeti moja na makelele yao unasikia bajeti ya waziri fulani imepitishwa,tutaogopana mpaka lini wakati nchi inazama na kuzamishwa kwa bajeti zilizojaa mizengwe ,si mmesikia viwanda viwili vimeuzwa kwa bei ya kiwanda kimoja : -

Alisema jambo ambalo limeishtua zaidi kambi hiyo, ni pale ilipobaini kuwa kulikuwa na viwanda viwili ndani ya kiwanda hicho ambavyo ni K1 chenye ukubwa wa hekta 6,214.5 na K2 ekari 3,153, lakini vyote vilihesabiwa kama kiwanda kimoja na kuuzwa kwa bei ya Sh16 bilioni.
"Kambi ya upinzani inaitaka serikali itoe majibu sahihi inakuaje viwanda viwili vyenye eneo la jumla ya ekta 9,367.5 viuzwe sawa na kiwanda kimoja cha Mtibwa?" alihoji Owenya na kusisitiza

Hapa si sehemu ya upinzani bali ni sehemu pia inayowahusu akina Mwakiyembe na Mwakipapai Je walisema kitu gani ? Au waliogopa kumukosea adabu Waziri husika na kuonekana hawana adabu ?

Akizungumzia Kiwanda cha Mgololo kilichobinafsishwa kwa Kampuni ya RAI Group Ltd ya Kenya mwaka 2004, Owenya alisema kauli ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko aliyoitoa bungeni mwishoni mwa wiki imezidi kuzua utata kwa kuwa mkataba wa mauziano una upungufu mkubwa ambao upinzani unahitaji ufafanuzi.
Alisema kuwa, upungufu huo ni pamoja na tofauti za bei ya mauzo katika mkataba huo ambazo zimeonyesha tofauti kubwa ya fedha kati ya bei ya mauziano ya awali na maelezo ya mkataba.

Mwakiembe na Mwakipapai hapa mnahusika au hamhusiki katika kuhoji au mpo hapo kulinda mafisadi tu ,kazi iliyopo hapa ndio inayokuhusu Mheshimiwa Mwakiembe uivalie njuga uwe tayari kumhoji waziri na serikali yake,na sio mambo ya Zanzibar hayo huyawezi labda kwa kutoa amri za fulani asulubiwe maana unajikomba kwa wakubwa ambao wao wenyewe wanakiri mambo ya Zanzibar ni mazito na sio mchezo hata mtoto mdogo akikwambia Zanzibar ni Nchi basi bora unyamaze la si hivyo atakuumbua na utake kumuadhibu.
 
MWAKYEMBE APONGEZWE: UNAFIKI UMEZIDI TANZANIA
Nimeufuatilia mjadala huu vizuri na kulazimika kutafuta kanda ya video inayomnukuu Dk. Mwakyembe live. Washikaji wengi wamepotoka na kumwelewa Dk. Mwakyembe vibaya kutokana na uandishi mbovu wa magazeti Tanzania. Dk. Mwakyembe anasema: wabunge na wananchi ni ruksa kusema chochote kuhusu Serikali yao, lakini mawaziri wanashikwa na kanuni ya kikatiba ya "collective ministerial responsibility" ambapo wakitaka kuikosoa Serikali au kiongozi wa Serikali, lazima wajiuzulu uwaziri kwanza. Kwa point hiyo Mwakyembe is correct. Tumeona ikitokea kwenye Serikali zote za kistaarabu. Wapi na watu, kiongozi mdogo kama Shamhuna unamvaa Prime Minister? Hiyo serikali au gulio? I wish we had many Mwakyembes in Tanzania. Anastahili kupongzezwa sanaaaaa!
 
