Ninyi watu... record unataka upewe film na ITV/TVZ/Chanel 10? Are you saying kuna mabadiliko ya katiba hayakwenda Dodoma na kupitishwa na bunge? Ama kweli... ninyi mnapenda chokochoko.

Achani choko choko... fanyeni kazi... tatizo la Zanzibar ni uchumi... sio kuitwa nchi huru!!!

Je baada ya Zanzibar kuwa nchi huru what will hapen... zaidi ya kuwa na matumizi zaidi ya kuwa na jeshi lenu zaidi, kufungua balozi nyingi etc.... kwa ajili ya kujilinda... na wengi zaidi... Kenya... Tangampya.. etc. etc....


Fanyeni kazi... achaeni politics
 

Well, if that's the case, then this whole Katiba thing is totally messed-up! So ninachokiona hapa ni hiki: Mwl na Karume hawakuweka mambo mengi (yanayohusu Muungano) bayana. Perhaps walikuwa too excited kipindi walipokuwa wanafunga hii ndoa ("Oh, tunaungana..., Sasa Afrika yote itafuata..."). Therefore, hawakuchukua muda wa kufikiria kwa undani (wala kutazama mbali) na kutambua confusion zitakazojitokeza baada ya wao kuwa wameanza. Na kwakuwa wote walishaanza na hatuna wa kumuuliza, "mlikusidia nini hapa?/hapa mlikuwa mnamaanisha nini?" My advice ni kwamba: Katiba iliyopo inahitaji marekebisho ya haraka sana. Otherwise, hizi kelele za akina Shamhuna (and those other guys/wapemba) zitaendelea leo, kesho, [na penginepo] mpaka Isa bin Maryam arudi.

And/or,

Muungano utakufa kifo cha mende (which, frankly, I don't give a damn!).
 

Hapa ndio maana naona hio sera ya serikali tatu hamuielewi! Kama Rais wa Zanzibar atakuwa Makamu wa kwanza wa Rais, huyo Rais wa Tanganyika atakuwa nani? Ikumbukwe kila sehemu itakuwa na serikali yake na rais wake kwa hiyo msitegemee hata siku moja huyo wa Tanganyika ataangalia kwanza maslahi ya Tanzania! Hapana, yeye priority yake itakuwa masuala ya Tanganyika kama vile huyo wa Zanzibar atakavyokuwa. Na kwa vile hawa nchi huru watamiliki hazina zao, majeshi yao n.k. huyo Rais wa muungano atabaki na nini?
 

Hili la Nkrumah nakuunga mkono. huyu mtu ukisoma historia yake kwa makini alikuwa katili sana na dikteta
 
Sorry lakini unaonekana kama mfanyakazi mkongwe serikalini, maamuzi ya tuunde tume, tuwarudishie wananchi, yaani unatoa general statement isiyotoa suluhu.

Samahani ni mtazamo tu naweza kukosea.

Nakubaliana na wewe, ila kuwa mkongwe au kijana inategemea na mawazo yako yanatafriwa vipi na msomaji. Kama anayetafsiri ni mkongwe basi ataona mawazo yako ni ya kikongwe kama yake, na kama ni kijana basi ataona mawazo yako pia ni ya ujana kama yake

FairPlayer;

Kama unakumbuka Katika muafaka wa CUF na CCM wao walipendekeza kuwa agenda irudi kwa wananchi kwani maamuzi yale ya kuishirikisha CUF kwenye serikali yalikuwa ni makubwa, Hivyo basi na hili la muungano kwa sababu ni kubwa zaidi tufuate mkondo ule ule uliopendekezwa na watawala wetu ili kutoa Democracy zaidi kama wao walivyoona. Nafikiri hapo itakuwa FairPlay
 

Lakini kweli maneno yako- yana mfupa.
 

Waziri mkuu ameongea kuhusu hili katika kikao kinachotakiwa, Mwakyembe ameliongelea hili kwenye kikao kinachotakiwa, lakini look Shamuhuna ameliongelea wapi? Sasa what that tells you kuhusu viongozi wetu huko?

