5) Without prejudice to the application of the Constitution
of Zanzibar in accordance with this Constitution concerning all
matters pertaining to Tanzania Zanzibar which are not Union
Matters, this Constitution shall have the force of law in the whole
of the Republic, and in the event any other law conflicts with the
provisions contained in this Constitution, the Constitution shall
prevail and that other law, to the extent of the inconsistency with
the Constitution, shall be void.


Mwenyekiti wa baraza la mawaziri ni Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania.

Kumbe Karume ni waziri wa Tanzania Zanzibar?
 
Mwenyekiti wa baraza la mawaziri ni Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania.

Kumbe Karume ni waziri wa Tanzania Zanzibar?

Weee acha choko choko...

Rais wa Zanzibar ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri, kama ilivyo mwanasheria mkuu nadhani pia ni mjumbe.
 
Mwalimu Kichunguu,

Hawa jamaa (wengi wao) shule ndio hawajaenda. Kumbukumbu yao nayo ni ndogo.

Nailinganisha(kiutawala na akili) Zanzibar = Palestine. Tanzania bara = Israel.
 
mwakyembe yuko sahihi. kumbuka tena huyu ni mtaalamu ya constitutional law. someni kitabu chake.
 
Weee acha choko choko...

Rais wa Zanzibar ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri, kama ilivyo mwanasheria mkuu nadhani pia ni mjumbe.


Itifaki kwenye baraza la Mawaziri ni kama ifuatavyo:

  1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  2. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  3. Waziri Mkuu
  4. Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
  5. Mawaziri Wote
  6. Mwanasheria Mkuu

Kama tunavyofahamu, Waziri kiongozi anateuliwa na Rais wa Zanzibar, ambaye yuko chini ya waziri Mkuu kiitifaki; kwa hiyo ni makosa kikatiba kusema kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar yuko ngazi moja na Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Nionavyo ni kuwa jamaa hawa wana uchu wa madaraka nje ya yale waliyopewa kikatiba, na huyu mouthpiece yao Shamhuna asipojihadhari, anaweza kukutwa anakabiliwa na kesi ya uhaini dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!!!
 

Ule wa Mkapa na Wazanzibari ulikuwa ni MCHAKATO ndani ya CCM kumpata mgombea wao; kama ilivyokuwa kwa Karume na Dr. Bilali. Ninachokiongea mimi ni UCHAGUZI mkuu baada ya michakato hiyo.
 
Kuna kitu kimoja tumekosea waTanzania bara nacho ni hiki... kuna wakati tunaongea utumbo kwa kusema kwenye kamati mbali mbali za Muungano, kuwe na wajumbe sawa/EQUAL badala ya wanaowiana/PROPORTIONAL

Nijuavyo mimi neno Sawa limetumiwa vibaya na sasa linatuletea shida... neno hili Sawa limetumika kama kwa tafsiri ya EQUAL badala ya Tafsiri ya PROPORTIONAL na kwa bahati mbaya limeeleweka hivyo kwa waZanzibar kwa muda mrefu.

In other words... kila tunachofanya tunapotaka uwiano sawa... lazima kusiwe na representation ya 50:50 kwa kuwa Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara hazijawahi kuwa EQUAL/SAWA kwa vigezo vyovyote vile...
 
Tatizo la Watanganyika ni bullies, mnawalazimisha Wazanzibari wabaki kwenye ndoa ambayo wenzenu wameichoka.

Wakisema Zanzibar ni nchi, je inaongeza au kupunguza nini kwenye tija ya mwananchi wa kawaida? Sana sana ni feel good factor tu kwa Wazanzibari kujisikia nao wana nchi yao.

Kwa mfano hapa UK, mara nyingi tu Scotland wanajiona kama ni nchi, lakini sijawahi kusikia waziri akilalamika wao kusema si nchi. Katiba iko wazi na inaeleza wajibu wa kila serikali.

Huu mjadala wote mimi naona ni kupoteza muda tu kuongelea mambo ambayo hatuna uwezo wa kuyatatua zaidi ya kuwaachia majaji kuamua. Mjadala huu hauna tofauti na mijadala ya dini, mtu akiwa na imani yake hata siku moja huwezi kumbadili. Muhimu ni kila mtu kuishi kwa amani kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo.