Hapa Kuna Tatizo Kubwa La Uelewa! Sidhani Kama Mwiba Anaielewa Issue Hii Aliyoianzisha. Unamhukumu Mtu Bure Bila Sababu Kwa Sababu Source Yako Ni Mtanzania Na Tanzania Daima Ambayo Imereport The Matter Nusu Nusu. The Mp Here Was Dealing With A Constitutional Matter. Kwako Mwiba Ni Suala La Ubishani Tu, Bila Context, Bila Kiini N.k. Nakushauri Ingia Kwenye Hansard Ya Bunge, Utajisikia Vibaya Mwenyewe Kuwa Ulikuwa Unaendesha Crusade Bomu, Unless Hiyo Ndo Assigment Yako, Maana Tanzania Inao Wengi Hao Wa "special Assignment".
 
Unajua sometimes Kikwete huwa anajaribu kufikiri sawa ingawa sio wakati wote, siku moja alimuambia Shamuhuna kuwa atamnyanga'nya vingora maana inaonekana vinampa taabu sana, kumbe alikuwa na ukweli,

Sasa anajua kuwa Muungwana yuko kwenye line na Bilali, kwa hiyo yale ya yeye na mtandao yameisha, amesahahu kuwa hata nafasi ya Deupty Waziri Kiongozi haipo kwenye katiba za Jamhuri au Visiwai, ila kilianzishwa tu kwa makubaliano kati ya Muungwana na Karume, kumsitiri Shamuhuna baada ya Mkapa kumgomea kuwa Makamu wa Rais wa Bara,

Mwakyembe anahitaji hongera kwa kuweka ukweli wazi bila kumuogopa huyu former Mtandao, can you imgine huyu ndio angkeuwa makamu wa rais wa Jamhuri? Damn! Halafu eti antaka kuwa rais wa Visiwani?
 
Mwakyembe is very right. I would expect these strong words to have been uttered by the president and the issue of Zanzibar would have come into the end. Leaving this issue of whether Zanzibar is a sovereign state or not into the hands of Sitta and people like Shamhuna it gives much worries if proper answer/solution can be obtained.

Good point. Kudos!
 
Field Marshall umegonga ndipo! Umeonyesha ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa. Hata mimi sasa najiuliza, huyu njemba angekuwa Makamu wa Rais, nchi ingelikuwa shwari au imesambaratika?
 
Mhadhiri Chuo Kikuu Dar ataka mdahalo wa `Zanzibar ni nchi`

2008-08-15 16:52:46
Na Haji Mbaruku, Jijini

Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk. Sengondo Mvungi, ameishauri Serikali ya Muungano kuitisha mdahalo utakaowezesha kumaliza utata kuhusiana na hoja ya kama Zanzibar ni nchi ama la.

Dk. Mvungi amesema kuwa bila kufanya hivyo, malalamiko kuhusiana na hoja hiyo yataendelea kushika kasi siku hadi siku.
Mhadhiri huyo wa sheria alikuwa akihojiwa na kituo kimoja cha redio hapa jijini.

Dk. Mvungi ambaye amewahi kugombea urais mwaka 2005 kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, amesema mdahalo ndio njia pekee ya kumaliza suala hilo.

Hoja ya Zanzibar sio nchi ilianzia bungeni mjini Dodoma wakati Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda akijibu maswali ya wabunge kama utaratibu wake alivyojiwekea.

Swali hilo ambalo liliulizwa na mbunge mmoja wa CUF, lilijibiwa na Waziri Pinda kuwa Zanzibar sio nchi.

Tangu kutolewa kwa majibu hayo, hoja mbalimbali zimekuwa zikitolewa kuhusiana na suala hilo.

Mwanasheria mkuu wa Zanzibar, Bw. Pandu Hassan alikaririwa akisema Zanzibar ni nchi, kabla ya wajumbe wa Baraza la wawakilishi kuchachamaa zaidi.

Hata pale, spika wa baraza la wawakilishi alipopiga `stop` suala hilo kuendelea kujadiliwa, wajumbe wa baraza waliendelea kuchomekea suala hilo kabla baadaye kutakiwa liachwe kwa wanasheria wa pande zote mbili ili wakae na kuyatolea ufafanuzi muafaka.

