Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Itifaki kwenye baraza la Mawaziri ni kama ifuatavyo:

  1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  2. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  3. Waziri Mkuu
  4. Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
  5. Mawaziri Wote
  6. Mwanasheria Mkuu

Kama tunavyofahamu, Waziri kiongozi anateuliwa na Rais wa Zanzibar, ambaye yuko chini ya waziri Mkuu kiitifaki; kwa hiyo ni makosa kikatiba kusema kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar yuko ngazi moja na Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Nionavyo ni kuwa jamaa hawa wana uchu wa madaraka nje ya yale waliyopewa kikatiba, na huyu mouthpiece yao Shamhuna asipojihadhari, anaweza kukutwa anakabiliwa na kesi ya uhaini dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!!!

Mbona unajikanganya Mkuu, usemayo si yakweli kwani kwa hiyo itifaki unayosema angalia makaazi na ujaji waq viongozi pengine hiyo elimu yako imekupotosha. Aidha nakupa assignment moja- angalia namba za escort ya Waziri Mkuu utaona kuwa ina namba 4 na angalia ya Rais wa ZNZ utaona ni 3. Sasa unataka kundanganya nani kwa hicho kajielimu chako kisicho na mpango wowote na pengine ni wale Vihiyo.
 
Nyinyi wananchi wa Visiwani, get this straight kwamba Zanzibari ni mkoa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama mnataka kuibadili hiyo inabidi mtumie sheria sio kupiga piga makelele kwenye migahawa na kashata, sisi huku forum hatuwezi kuwasaidia anything, kwa sababu hapa tuna mawe tu na fimbo hatuna peremende, wala tende, nendeni mkapigie kelele viongozi wa juu huko CCM.

Ahsanteni Sana.


And you na wenzio get it straight- kuwa nyinyi ni watu msio na Taifa . Tanganyika imekufa na haipo kwa mujibu wa Muundo wa Muungano wa Nyerere. Zanzibar (ipo kwa mujibu wa muundo huo) Hivyo ni haki yao Wazanzibari kulilia Zanzibar yao kwa mujibu wa Muundo wa Muungano wa Nyerere. Msiifanye Tanganyika kuwa ndio Tanzania. Hiyo haiwi asilani. Ama badilisheni muundo huo. Mpo. Ahsanteni sana.
 
Reverend na wenzio (wakiwemo Dr. Mwakiyembe na waheshimiwa wengine) na nyinyi mnaonyesha dhahiri kuwa hamuelewi Katiba ya Zanzibar. Hamuelewi Nini wajibu wa Baraza la Wawakilishi na majumbe wa Baraza la Wawakilishi, Hamuelewi nini wajibu na majukumu ya Rais wa Zanzibar na Baraza lake la Mawaziri kwa wananchi wa Zanzibar. Jifunzeni hayo kabla ya kushupalia kupayuka tu na kusisitiza misimamo yenu. Jamhuri ya Muunagno wa Tanzania ina madaraka yake nba mipaka yake, Na Zanz\ibar ina mipaka yake na madaraka yake. Sijui Tanganyika (Tanzania Bara) ambayo hamuelewi kama ipo ama imezimia.


Ni pale tu ninapokuwa ndani ya mipaka ya Tanzania ndio natakiwa kujua kuna Zanzibar, Kilimanjaro na Songea...

Nikiwa nje ya mipaka ya Tanzania inayolindwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) au Tanzania People's Defence Force (TPDF) ndio naitwa Mtanzania whether natoka Zanzibar (Unguja & Pemba) au Kilimanjaro, Songea.

Sio lazima kwa kila mtanzania kujua majukumu na sheria za serikali za Halimashauri ya Moshi, ya Jiji la Mwanza, Jiji la Dar es Salaam au Zanzibar, lakini ni Muhimu na huenda Lazima kufahamu majukumu na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni wakaazi tu wa Zanzibar, Dar es Salaam na Mwanza ndio wanatakiwa kujua makumu ya serikali zao (Local government), hizi serikali zaweza kuwa na viongozi wao na wao wakaitwa majina mbali mbali, Rais, Mwenyekiti, Meya etc... but at the end of the day wanakuwa na sheria ambazo hata siku moja hazipingani na za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Mkuu wa Medani! Shamhuna VP?!!!!!!!!! Was it planned by JK and his Team or?