A Deputy Waziri Kiongozi, anapoweza kwenda kuongelea a very serious ishu kama hii mitaaani badala ya kwenye proper vikao maana yake ni nini? Maana yake ni moja tu ni incompetence, hana uwezo wa kuwa kwenye hiyo nafasi ila alipewa tu kwa sababu ya political favors ambazo ndio hasa zimelifikisha taifa letu lilipo sasa,

Kiongozi serious anakwenda kwenye vikao serious vya taifa ndiko anakokwenda kulalamikia sheria, sio kulalamikia viongozi kwa sababu hilo haliwezi kutatua tatizo la kisheria ambalo ndio hasa kiini cha tatizo la muungano, kwenda public kulia lia maana yake ni moja tu kuwa kuna kiongozi anajaribu kutingisha kibiriti,

sasa tunawahakikishia viongozi wote wa namana hiyo kuwa sisi wananchi hatupendelei this nonesense na mtu yoyote atakayekuja hapa na the same nonesense mentality kama ya Shamuhuna hapa JF tuta-respond the same way, lakini anayetaka a decent debate pia anakaribishwa, ila msituletee siasa za mitaaani ambazo mnaonekana kuzijua sana ambazo ndio zimewafikisha mlipo na CUF,

Shamuhuna anatakiwa kuchukuliwa hatua kali kwa kuchochea wananchi, badala ya kwenda kusema kwenye vikao vinavyotambulika kisheria kama walivyofanya Pinda, na Mwakyembe.

Ahsante Mkuu.
 
Katika mjadala huu,
wengi wetu tunawasakama Pinda, Mwakyembe na Shamhuna bila kuangalia kama je wanatoa mawazo yao tu au wanaenegemea kwenye katiba. Kwa PM kusema Znz si nchi, alinukuu katiba, ambayo wengi wameapa kuilinda na kuitetea. WEngi wetu tunawajadili hawa watu badala ya tatizo.

Vyombo vya habari ndo kabisaaa, utadhani wanakatazwa kufanya analysis ya katiba kuhusu tatizo lililopo. Wao wanafaya reporting tu, ambayo hata kasuku angeweza kuifanya. Media inafuell balaa kwenye tatizo hili, na itabaki kujuta tu muda wa kujuta utakapowadia.
 

Shamuhuna anatakiwa kuchukuliwa hatua kali kwa kuchochea wananchi, badala ya kwenda kusema kwenye vikao vinavyotambulika kisheria kama walivyofanya Pinda, na Mwakyembe.

Lakini Shamhuna amezungumza aliyozungumza katika kikao cha Baraza la Wawakilishi. Hivi wewe hutambui kuwa kikao hicho ni kikao kinachotambulika hasa katika masuala yenye maslahi na Wazanzibari. Tukuelewe vipi?
 
Lakini Shamhuna amezungumza aliyozungumza katika kikao cha Baraza la Wawakilishi. Hivi wewe hutambui kuwa kikao hicho ni kikao kinachotambulika hasa katika masuala yenye maslahi na Wazanzibari. Tukuelewe vipi?

Kikao cha baraza la wawakilishi kunachojumuisha kina nani mkuu as far as Muungano is concerned?

Wakati Pinda anayasema kwenye bunge la Jamhuri, Shamuhuna hakuwepo? Kama alikuwepo alisema nini?
 
Kikao cha baraza la wawakilishi kunachojumuisha kina nani mkuu as far as Muungano is concerned?

Wakati Pinda anayasema kwenye bunge la Jamhuri, Shamuhuna hakuwepo? Kama alikuwepo alisema nini?
Sawa Mkuu. Shamhuna alipozungumza (achilia mbali lugha yake kuwa na munkar na jazba), alinukuu katiba ya Zanzibar ambayo hiyo hupitishwa na Baraza la Wawakilishi, Kikaoni ambapo ameongelea jambo linalohusu maslahim ya Zanzibar na Wazanzibari -kuna kosa gani hapo?
 