SOURCE: Alasiri
 
Hapa ni unafiki tu wa wachache ambao wanafikiri Zanzibar ikijitenga watafaidi. Baada ya hapo watataka na Pemba nao wajitenge, baadaye watataka hata vitongoji vijitenge na mwisho wake watataka nyumba nazo zijitenge. What a SIc thing!
 
Field Marshall amefanya analysis. Sasa hawa wengine akina Mwiba analysis ni hisia na bendera kufuata upepo maana hata suala la Lowassa kufukuzwa na Mwakyembe lilivyoingizwa humu, halieleweki! Kuna ka"element" ka chuki binafsi hapa, si ajabu huyu ni Karamagi mwenyewe using a pen-name. Hasira za kishabiki unaziona pale ambapo Mwiba anajaribu sana kuharibu jina la Mwakyembe na kumwongezea jina la "Mwakipapai" mbele ya jina lake. Huu ni udaku mzee Mwiba, kid-stuff, ukizingatia role aliyoplay Mwakyembe katika kuleta sanity kwenye system!
 
.....lets assume ulichoandika hapo juu ni sahihi.........sasa wewe kwa hiyo hoja je unakubaliana na justification ya kulinganisha anayoifanya Nudgu Mwiba kuwa Dr Mwakyembe..........kamchafua Lowassa na eti kwa kuwa Kamati yake haikuyasema maovu yote then anastahili kuadhibiwa?

.....where do we draw the line between the two here.......? where is the correlation....?

......Mkuu Mwiba nahisi kuna mtu kaiba password yako.....ama?

Mkuu Ogah, sikubaliani kabisa na anachosema MWIBA lakini naheshimu courage yake kuja hapa na kusema kile anachokiamini yeye. Dr Mwakyembe did a good job on Lowassa, hata kama hakusema yote aliyotaka kuyasema, dozi aliyotoa ilikuwa inatosha kabisa 'kumkoma Nyani'.Utakuwa umemchafua mtu kama utasema maneno ya uongo na uzushi kuhusu yeye, sidhani kama that is the case kama utasema ukweli lakini usiuseme wote! Na naamni kama ile kamati ingeongozwa na mtu mwingine huenda mambo mengi zaidi yangefunikwa.
 
Aliyeuliza swali lwa Zanzibar kama ni nchi ama la ni Mzanzibari, na kwa lugha ya mitaani, alijua kuwa anawasha moto wa makusudi. Hii inakufanya ufikirie zaidi kama ni hivyo, what was the motive behind? Je yeye hajui kama zanzibar ni nchi au si nchi kweli? au ametumwa? Na nani? 44 yrs after Union, kwa nini swali hili liulizwe? Walikuwa wanaishi wapi...kwenye nchi au kusiko nchi?

Kelele nyingi zimepigwa bara na visiwani ili katiba ifanyiwe mabadiliko haswa kwenye mapungufu yaliyomo kuhusu suala la muungano lakini serekali imetia pamba masikioni. Nadhani Shamhuna 'ametumwa' na kundi fulani la watu and all credits to him for having the courage 'kumfunga paka kengele', huenda huu ukawa mwanzo wa mambo makubwa ambayo wengi hatukutarajia kuyaona.
 
Hapa ni unafiki tu wa wachache ambao wanafikiri Zanzibar ikijitenga watafaidi. Baada ya hapo watataka na Pemba nao wajitenge, baadaye watataka hata vitongoji vijitenge na mwisho wake watataka nyumba nazo zijitenge. What a SIc thing!
Pemba na Unguja haziwezi kujitenga na hata ikihitajika hivyo hilo litakuwa sio la Tanzania tena ni lao wenyewe, wewe subiri tu kwa muendesho huu wa serikali unavyokwenda basi hata huko Tanganyika si ajabu ukasikia madai kutoka kwa wananchi wakitaka wajitenge,wazungu walifanya vibaya sana ila kwa maarifa yao ,kuigawa Africa katika mapande makubwa makubwa ,jambo ambalo ukitazama huko kwao nchi zao sawa na mikoa yetu ,na ubora huo umewafanya waishi kwa kutunzana na kuheshimiana ,lakini Nchi karibuni zote za Afrika ni lazima usafiri siku tatu ndio ufike mpaka wa upande wa pili.
jaribuni kutazama nchi za Ulaya pia angalieni matatizo mengi ni nchi gani kulinganisha na ukubwa yanakuwa nchi zao haziishi matatizo.
Let us Zanzibar Go and see what will happen in the near future in African continent.Anzeni kuisaka mipaka ya sukuma land.
 