Tunashukuru kusikia haya ila bado hilo halimnyimi nguvu ya kupiga kelele , mind u mtaalam ana machungu ya kutoswa NEC hivyo the only way ya yeye ku survive ktk siasa za Zenj ni kugusa area zote sensitive kila anapopata mwanya.

Tuipende nchi yetu kwa hoja za kujenga na si kutishana.

Ninajuavyo ni kwamba muungwana, aliombwa na Mkapa achague makamu wa rais, akapendekeza betweeen Meghji, Khatibu, na huyu Shamuhuna, Mkapa akagoma na kumuomba Mwinyi na Salimin waamue nani awe, wakamua Shein aendelee,

Muungwana akakata deal na Amani kumpa u-Deputy Waziri Kiongozi, sasa alipopewa tu, akaanza kampeni za urais wa huko visiwani, Muungwana akasikia, kwenye kikao cha cc akammwambia wazi kuwa nasikia kukupa ving'ora imekuwa taabu, naona nitavitoa hivi karibuni,

Hesabu za siasa huko sasa ziko wazi kuwa Bilali for now ndiye chaguo lake muungwana kumrithi Amani, sasa Shamuhuna anaamini kuwa anaweza kui-bully CCM kumpa yeye hiyo nafasi, hapo ndio kabisaa amepiga mwamba na sisi wananchi wa bara we could care less na hizi kelele zisizokuwa na any permannet political solution, kwa Deputy Waziri Kiongozi kupiga kelele kama mhuni wa mtaani it is beyond my belief,

Kama ana tatizo na muungano aende huko kwenye vikao atafute solution, lakini sio kupiga kelele zisizokuwa na uzito wowote kwa taifa zaidi tu kuanzisha matatizo kwa wananchi, wakati sheria ziko wazi on this ishu kuw rais wa Zanizbar ni mjumbe tu wa cabinet, sio a co-rais.
 
Kuna kitu kimoja tumekosea waTanzania bara nacho ni hiki... kuna wakati tunaongea utumbo kwa kusema kwenye kamati mbali mbali za Muungano, kuwe na wajumbe sawa/EQUAL badala ya wanaowiana/PROPORTIONAL

Nijuavyo mimi neno Sawa limetumiwa vibaya na sasa linatuletea shida... neno hili Sawa limetumika kama kwa tafsiri ya EQUAL badala ya Tafsiri ya PROPORTIONAL na kwa bahati mbaya limeeleweka hivyo kwa waZanzibar kwa muda mrefu.

In other words... kila tunachofanya tunapotaka uwiano sawa... lazima kusiwe na representation ya 50:50 kwa kuwa Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara hazijawahi kuwa EQUAL/SAWA kwa vigezo vyovyote vile...

Hayo yote yatakuja pale tutapokaa pamoja kama equal partners na kuamuwa na kukubaliana hicho mnachotaka lakini isiwe kama tulivyo sasa kuhodhiana.
 
And you na wenzio get it straight- kuwa nyinyi ni watu msio na Taifa . Tanganyika imekufa na haipo kwa mujibu wa Muundo wa Muungano wa Nyerere. Zanzibar (ipo kwa mujibu wa muundo huo) Hivyo ni haki yao Wazanzibari kulilia Zanzibar yao kwa mujibu wa Muundo wa Muungano wa Nyerere. Msiifanye Tanganyika kuwa ndio Tanzania. Hiyo haiwi asilani. Ama badilisheni muundo huo. Mpo. Ahsanteni sana.

