Itifaki kwenye baraza la Mawaziri ni kama ifuatavyo:
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Waziri Mkuu
- Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
- Mawaziri Wote
- Mwanasheria Mkuu
Kama tunavyofahamu, Waziri kiongozi anateuliwa na Rais wa Zanzibar, ambaye yuko chini ya waziri Mkuu kiitifaki; kwa hiyo ni makosa kikatiba kusema kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar yuko ngazi moja na Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Nionavyo ni kuwa jamaa hawa wana uchu wa madaraka nje ya yale waliyopewa kikatiba, na huyu mouthpiece yao Shamhuna asipojihadhari, anaweza kukutwa anakabiliwa na kesi ya uhaini dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!!!
Mbona unajikanganya Mkuu, usemayo si yakweli kwani kwa hiyo itifaki unayosema angalia makaazi na ujaji waq viongozi pengine hiyo elimu yako imekupotosha. Aidha nakupa assignment moja- angalia namba za escort ya Waziri Mkuu utaona kuwa ina namba 4 na angalia ya Rais wa ZNZ utaona ni 3. Sasa unataka kundanganya nani kwa hicho kajielimu chako kisicho na mpango wowote na pengine ni wale Vihiyo.