Haya mambo ya nani mkubwa zaidi ya mwenzake hayana maana yoyote. Kama mmoja ni mkubwa, basi ukubwa wake uongozane na delivery ya services za maana kwa hao waliochini. Nini maana ya kuwa mkubwa huku kuwepo au kutokuwepo kwako hakuongeze tija yoyote?

Watu wanahangaika kwa umaskini na maradhi, nchi nzima inahangaikana kupandisha misuri ili kujua nani mkubwa kuliko mwenzake?

Sitashangaa tunakoenda ni kutwangana risasi shauri ya kutaka kuonyeshana nani mkubwa, baada ya hapo tunarudi hatua 20 nyuma kwa umaskini. Angalia yale ya Georgia.

Give me peace! I don't care Zanzibar ni nchi au sio nchi, Muhimu ni wananchi wetu kupata huduma muhimu na kuendelea kuishi kwa amani na utulivu kama binadamu wengine wa dunia hii. Kama wanaweza kuishi hivyo ndani ya muungano sawa, wakiamua kujitenga pia sawa. Hakuna sababu ya kutumia mtutu kulazimisha ndoa iliyochuja.
 

Haya ni maneno mazito mkuu!!! Fairplayer wewe ni mwanasheria?
 
mimi ninadhani,kwa wakati huu raisi ambaye ni Mzanzibari ndiye anayeweza kutatua haya matatizo ya muungano kwa urahisi zaidi, raisi kutoka bara ni vigumu sana kudeal na ishu ya muungano bila kuonekana ana ajenda ya siri dhidi ya zanzibar, kama CCM wanataka kurekebisha kasoro za muungano na kuwaridhisha wazanzibari(ambao ndo mara nyingi wananung'unikia muungano huu) hawana budi kumsimamisha mgombea kutoka zanzibar na kisha kumpa jukumu la kuhakikisha anatatua tatizo hili,
 
Hawa jamaa wanatangaza secession na Rais wa Muungano anabaki kucheka cheka tu!!

Bwana Mkuu vitu hivi vipo na vinafanyakazi na hao Maraisi wote waliopita hata huyo Muasisi wa Muungano wanavijua vipo na hawakuwahi kusema wala kuchukua hatuwa yoyote. Kama kwa mtazamo wako hili ni kosa basi elewa kuwa hapa pana ubabaishaji na sio Muungano as such. Hii ni Marriage of convinience na wakati sasa si muafaka kuendelea kama ilivyo. Karibuni nilisikia kwenye ITV kipindi cha LONGA MWANAMUME kuwa wanawake hawaolewi ndani ya ndowa bali Wanaowana na patners zao wa kiume. Nasi Muungano wetu uwe wa Kuowana na sio mmoja kumuowa mwengine. Kumlaumu Rais kwa uozo wa Muungano huu si halali na badala yake ni kumtaka ausafishe Muungano huu uwe kama wanavyotaka wenzetu wa kike. ni wa KUOWANA na sio mmoja kumuowa mwengine.
 

Si kweli kuwa Wazanzibari wamezoeya kutawaliwa na ndio maana walipindua kwa kumwaga damu tofauti na nyie mliobadilisha ukoloni kwa ukoloni mambo leo. Na kwa mantiki hiyo hiyo ya kukataa kutawaliwa ndio hizi harakati za kudai Muungano wa haki na sio kutawaliwa kama hivi sasa.
 

Bahati mbaya hujui mambo mengi ya Zanzibar na mara zote unakurupuka kwa habari za magazetini . Hao waandishi wa habari unaowataka wakupe jibu si tofauti na wewe kwani pengine hawajawahi kufika huko Zanzibar na hivyo kila pakifunuliwa ukweli inakuwa darasa jipya kwenu nyote. Ningewashauri mnaposikia neno linalohusu Zanzibar basi mgejongelea Wazanzibari wenyewe na kupata ufafanuzi. Haya mambo ya kusikia ndio yanayojenga nyie kuwa na mtazamo mbaya kwa Wazanzibari hata wakidai jambo la haki.
 
Ngekewa,

Usihitimishe mambo na kujumulisha issues. Hujui jamaa wanaulewa kiasi gani kuhusu Zanzibar.

Tuambie Pinda na Nahodha nani yupo juu ya mwingine?
Je zanzibar ina majeshi yake ya ulinzi?

Maswali madogo tu hayo.
 