Mkuu go take your cry kwenye the right place, sio hapa JF wa kubadilisha muundo ni nyinyi ambao kwenye kikako cha muungano rais wenu ni a mere cabinet member, sisi wananchi wa bara hatuna matatizo na muungano you know that better,

Kwenye hii ishu siku zote huwa mnaonyesha uwezo wenu mdogo wa ku-deal na matatizo ya kisiasa, kwa kukimbilia kulia kilio chenu kwenye the wrong places, wakati mnajua kabisa kuwa kama matatizo yote ya kisasa on muungano yanatakiwa kuepelekwa wapi, kama tatizo lenu ni kutafuta public opinion ya bara, ukweli mnaujua kuwa sisi wananchi wa bara we could care less na muungano's nonesense! tumechoka pia kama nyinyi nendeni NEC, kamat kuu ya CCM, na bungeni mkalitatue hilo tatizo,

Mambo ya kupiga kelele kwenye magazeti na media hayawezi kuwasiaidia kutatua tatizo lenu.
 
Hayo yote yatakuja pale tutapokaa pamoja kama equal partners na kuamuwa na kukubaliana hicho mnachotaka lakini isiwe kama tulivyo sasa kuhodhiana.

Ndugu we are not equal and we have never been equal, population of 35Millions against 1Millions... hata vitabu vya dini haviwezi sema hapa kuna equality.

This is a fact na ni fact ambayo wewe na viongozi wako hawaikubali.

Tunaweza kuongea kwa uwiano.

Zanzibar population ni ndogo kuliko Wilaya ya Kinondoni.

- Wilaya ya Kinondoni ina population ya 1.4M na Zanzibar ni 1.0
- Zanzibar kuna wabunge wa Jamhuri 52... wenye mashangingi na kila kitu
- Kinondoni ina wabunge watatu... Kinondoni, Ubungo na Kawe.
- Kinondoni hakuna waziri.
- Kinondoni hakuna Rais

Haya mambo yameifanya Zanzibar ibweteke.... imepewa hisani kubwa sana... mkuu...

Mwisho mchawi wa Zanzibar ni uchumi ambao unasababishwa na kutofanya kazi na kupendelea sana siasa... (over political representation); nguvu kazi kubwa iko kwenye siasa badala ya uzalishaji! kijiji changu kina population ya watu 10,000...ingekuwa Zanzibar tungekuwa na Mwakilishi, Mbunge, masheha kibao... mkuu wa wilaya... RPC etc... etc.

Mchawi wake sio serikali ya muungano hata kidogo...
 
Haya ni maneno mazito mkuu!!! Fairplayer wewe ni mwanasheria?

5) Without prejudice to the application of the Constitution
of Zanzibar in accordance with this Constitution concerning all
matters pertaining to Tanzania Zanzibar which are not Union
Matters

HAYO NDIO YALIYOTANGULIA NAWE UNAJARIBU KUYAACHA
 
Hayo yote yatakuja pale tutapokaa pamoja kama equal partners na kuamuwa na kukubaliana hicho mnachotaka lakini isiwe kama tulivyo sasa kuhodhiana.

Kuwa equal patners kwenye muungano ni tatizo la sheria, sio la siasa sasa dawa ni nyinyi kuwasisitiza viongozi wenu wa bara kubadili sheria, sio kutupigia kelele sisi wananchi wa bara, kwa sababu we could care less kuhusu status yenu kwenye muungano,

Halafu tunakuwaje political equal patners, wakati uchumi wenu ni almost hakuna kulinganisha na uchumi wetu bara? Hivi hamuoni UN jinsi mambo yalivyo wazi kwamba wenye uchumi mkubwa ndio wana sauti kubwa kwenye dunia?
 
Ngekewa,

Usihitimishe mambo na kujumulisha issues. Hujui jamaa wanaulewa kiasi gani kuhusu Zanzibar.

Tuambie Pinda na Nahodha nani yupo juu ya mwingine?
Je zanzibar ina majeshi yake ya ulinzi?

Maswali madogo tu hayo.