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yamtaka Mwakiyembe aombe Radhi
 
Mwiba

Unachekesha sana natumaini unaona yanayotokea Georgia na kuona kuna nchi ndogo kama Rwanda, Burundi au Togo, swaziland, Lesotho n.k.

Tamaa ya fisi itakuponza huwezi kuongea hapa kama vile unawaongelea Wazanzibari wote kwani mlipojiunga kutoka Afroshiraz to CCM mlilazimishwa? Tena Zanzibar ndio mlifurahia sana rejea hotuba ya mchonga kule Zanzibar. Mimi sioni ubaya wa wewe na mawazo yako hata CUF wanafikiri hivyo hivyo kwa kutegemea kufaidi lakini usisahau ukishaanza kula nyama ya binadamu huwezi kuacha kwani ni tamu kweli kweli ndio ilivyo kwa MAFISADI.
 
Unajua sometimes Kikwete huwa anajaribu kufikiri sawa ingawa sio wakati wote, siku moja alimuambia Shamuhuna kuwa atamnyanga'nya vingora maana inaonekana vinampa taabu sana, kumbe alikuwa na ukweli,

Sasa anajua kuwa Muungwana yuko kwenye line na Bilali, kwa hiyo yale ya yeye na mtandao yameisha, amesahahu kuwa hata nafasi ya Deupty Waziri Kiongozi haipo kwenye katiba za Jamhuri au Visiwai, ila kilianzishwa tu kwa makubaliano kati ya Muungwana na Karume, kumsitiri Shamuhuna baada ya Mkapa kumgomea kuwa Makamu wa Rais wa Bara,
Mwakyembe anahitaji hongera kwa kuweka ukweli wazi bila kumuogopa huyu former Mtandao, can you imgine huyu ndio angkeuwa makamu wa rais wa Jamhuri? Damn! Halafu eti antaka kuwa rais wa Visiwani?
Yaani mkuki kwa nguluwe au sio ,pale Shamhuna alisema hakuna selikali ya Mseto wala choloko ,akina Mwakiyembe walipiga makofi,sasa inakuwaje leo aombe lazi.tamko rasmi kutoka serikalini SMZ mmelisikia ni majibu kutoka CCM kisiwa ndui Zanzibar(Wahafidhina wakiitaka timu ya Butiama iombe razi)
 
MWAKYEMBE APONGEZWE: UNAFIKI UMEZIDI TANZANIA
Nimeufuatilia mjadala huu vizuri na kulazimika kutafuta kanda ya video inayomnukuu Dk. Mwakyembe live. Washikaji wengi wamepotoka na kumwelewa Dk. Mwakyembe vibaya kutokana na uandishi mbovu wa magazeti Tanzania. Dk. Mwakyembe anasema: wabunge na wananchi ni ruksa kusema chochote kuhusu Serikali yao, lakini mawaziri wanashikwa na kanuni ya kikatiba ya "collective ministerial responsibility" ambapo wakitaka kuikosoa Serikali au kiongozi wa Serikali, lazima wajiuzulu uwaziri kwanza. Kwa point hiyo Mwakyembe is correct. Tumeona ikitokea kwenye Serikali zote za kistaarabu. Wapi na watu, kiongozi mdogo kama Shamhuna unamvaa Prime Minister? Hiyo serikali au gulio? I wish we had many Mwakyembes in Tanzania. Anastahili kupongzezwa sanaaaaa!

