Mimi nimestushwa... na the so called defence system! kama ilivyo quoted kwenye original post!

Hilo ni neno zito sana na jipya kulisikia kwenye sakata hili,,, ambalo waandishi wa habari wana haja/wajibu wa kuhitaji clarification zaidi kutoka kwa msemaji huyo.

Kumbukeni... Jeshi la Poli ni (Usalama wa Raia) ni tofauti na TPDF (Tanzania Peoples Defence force)!

Mtu anaposema kuna version ya TPDF kule Zanzibar lazima aulizwe vizuri...

Hili la bendera sina shida nalo... hata Jiji la Dar es Salaam... na halmashauri zote zina bendera zao... alafu pia shule zina nyimbo zao za shule mfano Ilboru Sekondari niliwahi kuambiwa wa wimbo wa shule... no issue on this!
 
Tuwe na serikali moja au tuvunje Muungano haya mambo ya kusema sijui tume ya kufuatilia na kutatua kero za muungano haisaidii kitu.

IMO...Muungano uvunjwe tuu.
 
(1) Jamaa anayedai kuwa waziri wa serikali ya mapinduzi hawajibniki kwa waziri mkuu wa Tanzania ni mpuuzi kabisa. Huyu hafai hata kuwa kiongozi kwa vile hajui itifaki. Hivi hajui kuwa mkulima wa kijijini pamoja na kutokuwah mtumishi wa serikali, lazima anawaheshimu mawaziri wote wa muungano na wale wa serikali ya mapinduzi? Kama zanzibar ni sovereign state, kwa nini basi raisi wake Karume awe ni sehemu ya baraza la mawaziri wa Serikali ya jamhuri ya Muungano, tena akiwa chini ya waziri mkuu? Itifaki kwenye cabinet ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu halafu Raisi wa Zanzibar, mawaziri wote, mwanasheria mkuu

(2) Mtu wa kuadhibiwa hapa siyo yule anayedai kuwa Zanzibar ni sovereign state, bali maraisi wote wawili: Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Raisi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kushindwa kulinda na kutetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama walivyoapa wakati wanachukua madaraka waliyo nayo.
 
Soma magazeti ya leo au jana wamesema wana mfumo wao wa ulinzi.

La pili, Mizengo Pinda ni waziri mkuu wa JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA. No inakujaje hapo? naomba kueleweshwa!


Unaamini magazeti au Katiba ya Jamhuri ya Muungano?
 
Ama kweli Muungano tuliuingia bila Wataalam wanaofahamu nini maana ya Muungano..
Hivi kweli hawa watu wanaweza kutoa mfano wowote ule wa Muungano wowote ule ambao PM wa serikali kuu ya Muungano yup chini ya PM wa jimbo iwe province ama State!...
Hapa canada kuna PM wa Muungano wa majimbo yote na hakuna provincial Premier anayeweza kusema ati PM hana madaraka ktk serikali za Province hizo...Upupu wa viongozi waliosoma darasani bila kuwa exposed na Utawala.
Hilo jeshi la KMKM kama ndio wanalizungumzia ni sehemu ya Jeshi la Taifa. Hata huku yao majimbo yenye majeshi na yana majina tofauti laini huwezi kutenganisha nchi nzima kwa kutumia kikosi cha jeshi fulani..
Kuwepo kwa bendera za Kimajimbo haina maana kabisa kuwa Zanzibar ni nchi kwani hata Pemba na Unguja wanazo bendera zao kutokana na mipaka ya territorial ambayo haitengenezi nchi. Hata bara wakumbuke tunayo bendera yetu ambayo imemezwa na ile ya Jamhuri kutokana na Muungano..

Ningeomba hawa viongozi waliosema maneno haya kwanza wapewe ziara ktk nchi zenye Muungano wakajifunze huko waelewe nini maana ya Muungano kisha wajenge hoja zao wakifahamu madaraka ya PM wa Jamhuri yanaishia wapi!..
Labda kosa kubwa lililofanyika ni kuwepo kwa rais wa Zanzibar na rais wa jamhuri ya Tanzania kiasi kwamba WaZanzibar wameshindwa kuelewa hata nafasi ya Kikwete nchini kwao. Utaratibu wote wa kuchagua viongozi ktk ngazi za KULA ndio sababu kubwa ya mgogoro huu hakuna kipya!
 
KMKM ni Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo.

Sio jeshi la ulinzi. ila nawalaumu waandishi wetu ambao hawakuhoji huo ulinzi. jamaa wa Zenji kwa mara nyingine wanaanika ujinga wao. Samahani Dr Who aka game theory.