Of course wako sawa kwa issue za Serikali za Tanzania(Muungano na Zanzibar) .Asafar as Union Government Nahodha hana nafasi yoyote na Pinda kwa Serikali ya Zanzibar si chochote.

Whether you like it or not that is our MSETO (Muungano wa Tanzania)
 
Napenda kuwashirikisha katika sehemu hii ya sheria ya muungano

katika sheria ya muungano Na.45 ya mwaka 1965 ambayo ndio ilikuwa inaitwa Katiba ya muda, ibara ya 13 inasema...

'There shall be two vice presidents of the United Republic who shall be styled The First Vice President and The second Vice President respectivley;one of whom shall be the Principle Assistant of the President in the discharge of his executive functions in relation to Zanzibar and under the style of the President of Zanzibar, the head of the executive for Zanzibar. The other shall be the principle Assistant of the President in discharge of his executive functions in relation to Tanganyika and the leader of the government business in the National Assembly.
Hiyo bold haipo tena katika katiba na inaonesha nia ya mfumo wa muungano ilikuwa ni serikali moja ya muungano yenye nguvu iliyogawanywa tawi la utendaji kwa Tanganyika na Zanzibar. Hivi sasa tawi la utendaji ni 'fused' na ndio mjadala huu aliouleta Mwakyembe.

Nani anakumbuka mara ya mwisho Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano alifanya ziara katika mkoa wowote wa Zanzibar kama Waziri Mkuu kwa maana ya ziara ya kikazi kama anavyofanya Mbeya au Singida? Mimi sikumbuki. Kikatiba Waziri Mkuu ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, madaraka yake yapo bara na zanzibar. Ila kimatendo na mazoea madaraka yake yapo bara peke yake. The origin (uasili) wa muungano PM au mtu yeyote ambae anakuwa mkuu wa shughuli za serikali Bungeni (kumbukeni kuna kipindi miaka ya 70 nafasi hii ilifutwa kabisa) anakuwa na madaraka ya utebdaji ndani ya Tanzania bara.

Hivyo kiasili, kwa maoni yangu, Waziri Mkuu wa sasa nafasi yake ni ya utendaji kwa masuala ya bara na mbia wake sio Waziri Kiongozi bali ni Rais wa Zanzibar. Kiasili ya Muungano - Mkuu wa Utendaji kwa masuala yasiyo ya muungano kwa Zanzibar anaitwa Rais wa Zanzibar! Mkuu wa Utendaji kwa masuala yasio ya muungano kwa Tanzania bara anaitwa Waziri Mkuu!

My take ni kwamba, PM hana mamlaka juu ya mawaziri wa Zanzibar kama ilivyo kwa Rais wa Zanzibar asivyo na mamlaka kwa mawaziri wa Serikali ya Muungano kwa mambo yasiyo ya muungano kama kilimo nk. Ingekuwa Shamhuna amempinga Rais wa Jamhuri ya Muungano, hapo tungesema kakosea kwani Rais wa Muungano ana mamlaka na mambp yote ya Tanganyika na Zanzibar, yaliyo ya muungano na yasiyo ya muungano. Ikumbukwe kuwa Rais wa Muungano amekasimu, kikatiba, mamlaka ya utendaji wa Zanzibar kwa Mkuu wa utendaji kule anayeitwa Rais wa Zanzibar lakini bado ana mamlaka yote.Huu ndio muono wangu na mjadala uendelee
 
5) Without prejudice to the application of the Constitution
of Zanzibar in accordance with this Constitution concerning all
matters pertaining to Tanzania Zanzibar which are not Union
Matters

HAYO NDIO YALIYOTANGULIA NAWE UNAJARIBU KUYAACHA


5) Without prejudice to the application of the Constitution
of Zanzibar in accordance with this Constitution concerning all
matters pertaining to Tanzania Zanzibar which are not Union
Matters, this Constitution shall have the force of law in the whole
of the Republic, and in the event any other law conflicts with the
provisions contained in this Constitution, the Constitution shall
prevail and that other law, to the extent of the inconsistency with
the Constitution, shall be void.