Hongera kwa kufanya kazi ya kujaribu kumsafisha shujaa wenu lakini ulishindwa kufanya utafiti wa kujua madaraka ya Shamuhuna na yale ya Pinda.
Mwakyembe anapozungumzia mawaziri anataka kutwambia kuwa Mawaziri wa Zanzibar wapo chini ya Waziri Mkuu kwani Shamuhuna ni Waziri wa SMZ. Mbona tu wagumu kufahamu kuwa Serikali ya Mapinduzi ni tofauti na Serikali ya Muungano na hakuna pahala popote ndani ya Katiba panapoonyesha uhusiano kati ya vyombo viwili hivi. Aidha Bunge na Baraza la Wawakilishi ni vitu viwili tofauti. Pinda ni bosi wa Bunge na Shamuhuna ni bosi Baraza la Wawakilishi na kilichofanyika ni kwa Pinda kutamba katika himaya yake na Shamuhuna yake sasa Mwakyembe analeta kiherehere cha nini?
 
Hapa Kuna Tatizo Kubwa La Uelewa! Sidhani Kama Mwiba Anaielewa Issue Hii Aliyoianzisha. Unamhukumu Mtu Bure Bila Sababu Kwa Sababu Source Yako Ni Mtanzania Na Tanzania Daima Ambayo Imereport The Matter Nusu Nusu. The Mp Here Was Dealing With A Constitutional Matter. Kwako Mwiba Ni Suala La Ubishani Tu, Bila Context, Bila Kiini N.k. Nakushauri Ingia Kwenye Hansard Ya Bunge, Utajisikia Vibaya Mwenyewe Kuwa Ulikuwa Unaendesha Crusade Bomu, Unless Hiyo Ndo Assigment Yako, Maana Tanzania Inao Wengi Hao Wa "special Assignment".

Jee kuna kipengere kwenye Katiba kinachosema kuwa kumpinga Waziri Mkuu ni KOSA? Na jee Mwakyembe au Bunge linauwezo gani juu ya Shamuhuna na nini adhabu ya"kosa" la Shamuhuna kwa kanuni za Bunge?
Usipoyajibu hayo basi Mwakyembe ni fyongo.
 
Unajua sometimes Kikwete huwa anajaribu kufikiri sawa ingawa sio wakati wote, siku moja alimuambia Shamuhuna kuwa atamnyanga'nya vingora maana inaonekana vinampa taabu sana, kumbe alikuwa na ukweli,

Sasa anajua kuwa Muungwana yuko kwenye line na Bilali, kwa hiyo yale ya yeye na mtandao yameisha, amesahahu kuwa hata nafasi ya Deupty Waziri Kiongozi haipo kwenye katiba za Jamhuri au Visiwai, ila kilianzishwa tu kwa makubaliano kati ya Muungwana na Karume, kumsitiri Shamuhuna baada ya Mkapa kumgomea kuwa Makamu wa Rais wa Bara,

Mwakyembe anahitaji hongera kwa kuweka ukweli wazi bila kumuogopa huyu former Mtandao, can you imgine huyu ndio angkeuwa makamu wa rais wa Jamhuri? Damn! Halafu eti antaka kuwa rais wa Visiwani?

Unapozungumza kuwa mkweli mwanzo mpaka mwisho. Ivo umesahau yule Mnyamwezi wa Tabora ndie alikuwa Deputy Chief Minister wa mwanzo?
 
Hongera kwa kufanya kazi ya kujaribu kumsafisha shujaa wenu lakini ulishindwa kufanya utafiti wa kujua madaraka ya Shamuhuna na yale ya Pinda.
Mwakyembe anapozungumzia mawaziri anataka kutwambia kuwa Mawaziri wa Zanzibar wapo chini ya Waziri Mkuu kwani Shamuhuna ni Waziri wa SMZ. Mbona tu wagumu kufahamu kuwa Serikali ya Mapinduzi ni tofauti na Serikali ya Muungano na hakuna pahala popote ndani ya Katiba panapoonyesha uhusiano kati ya vyombo viwili hivi. Aidha Bunge na Baraza la Wawakilishi ni vitu viwili tofauti. Pinda ni bosi wa Bunge na Shamuhuna ni bosi Baraza la Wawakilishi na kilichofanyika ni kwa Pinda kutamba katika himaya yake na Shamuhuna yake sasa Mwakyembe analeta kiherehere cha nini?

