Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Fundi mchundo naona unashindwa kuelewa kwamba tunaong'ang'ania muungano ni sisi watu wa bara.

Hivi unasoma hata magazeti? Ni mara nyingi viongozi wa visiwani walisema wamechoka na muungano.
Sisi watangayika tukisikia hayo tunaanza kuwashitaki nakusema wanavunja sheria.

Waziri kiongozi wa Zanzibar akiitetea Zanzibar yake basi ni kama Pinda bara.

Wazanzibari wengi hawautaki muungano bali sisi wa bara tumewang'ang'ania kwa kuogopa kwamba watatupita kimaendeleo na wananchi wengi watauliza kwanini Zanzibar iweze sisi tushindwe.

Unawajua mafisadi wangapi kutoka visiwani?

Kwenye bajeti gani wawe mafisadi? Mafisadi wa Zanziba ni hao wafanyabiashara uchwara (wakina Raza n.k.) wanaoshirikiana na wanasiasa.

Ni imani potofu kusema kuwa ni watanganyika wanaowang'ang'ania wazanzibar. Ni viongozi wachache ambao katika kumuenzi baba wa taifa wanaona muungano kuwa ni sacrosant. Ukweli ni kuwa watanganyika wengi wala hawana habari na kinachoendelea Zanzibar. Kuwepo kwake na kutokuwepo kwake hakumsaidii chochote. Tofauti ni kuwa Zanzibar wanapiga kelele wakati wenzao wako kimya. Kuwa kimya kwao si kuwa wanaafiki hali ilivyo. Mara chache wanatokeza watu kama Mchungaji Mtikila wanaotamka bayana kuwa hawana mpango na Muungano.. Lakini unaamini kweli kama itafanyika referendum pande zote mbili, watanganyika watautaka Muungano? Unadhani hizi habari za madeni ya Tanesco, vurugu za unguja na pemba n.k. haziwagusi?

Tatizo ni kuwa kwa kukaa kimya kwao, wenzetu wanachukua fursa kutafuta umaarufu usio na maana kwa kututia vidole machoni! Ukoloni gani wakati wamepewa upendeleo katika Bunge la Muungano? Hivi kama kweli hiyo idadi ya majimbo huko Zanzibar inaendana na hali ilivyo? Chama kilichoshinda Pemba leo ndio kinakuwa Chama kikuu cha upinzani! Uwaziri hata katika wizara ambazo si za Muungano wanapewa wazanzibari bila mtu kulalamika. Watanganyika wanazuiwa kupiga kura Zanzibar wakati wazanzibari ruksa kupiga kura na kukaa kokote katika Tanganyika bila kubughudhiwa na mtu! Wanadai kudhalilishwa kwa Rais wao kwa kutokuwa makamu wa Raisbila kuangalia kuwa kuna Makamu wa Rais (ambaye atamrithi Rais kama jambo lolote likimpata) kutoka Zanzibar! Hawataki kusema kuwa ikiwa Rais wa Zanzibar atakuwa Makamu wa Rais, basi itabidi agharamiwe na serikali ya Muungano! Walidai Mamlaka kwenye bandari zao , wakapewa. wameshindwa kuziendeleza lakini leo wanadai wapewe mgao kwenye Bandari za Tanganyika!

Mchezo wanaofanya viongozi wa Zanzibar ni mbaya. Wao wanaaminim kuwa hata iwaje watanganyika hawawezi kuutema Muungano. Lakini wanasahau uvumilivu una kikomo chake. Na sio wote watakaokuja watakuwa na sentiments za viongozi wa sasa.

Hakuna kiongozi wa Zanzibar anayetamka wazi kuwa muungano uvunjwe. Wanachodai ni marekebisho ambayo yataupelekea kufa. Sasa kwa nini watupatishe taabu kote huko? Waseme tuu, kuwa Muungano hatuhutaki, tuanze mazungumzo ya kugawana mali. Lakini, chonde chonde, yasiwakute yaliowakuta viongozi wa Quebec. Referendum ilipofanywa, na wananchi kufahamu kuwa si masihara tena, canada ndio hio, wakawatosa. Tumeoleana, tumezoeana, msitake kutuharibia!
 
Wajumbe Zanzibar wataka Wabara watumie pasipoti

Na Ali Suleiman

BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamepinga sera ya vitambulisho vya Mzanzibari mkazi na kusema suala hilo linafanywa zaidi kisiasa na kutaka kurudishwa kwa hati ya kusafiri kati ya Tanzania Bara na Zanzibar ambayo iliondoshwa mwaka 1995.

Hayo yalisemwa jana na Waziri Kivuli Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bw. Abdalla Juma, wakati akisoma maoni ya kambi ya upinzani katika suala la sera ya vitambulisho vya Mzanzibari mkazi.

Alisema haiwezekani Wazanzibari kuitwa wakazi katika nchi yao na kuongeza kwamba vitambulisho hivyo havifai.

"Vitambulisho hivi kwa kweli havifai, sera hii haifai isipitishwe, kwa sababu inaonekana wazi kuwadhalilisha Wazanzibari katika nchi yao," alisema Bw. Abdalla.