Ngekewa,

Sitochoka kukupa shule, nilitaka kuachana na wewe ila nikaona nisikuache gizani AMI wangu.

Ukisha maliza kuruka ruka nasisitiza nijibu maswali yangu ambayo hata mtoto wa nursery school anaweza kuyajibu ila wewe unayakimbia.

Wasalaam
 
Mtatumia kila msamiati lakini mkae mkijua wenzenu mnaowalinda au kulindana wameshikwa pabaya ndio hivyo hapa JF hapawezi kuwasaidia kujiungisha kimabavu,tayari muungano ni pande mbili ,kama mnazungumzia ule Muungano wa pande moja uliokuwa ukipatikana Yemen na Germany na kwengineko hapa haupo.

Breaking In News.Muungwana kulihutubia Bunge Alhamisi ,sijui kama mnayo habari !! Just now nimetoka kwenye ofisi ya matayarisho ya vikao vinavyofanyika bungeni kupata yanayotayarishwa kwa wiki hii.
 
Ngekewa,

Tunaomba ujibu kwa kufuata katiba na sio maoni yako binafsi.

Bado maswali yangu hapo juu hujayajibu kabisaaa. Na kama unaona umejibu basi sio sifuri ni chini ya hapo. Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Tanzania ni Tanganyika + Zanzibar) hicho ndio cheo cha Pinda Mizengo wa Kayanza.

Nasubiri majibu bado.

WEWE ni mjuzi hebu naomba nieleze Waziri Mkuu atatoka wapi na atafanya kazi gani ? Tafadhali usinyofoe sehemu za Katiba na badala yake chukuwa Katiba nzima. Sasa nasubiri wewe muelewa ili nithibitishe mark ya100 unayostahiki.
 
Mtaendelea kulalamika kama WAPELESTINA nyinyi.

Kwanza muungano wenyewe mnafaidika nyie, mngekuwa na busara mngekataa kupewa uwakilishi kibao usio na sauti kwenye bunge. Kila mbunge ana watu 40,000(wastani) wakati bara kila mbunge ana waru sio chini ya 500,000.

ES na Kasheshe,

Tuwaagizie mtambo wa shira na tuahakikishe mwarabu akikonpwa hasilipwe; kisha tuwapelekee halua na tende kibao watanyamaza hawa watu!

LOL
 
Mungu wangu. Mzee unaishi Tanzania au ulikimbia miaka ileeee?

Jeshila kujenga UCHUMI - JKU sio jeshi la kujenga taifa. Kaka/dada vipi? naona unaingilia mlango wa kutokea au unadandia basi liendalo kasi kwa mbele!

Jeshi la ulinzi na la kujenga taifa ni la muungano. Makamanda wote kule wanatii amri ya waziri wa ulinzi wa Tanzania (sio zanzibar) na amiri jeshi mkuu ni Rais wa Tanzania nzima.

Hilo nakusamehe ulikuwa hujui.

Jibu swali la Mizengo Pinda ni waziri mkuu wa wapi?

1. walichosema Zanzibar ni mfumo wa ulinzi sio jeshi .
2. Pinda ni Waziri Mkuu wa Tanganyika na mambo ya Muunganosio Waziri Mkuu wa Zanzibar na hilo limeshathibitishwa na serikali ya Zanzibar yenyewe.
 
Kuna mchangiaji humu anajibu hoja ki-mdebwedo. When it comes to worse, the Constitution prevails. Not hearsay, not opinion. Ukisoma jinsi Jaji A Ramadhani na wenzake walivyochambua vifungu hadi kufikia maamuzi kwamba hakukuwa na uhaini Zanzibar, ndio mfumo huo huo utakaotumika kuamua nani mkubwa: Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zenj, au Waziri Mkuu..