Halafu huyu Mwakiyembe ni mchochezi na hajui maana halisi ya neno Fedheha kwa taifa kama ni fedheha basi Tanzania ilipata fedheha kwa kutoa wakimbizi waliokimbilia shimoni baada ya unyama wa dictator nduli Benyamin kuyapeleka majeshi Zanzibar na kwenda kuuwa na kufanya ushenzi wa kupindukia kule Pemba , mnaoulinda Muungano haya ndio mnayoyaunga mkono na hamna jingine ,kusema Muungano hauna kasoro unafaida zaidi kwa Zanzibar ni kwa haya ya akina Mwakiyembe kusimama kifua mbele kusema Shamhuna kakosa adabu , mwakiyembe amepata mdomo kwa sababu ya kuwazamisha wenziwe na hivyo hapo alipo anatumiliwa tu na muda wake ukiisha atatupwa jalalani kama wengine ,msemo wa Kiswahili husema kila ngoma ivumapo ndipo inapokalibia kupasuka wako wapi magogo ya CCM ambayo yakisifika ,na yakitembea bega kwa bega na Nyerere ,leo hii si tumeona wamepigwa buti kwenye kinyang'anyiro cha Uraisi ,na wengine wowote wale huwa wanatumiliwaga tu ,yupo wapi Mangula ? hata humsikii mtu ambae alikuwa ni mtetezi wa CCM kwa hali na roho,Mwakiyembe fahamu tu Waziri Pinda alishaliona kosa lake na hadi hii leo hakurupuki tena kujibu masuala yanayohusu Muungano ,na kila siku tunasikia Sitta anavyomukinga.Imeonekana Waziri Mkuu hakupata mafunzo ya kujibu masuala ya papo kwa papo kitu ambacho kiongozi wa juu ni lazima akutane na usalama wa Taifa wamfundishe namna ya kujibu.
Mimi Mwiba kama suala aliloulizwa Pinda ningeulizwa basi ningelijibu kwa ufasaha kabisa tena kwa maneno mafupi na watu wa pande zote mbili wangeliridhika.
Ila Muheshimiwa Pinda ameteleza na hili halina mjadala ,hasa ukiichukulia maana ya kuteleza.
 
Mwiba

Unachekesha sana natumaini unaona yanayotokea Georgia na kuona kuna nchi ndogo kama Rwanda, Burundi au Togo, swaziland, Lesotho n.k.

Tamaa ya fisi itakuponza huwezi kuongea hapa kama vile unawaongelea Wazanzibari wote kwani mlipojiunga kutoka Afroshiraz to CCM mlilazimishwa? Tena Zanzibar ndio mlifurahia sana rejea hotuba ya mchonga kule Zanzibar. Mimi sioni ubaya wa wewe na mawazo yako hata CUF wanafikiri hivyo hivyo kwa kutegemea kufaidi lakini usisahau ukishaanza kula nyama ya binadamu huwezi kuacha kwani ni tamu kweli kweli ndio ilivyo kwa MAFISADI.

Tatizo lenu lenu kuwa mkimuamii mtu mnakuwa karibu ya kumuabudu kwani huyo Nyerere ni nani kwa Wazanzibari/ Ni kweli kuwa Wazanzibari walidanganyika na ulahai wake kama Watanganyika walivyohadaiwa na Ujamaa wake. Mbona baada ya kuona mlivyodanganywa mliamua kuutupilia mbali Ujamaa na Wazanzibari wameshajua kuwa Muungano kwa namna ulivyo sasa hauwafaidii na hivyo wanataka mabadiliko na kama mnafutuka na kuuvunja muungano potelea kwa mbali. Hebu jaribuni kuachia hatamu na muone mtakavyokimbiwa mbali.
 
Back
Top Bottom