Zenji to me ni mkoa tu tena wenye watu wasiojilewa na wasio elewa muungano ni nini.
 
Waacheni Wazanzibari wajitawale wenyewe. Mambo ya kushikilia nchi za watu huku huna pesa za kuwapa ni bugudha tupu.

Kwa Wazanzibari sisi wabara ni kama wakoloni tu. Sasa kama tunajifanya hatuelewi huku sisi wenyewe tunapinga ukoloni, hiyo sio double standard?

Mimi nafikiri tuwape uhuru na waamue kwa kura huru kama wanataka kujitenga au la. Tukijifanya tuna manguvu kama Russia wakati ukweli ni kwamba hatuna hayo manguvu, tutaumia bure.
 

Kweli, KMKM si jeshi la ulinzi: Hiki ni kikosi maalum cha polisi wa majini kilichoanzishwa kupambana na magendo huko Zanzibar. JKU kama JKT ni kikosi ambacho kilianzishwa ili kuwafundisha vijana mafunzo na nidhamu ya kijeshi; vikosi hivi (JKU na JKT) vinalelewa na JWTZ, lakini huwezi kuviita kuwa ni majeshi ya ulinzi.


Zanzibar siyo mkoa, ila ni sehemu ya nchi ijulikanayo kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tatizo kubwa hapa ni kwa vile Zanzibar ina serikali yake ya ndani, basi viongozi wa serikali hii wanataka kuwa madaraka makubwa zaidi ya waliyopewa kikatiba kwa kujaribu kujibebesha pia madaraka yaliyo chini ya serikali ya Jamhuri ya Muungano.
 
Hawa jamaa wanatangaza secession na Rais wa Muungano anabaki kucheka cheka tu!!

Mkjj

Naungana na wewe, hata nyumbani baba akiwa ana cheka cheka sana na watoto wanapunguza heshima na hata kuaibisha mbele ya wageni. Rais wetu amekuwa soft sana, wanajua hilo kwani enzi za BWM hawa jamaa walikuwa na heshima na serikali ya Muungano.

JK anatakiwa achukue hatua na aanze na wote wenye tuhuma za ufisadi kama kina Lowassa, RA, Chenge n.k. Akishawashughulikia hawa jamaa watamuheshimu kama Rais wa Tanzania, kwani kachaguliwa na watanzania wote Bara na visiwani.

Hawa wazenji wanajaribu kuchokonoa nyuki kwenye mzinga. na kwa kuwa sasa hivi Nyuki hawaumi? wanaanza kuwatia mifukoni na makwapani. Uoga wa kina JK Muungano kuwafia mikononi mwao ndio unawapa kibri SMZ. Mbona Nyerere aliwawajibisha akina AJ na SSH?.

Lakini pia ukiangalia upande wa pili wa sarafu inawezekana hawa Jamaa CCM, wapo kwenye strategy ya kuwasahaulisha wadanganyika mjadala juu ya UFISADI unaofanywa na CCM na kushinikiza hatua kuchukuliwa kwa wale wote walioshiriki. "Strategic distortion of Gland Corruption Forums towards 2010".
 
..nilikuwa nasubiri jibu toka visiwani,baada ya mwakyembe ku-fill the vacuum ya uongozi kwenye suala hili.

..jibu limepatikana. and make no mistake about it, hiyo ndio kauli na msimamo wa serikali ya mapinduzi.

..mwaka huu kabla hujesha, tutaona mengi!
 
Ukisoma maandishi hapa wengi ni Watanzania bara, je tuko tayari kusikia hoja za Wazanzibari? Au ndio tumeamua kuwa bullies?

Huu muungano wetu una matatizo makubwa. Mimi nafikiri njia pekee ni kuwapa wazanzibari nafasi ya kuamua kama wanataka kuendelea kuwa kwenye muungano au la. Vinginevyo wakitaka kujitenga wacha wajitenge. Hakuna haja ya kulazimisha ndoa ambayo imeingia mchanga.
 


..maneno haya waambie wazee wako wa bara usikie watakachosema.

..kama unataka kuachiwa radhi.
 
The centerpiece of the argument raised by the original post echoes an earlier post of mine which questioned Dr. Mwakyembe's criticism of Shamhuna's lack of collective responsibility due to an ambiguos hierarchy in the Tanzanian union structure.

Augustoon posted a detailed post which pointed out the fallability of the Union due to some legal foundations.

I proposed, and further supports an immediate (2010), uneiquivocal and banal declaration of endorsement of a simple majority referendum on the Union.If Kikwete does nothing else right in his administration, but get this right, he will have redeemed his legacy sufficiently successfuly in my book.
 