Kama hoja ni kuvunja muungano... basi hoja na iwe kuvunja muungano. Tatizo, wanaotaka kuvunja muungano hawana ujasiri, wanatumia vi-hoja vyepesi vyepesi, typical Zanzibari. Muda wa kupiga Kiswahili umekwisha, ndiyo maana Waziri Pinda mpaka leo hajabadili kauli kwamba Zanzibar si nchi, that's how the books say.

My vote: Let Zanzibar Go, Its Been a Pain all Along. Tanganyika has enough problems to focus on, Umaskini, Mafisadi n.k

So far every one does not want to admit that worse. However clear and aunthentic thing does not want clarification as our leaders seek from other bodies. As far as MDEBWEDO that is our style of making you to realise that "the constitution says so" style will not yield agreememnt on the issue.
 
..tanganyika ikirudi hakutakuwa na zanzibar, kutakuwa na unguja na pemba.

..mtakuwa kama visiwa vya comoro. in fact zanzibar itabidi itawaliwe. kwasababu kutakuwa na civil war isiyoisha.
Hayo sidhani kama yanawahusu , maana badala ya kuongelea ndoa yako unaenda kuongelea ndoa za wengine ,sasa hii tuiite ni katika tabia za aina gani ? Halafu badala ya kujibu lililoulizwa unaenda kusema mie nikihama ujirani na nyumba nyengine utakufa sasa mbona umeelekeza huko tu kwa nini usiseme kama udugu utazidi ? Mkiambiwa roho zenu zimejaa maovu mnapiga makelele.
Kwa upande wangu Muungano ambao umeshakatika umebakia maneno ya vipi utaungwa ungwa ,utaisaidia tanganyika kuendeleza raia zake kwa nguvu mpya ,Na Zanzibar nako watajipigapiga wajikwamue katika uchumi uliodumazwa na mwisho kutatokea ushindani kati ya viongozi na raia katika kujenga nchi yao ,maendeleo yaliokuwa ni ahadi hewa yataonekana yakifanyika kwa jicho yakinifu ,kila upande upande utalinda maendeleo yake yawe yenye kupiga hatua kuliko ilivyokuwa kabla ya Muungano kuekwa pembeni na hivyo raia watashuhudia maneno aliyoyasema Muungwana Maisha bora kwa kila raia wa Tanganyika na Zanzibar ,kwa kweli naona maendeleo tu na wala sio mgawanyiko kama mnavyotarajia machogo wengi,maana ule ufisadi mnaona dunia nzima ni mafisadi kama viongozi wenu.
 
Sekenke,

Ni vizuri ukamtaja tu kama ni Mwiba au huyu Ngekewa. Kwa kweli wanachoandika ni purely kutoka kichwani mwao na si katika maandiko ya katiba na uamuzi wa mahakama.

Ukiwauliza maswali madogo kama Pinda ni waziri mkuu wa wapi, Hawana majibu.

Ngoja nijadiliane na wengine, ndio maana nimesema kuwa hii ni kama Palestine na Israel.

Tatizo lako roho yako ina pepo wa ubaya . Ivo wewe unajiringia kuwa Muisrael nafikiri Watanganyika ni watu wasiopenda dhuluma. Pengine wewe ni exceptional.
 
mwakyembe yuko sahihi. kumbuka tena huyu ni mtaalamu ya constitutional law. someni kitabu chake.
Sijui ulimfahamu vipi yule Nndengereko aliesema wamesoma lakini....!
Sasa kama ni mtaalamu mbona amevuruga na sio kuvuruga bali amevurunda ,amesema uchovu na amepinga kauli ya spika ,hilo tu limeshamkosesha adabu kama hajui kukosa adabu ,hawa ndio wale watu wanaojifanya mafundi wakaingilia kati na kutaka kutengeza kumbe ndio wanazidi kuharibu ,ukimuuliza mbona gari yangu sasa inatoa sauti ya mnyororo atakwambia ndivyo ilivyokuwa tokea mwanzo.
 
Back
Top Bottom