Wakati Pinda anayasema kwenye bunge la Jamhuri, Shamuhuna hakuwepo? Kama alikuwepo alisema nini?

Sasa unaona. Turudi kwenye sheria kule kule unakokazania wewe. Hivyo ni vyombo viwili tofauti vyote vinatambuliwa na sheria za Tanzania -Bunge na Baraza la Wawakilishi. Wakati Mh. Pinda akilizungumzia hilo Bungeni Shamhuna hakuwepo huko, hana ubavu wa kuweko huko kwani si Mbunge wala hayumo katika Baraza la Mawaziri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini yumo katika Baraza la Mawaziri la SMZ, na katika Baraza la Wawakilishi, vyombo vyengine ambavyo kisheria vipo kushughulikia maslahi ya Zanzibar , watu wake na mali zake. Jee hakuwa na haki ya kuongelea jambo hilo katika Kikao halali cha Baraza la Wawakilishi?
 



Kitila ,

Mbona unazungumza kama wabara ndio wanaowalazimisha wazanzibari kuwa kwenye huu muungano ? Kwa mtazamo wangu naona ya kuwa pande zote mbili zinanufaika kutoka kwenye huu muungano . Mtu anayefikiri kutakuwa na kitu kinachoitwa ZANZIBAR nje ya muungano ni kichaa ! Once huu muungano ukifa basi kutakuwa na kitu kinachoitwa Pemba na Unguja na sio Zanzibar .

Mimi nadhani hii debate ni nzuri kwa afya ya huu muungano .Lazima tuache hii tabia ya kuogopa kuzungumzia huu muungano manake imekuwa kama taboo. Binafsi namlaumus sana Nyerere kwani akuruhusu watu kuzungumzia huu muungano.
 

Hivi Mwiba wewe ni Mtanzania? mwenye uchungu na nchi hii? upo bongo hapa? mbona unaturudisha nyuma sana? Think for yourself na ufuatilie hotuba za Mwakyembe utaona. Argument yako hapa inaonyesha uwezo wako wa kufikiri na kunyambulisha mambo ni mdogo sana au hakuna. huwezi kuungwa mkono kwa hizi hoja zako
 

Mwakyembe na Pinda, wameyasema kwenye kikao cha pande zote mbili, bunge la jamhuri linahudhuriwa kisheria na wabunge wa Zanzibar na Bara,

lakini kikao cha wawakilishi hakihudhuriwi kisheria na wabunge wa bara, kwa hiyo mahali muafaka kisheria na kisiasa pa kuhoji maswala ya muungano ni kwenye bunge la pamoja, yaani la Jamhuri ambako ndiko Pinda na Mwakyembe, walipotoa hoja zao, sasa kipi ni kigumu kuelewa hapa?
 
Date::8/18/2008 Wanasheria wapigilia msumari kuwa Zanzibar si nchi Kizitto Noya na Happiness Matanji
WATAALAM wa Sheria wamesema mgogoro wa hadhi ya Zanzibar kuwa nchi hauwezi kutatuliwa kwa kutumia sheria bali busara ya ama kufuta Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) au kuanzisha serikali ya Tanganyika.

Wakizungumzakwa nyakati tofauti jana, wanasheria hao walisema sheria haiwezi kutumika kumaliza mgogoro huo kwa sababu imeshafikia kikomo chake cha maamuzi.

Wakili maarufu wa kujitegemea, Twaha Taslima, alisema sheria ina ukomo katika kushughulikia mambo hasa baada ya Mahakama ambayo ndiyo ya mwisho katika kutoa maamuzi, kupitisha hukumu.

Alisema kuhusu Zanzibar, mahakama ilishatoa hukumu kwamba Zanzibar sio nchi na kuwaachia huru watuhumiwa wa kesi za uhani katika miaka ya hivi karibuni na Katiba pia imeweka bayana kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano.

Akinukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema Ibara ya Kwanza imetamka bayana kwamba Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano hivyo sheria ya maandishi haina jibu lingine.

Taslima alisema maelezo hayo na kitendo cha Mahakama Mahakama Kuu kuwaachia huru watuhumiwa wa uhani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), ndio mwisho wa tafsiri za kisheria kuhusu suala la Zanzibar na kwamba kilichobaki sasa ni busara ya kawaida kutumika.

Hata hivyo alisema sheria imechangia kuleta utata wa suala hilo kwani ukisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ibara ya nne vifungu vya kwanza hadi tatu utapata picha kwamba, kiutekelezaji Zanzibar ni nchi na kiutendaji sio nchi.

“Ibara ya Nne, kifungu cha kwanza hadi cha tatu vinasema: 'Kwa ajili ya utekelezaji bora na mgawanyo wa mamlaka, kutakuwa na mambo ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano',” alisema na kuongeza:

''Shughuli zote za Mamlaka zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo vyenye mamlaka ya utekelezaji (SMZ na Serikali ya Muungano) na mamlaka ya kutoa haki itakuwa ya vyombo viwili vya kutoa haki (Mahakama ya Zanzibar na Muungano)''.

Kuhusu mjadala wa ama Mbunge wa Kyela Harrison Mwakyembe alikosea kuwataka mawaziri wa Zanzibar waadhibiwe kwa kupingana na Waziri Mkuu kuhusu hadhi ya Zanzibar, Taslima alisema alikuwa sahihi ingawa pia haikuwa busara kwake kutoa tamko hilo hadharani.

''Mwakyembe angepeleka suala hilo kwenye vikao vya chama ili wakajadili, lakini pia hakukosea kusema mawaziri hao waadhibiwe kwani kimsingi dola ya Muungano ndio yenye nguvu kuliko SMZ na yeye alikuwa anazungumzia masuala ya Muungano,'' alisema

Kauli ya Taslima iliungwa mkono na mtaalam wa mambo ya katiba na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Sengondo Mvungi, aliyesema kuwa sasa inatakiwa busara itumike kuhusu hoja ya hadhi ya Zanziba.

''Mbona tunasema hamwaelewi, mnataka sheria isemeje?” alihoji Dk Mvungi na kuendelea: ''Katiba inasema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi moja yenye Mamlaka, ukilijua hilo swali kwamba Zanzibar ni nchi au sio halizuka tena, vinginevyo hawa wanaoendeleza mjadala huo watwambie wana maana gani,'' alisema.

Kuhusu suala la Mwakyembe alisema kwa sababu dola ya Jamhuri ya Muungano ndio yenye nguvu, mawaziri wa Zanzibar wanapaswa kumheshimu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ingawa anayeweza kuwaadhibu ni Rais wa Zanzibar.

''Mwakyembe yuko sahihi kwamba mawaziri wa Zanzibar wanatakiwa kumheshimu Waziri Mkuu na ikumbukwe kuwa Pinda alizungumzia suala la Muungano hivyo wadhifa wake bado ni mkubwa na usiopaswa kupingwa hadharani na watendaji wa serikali,'' alisema Mvungi.




Source: Mwananchi
 


Kumbe hata sheria ya taifa letu huijui, kwamba huwezi kuwa waziri katika serikali ya bara wla visiwani, bila kuwa mbunge either wa kuchaguliwa na wananchi au rais, either wa bara au visiwani?

Shamuhuna ni mbunge, ndio maana akawa waziri, kwa hiyo mahali muafakapa ye kutoa kero zake on mungano ni kwenye bunge la jamhuri ambako ana haki kisheria ya kuingia kama mbunge an waziri na hasa Deputy Waziri Kiongozi,

Kwenda kuongelea kero zake za muungano, kwenye Baraza la Wa Wakilishi ambako wabunge wa bara hawako mandated kuhudhuria kisheria ni tabia mufilisi ambayo ndio hasa tunayoikataa hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…