Mheshimiwa Kichuguu nakuomba uweke mbali unazi wako na utafakari kilichozungumzwa.

Kimuundo Tanzania ina Serikali mbili ile ya Muungano ambayo itashughulikia masuala ya muungano na masuala ya jamhuri ya iliyokuwa Tanganyika na Serikali ya pili ni SMZ ambayo itashughulikia mambo ya Zanzibar.

Katika Serikali ya Muungano kutakuwa na Waziri Mkuu ambaye ataongoza mambo ya Muungano na yale ya Tanganyika. Huyu Bwana Bosi wake ni Rais wa Muungano ambaye ndie kiongozi wa Muungano. Kimakubaliano ni kuwa Rais wa Zanzibar atakuwa Kiongozi Mkubwa kwa Tanzania namba mbili akizidiwa na Rais pekee.
Rais wa Zanzibar atakuwa na mamlaka kamili juuu ya Zanzibar na Rais wa Muungano hatoweza kufanya kitu chochote kwa Zanzibar bila kumshauri huyu Rais wa Zanzibar. Rais wa Zanzibar ana Baraza lakw la Mawaziri na Serikali yenyewe ina Baraza lake la Kutunga Sheria ambalo Kiongozi wake ni Waziri Kiongozi. Sasa ukubwa wa Waziri Mku kwaZanzibar uko wapi?
Mkorogeko wa mambo upo kwa ile hatuwa ya kuunganisha vyama na wakati wa hatamu za chama mkorogo ulikuwa mkubwa na ndio maana mambo mengi ya kuimaliza Zanzibar yalifanywa kwa jina la CCM.
Wakati umeshabadilika na Wazanzibari wameamuwa kutaka muungano kama ulivyokubaliwa awali sasa tatizo nini wenzetu kututukana na kutuona maaduwi badala ya kufurahia kuwa tunataka Muungano utakaoondowa migogoro ya kila siku? KUWENI FAIR sisi ni nchi mbili tulioamuwa kuungana basi matakwa ya kila upande yatapatikana kwa mijadala na mashauriano.
 
Ngekewa,

Tunaomba ujibu kwa kufuata katiba na sio maoni yako binafsi.

Bado maswali yangu hapo juu hujayajibu kabisaaa. Na kama unaona umejibu basi sio sifuri ni chini ya hapo. Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Tanzania ni Tanganyika + Zanzibar) hicho ndio cheo cha Pinda Mizengo wa Kayanza.

Nasubiri majibu bado.
 

Nini maana ya mfumo wa ulinzi na umesahau jeshi la kujenga Taifa na hata amri ya Abbass Kandoro ya Mgambo. Ama kweli kama Wazanzibar wajinga basi kuna mliowazidi kwani unakurpuka kumwambia mwenzio yuko uchi kwa kuvaa msuli wewe umevaa chupi hadharani.
 

Mungu wangu. Mzee unaishi Tanzania au ulikimbia miaka ileeee?

Jeshila kujenga UCHUMI - JKU sio jeshi la kujenga taifa. Kaka/dada vipi? naona unaingilia mlango wa kutokea au unadandia basi liendalo kasi kwa mbele!

Jeshi la ulinzi na la kujenga taifa ni la muungano. Makamanda wote kule wanatii amri ya waziri wa ulinzi wa Tanzania (sio zanzibar) na amiri jeshi mkuu ni Rais wa Tanzania nzima.

Hilo nakusamehe ulikuwa hujui.

Jibu swali la Mizengo Pinda ni waziri mkuu wa wapi?
 

Lakini kisichofahamika hapa Wazanzibari si WANA HAKI ya kuamuwa wanachotaka basi na waachiwe waamuwe. Mtaendelea kuwaamulia mpaka lini?
Kwa akili yangu ndogo nahisi kutokana na wasifu mnaowapa Wazanzibari ni bora kuwaepuka na sio kuwangangania. Mmekuwa nao kwa miaka 44 mmeshindwa kuondowa ujinga wao, udini wao, uharamia wao, kutothamini fadhila mnazowapa, kuwalinda mnakowalinda na faida chungu mzima mnazowapa lakini bado wana msimamo mwengine BASI BORA KUWAACHIA WATOKOMEE.
Kuendelea kuwangangania huko mkiwatukana SI USTAARABU ambayo ni tabia yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…