)
Matatizo ya sasa ya kisiasa Zanzibar hayawezi kutatuliwa kwa kujaribu ku-vent frustrations zenu on viongozi kama Mwakyembe, ni kufukuza hewa,
toeni ushauri wa namna ya kuumaliza mgogoro wenu wa muafaka huko Visiwani, ni nyinyi wenye matatizo in the first place,
kauli za Shamuhuna ni za kushauriwa na washauri wabovu kuwa ajaribu kum-bully Muungwana, ili ampe nafasi ya kugombea urais wa huko wakati muungwana ameshaamua kwenda na Bilali, kwa sababu anahitaji a strong hand ya ku-deal na siasa za huko, Shamuhuna mpambe wa Rostam hana huo ubavu, na besides hana ukaribu sana na muungwana kuliko Khatibu na Ameir,
na hicho cheo kulikuwa ni one term only maana Mtandao sasa hauhitaji tena watu kama Shamuhuna, ili kushinda term ya pili, kwa hiyo he is doomed sasa anaweza kupiga kelele as much as he wants, ndio maana kina Husein Mwinyi, walihamishiwa huko, ni ili waje wazibe nafasi za kina Shamuhuna.
Ahsante Mkuu.
Mkuu mwenzetu shukurani sana kwa uelewa wako wa siasa za Zanzibar lakini kwa hili naona hujalipatia.
Issue iliopo sasa hauhusu maisha ya kisiasa ya mtu mmoja yaani Shamuhuna bali ni issue inayoikabili CCM yote Zanzibar. Aidha elewa kuwa CCM wanajidanganya kumuweka Bilali kwenye nafasi ya Urais kwani kitendo chake cha kujiunga na upande wa Bara dhidi ya kuitambua Zanzibar kama nchi hakivumiliki kwa Wazanzibari wote bila kujali itikadi zao.
Mkuu elewa kuwa hii issue ya kutotambuliwa inamuumiza kichwa hata Amani mwenyewe kwani ili ubaki kwenye madaraka basi Wazanzibari wajue kuwa wana nchi yao kama Zanzibar.
Baada ya hapo turudi kwa Mwakyembe, yeyote mwenye kutowa kauli ya kutoitambuwa Zanzibar atakuwa anajitia kwenye makinzano na Wazanzibari kwani kwao wao katiba au nguvu Zanzibar ni nchi na imo kwenye Muungano kama nchi kwani haijapata kuuzwa bali iliungana. Inaafaa kueleweka kuwa Wazanzibari wanataka Muungano wa kuheshimiana na sio upande mmoja ujione kuwa una mamlaka yote kwa Zanzibari na hivyo watasshughulikiwa watu kama Mwakyembe kama Mwakyembe kwani imani ni kuwa Watanzania wanaelewa kuwa Zanzibar ni nchi katika Muungano wa nchi na sio mikoa au wilaya.