Acheni jazba ,inaonekana hata humu mumepoteza muelekeo na sasa ni wazi uzalendo wa Utanganyika unawaandama japo wengine mnaota kuwa Tanganyika ilikwisha kufa,hao siwezi kuwaelewesha ni sawa na kumtambua mwendawazimu aliepona na kumpa uhuru.
Hizi serikali mbili ni tofauti ,na kila serikali ina mamlaka yake na mipaka yake ,sasa inapohojiwa kuwa Je serikali ya Muungano ina mamlaka juu ya serikali ya Zanzibar ,msiwe na pupa na kukurupuka na kujijibu wenyewe ,maana mnajiuliza halafu mnajijibu ,kwa nini msitazame mipaka ya serikali hizi ? Mimi sitaki kuweko upande wenu kwa mnayoyaona mambo haya ni mepesi na hivyo mnajibu vile mnavyojiuliza wenyewe ,very interesting !
Sijui Mwakiyembe ni Mwanasheria atulie na hawezi kujibu hoja hizi za viongozi wa Zanzibar maana ni za kipumbavu, nilisema katika ile topik ya Mwakiyembe ndie aliekuwa hana adabu ,maana amevunja hata amri ya Spika ,mnakuja na kuhoji eti nikatazame nukuu za Bunge , mimi si mwana siasa wala mwanasheria ni mlala hoi tu,lakini kauli ya Mwakiyembe at the first hearingi niliiona amekwisha kosea kwa maneno aliyotumia ,haihitaji misamiati mingi kuielezea na nilisema Mwakiyembe akibanwa basi atakuwa matatani kwa kauli aliyotumia hasa maneno au lugha chafu ,nikatoa Chalenge ,yatazamwe maneno aliyosema Shamhuna na aliyosema Mwakiyembe ,mnaposikia kila ngoma ikivuma ndipo inapokaribia kupasuka ,Mwakiyembe amepasuka na sasa hafai na ametoa mtihani mwengine kwa Bunge na Raisi Kikwete ,japo kwa mtazamo wenu mnaona hana kosa ,lakini sivyo Mwakiyembe ametenda kosa tena baya zaidi hata kuliko wale wanaosema Zanzibar si nchi.
Ninachowataka msiingie katika kujigawa mkaona labda Mwiba niMpemba Mzanzibari anatetea WaZanzibari na Mwakiyembe ni mwenzetu Chogo basi tumlinde ,mtakuwa mnakosea , mimi ninaweza kuwa bora kwa Mwakiyembe kuliko nyinyi mnaojidai kumlinda na kumkazania ashike na kusimamia msimamo wake ,hamumtakii mwema Mwakiembe , mmesikia mmoja alipohojiwa kuhusu madai ya Zanzibar na kauli ya Mwakiyembe na taratibu za Bunge ,jamaa alijibu waandishi nendeni katafuteni ,soma hiki kipande :-
...Naye Naibu Spika wa Bunge, Bibi Anne Makinda alipoulizwa kuhusu kanuni za Bunge zinasemaje kuhusu shinikizo anazopewa Dkt. Mwakyembe, alimtaka mwandishi azitafute ili ajionee mwenyewe... Umeona ustadi wa kukwepa suala ,huyu Bibi Anne ameshaona tatizo linalomnyemelea Mwakiyembe.
Ushauri wa bure kwa Mwakiyembe ,awaombe radhi ikiwa anajiona ana kosa au hana kosa na atakuwa amefunga mjadala kiustaarabu kabisa.Mwakiyembe afahamu kuwa yeye ni mbunge na natumai anaifahamu CCM vilivyo ,Mwakiyembe amegusa sega ,sega ambalo linawanufaisha magogo wa CCM bara , natumai mtaiona factor na hatari inayoplay kwa Mwakiyembe.
 
Mbona hamuidai Tanganyika na mmeng'ang'ania Muungano ? Yupo wapi Mtikila ? Ipo wapi G-55 ? Sababu gani zinamfanya Mtikila na Kundi la G-55 kuidai Utaifa wa Tanganyika ? Je hao ni au walikuwa wajinga ? Wasioitakia mema Tanzania ?
 
..hivi, haya mafuta ambayo hata bado kuchimbwa ndio yanayoleta sokomoko lote hili?, yakichimbwa je?
 
..hivi, haya mafuta ambayo hata bado kuchimbwa ndio yanayoleta sokomoko lote hili?, yakichimbwa je?

Sababu si Mafuta bali ni Mafisadi ,hivi unafahamu kuwa Serikali ya Zanzibar hawana mafiasadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…