Wajumbe wengine wa Baraza walitaka kurudishwa kwa utaratibu wa zamani wa kuwapo hati za usafiri wakati wa kuingia katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Mwakilishi wa Magomeni, Bw. Salmin Awadh, alitaka kurudishwa kwa hati za usafiri na kusema kuondoshwa kwake kwa kiasi kikubwa kumesababisha kasi ya ujambazi na uhalifu.

"Tunataka kurudishwa kwa hati za usafiri kati ya Zanzibar na Tanzania Bara...tunataka kuwepo kwa udhibiti katika eneo la bandari pamoja na uwanja wa ndege'alisema Awadh.

awadh alisema sera ya vitambulisho vya uzanzibari ukazi lengo lake ni ulinzi kwa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba na kuweza kuwatambuwa hasa Wazanzibari na wageni.

mwakilishi wa viti maalumu kutoka katika chama cha wananchi CUF Zakia Omar naye alitaka kurudishwa kwa utaratibu huo ambao alisema ulisaidia sana kudhibiti vitendo vya uhalifu.

alisema kuondoshwa kwa hati za kusafiria kati ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa kiasi kikubwa kumerudisha wimbi la vitendo vya uhalifu.

hati ya kusafiri kati ya Tazania Bara na Zanzibar pasipoti iliondolewa katika miaka ya 1995,baada ya kubainika kuwepo kwa vikwazo vya usafiri katika nchi moja ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuonekana kwenda kinyume na katiba.

source: majira
 
Hayo ni marudio tu,hamna jipya kuhusu hilo swala la pasi za kusafiria.
A small picture in that big picture ni swala la MUUNGANO.
Shime lipatiwe ufumbuzi kabla shati jeupe harijaingia DOA
 
Tatizo kubwa la hawa wazanzibara ni ubaguzi tu!
wamekuwa wakibaguana sana kwa misingi ya upemba na uunguja mara uCUF na uCCM. Wameona hiyo haitoshi sasa wanataka sisi twende kwao kwa passport???!!!mbona hawasemi na wao waje kwetu kwa passport???wao wanapenda vya bure tu, kweli hawa mdebwedo wameishiwa sasa wanalazimisha mambo.
 
Hivi hawa jamaa mnawabembelezea nini? wenyewe ndio wamejazana huku Bara wanaongeza tu hewa chafu jijini.
Inatakiwa wenyewe ndio waje kwa passport kwanza wanawabania watu wa bara, shughuli za kawaida kama kuendesha maduka ambazo zingewezwa kufanywa na wazawa wa bara wenyewe ndio wanakuja kuzidominate huku, wanakuwa kama wachina wanaokuja kuuza ice cream na mapambo. Enough is enough bwana
 
Ndugu zangu ya nini kutumia passport wakati bara na visiwani ni nchi moja? Mambo haya yanaendeleza mpasuko baina ya sehemu hizi mbili, tukiendekeza swala hili mwisho watadai passport za bara na visiwani ziwe tofauti....au watataka tuweke 'trade barriers' kama vile ni nchi mbili tofauti. Kuna mambo mengine hayana maana na yanaleta tu 'confusion'.
 
Mimi nimechoshwa na hizi chokochoko za wazanzibari kuhusiana na muungano.Sifahamu nini tunachoendelea kuung'ang'ania,sioni sababu ya kuridhisha ya kuendelea kuwa nao kama wao ''wazanzibari'' hawataki.

Ipo haja ya kufanya kura za maoni kwa nchi nzima kuona kama tunahitaji kuwa na huu muungano au la.

Na kama hatuihitaji kuwa na muungano,nini hatima ya wapemba na wazanzibari wengine wanaomiliki ardhi,nyumba na biashara huku bara (Tanganyika)?

Yangu macho na masikio!
 
Hakuna kiongozi wa Zanzibar anayetamka wazi kuwa muungano uvunjwe. Wanachodai ni marekebisho ambayo yataupelekea kufa. Sasa kwa nini watupatishe taabu kote huko? Waseme tuu, kuwa Muungano hatuhutaki, tuanze mazungumzo ya kugawana mali. Lakini, chonde chonde, yasiwakute yaliowakuta viongozi wa Quebec. Referendum ilipofanywa, na wananchi kufahamu kuwa si masihara tena, canada ndio hio, wakawatosa. Tumeoleana, tumezoeana, msitake kutuharibia!
Shabash u sound very good. Ukweli ni kuwa mfumo wa huu Muungano ndio unaohitaji marekebisho. Lazima Tanganyika na vyombo vyake vitolewe katika Vyombo vya Muungano na vitengwe kama vile Zanzibar na vyombo vyake vilivyotengwa. Au vyombo vyote vya Zanzibar lazima viwe "intergrated " katika Vyombo vya Muungano kama vile vyombo vya Tanganyika vilivyokuwa "intergrated". Kinyume cha hayo uliopo sasa ni usanii. Serikali ya Tanganyika haiwezi kuwa ndiyo hiyo hiyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. It is just as simple as that. Kama wa-tanganyika wa kawaida hata hawana habari na kinachoendelewa Zanzibar- Wazanzibari wa kawaida wana habari tosha na kubinywa na Serikali ya Muungano katika kupata maslahi yao. It is just as simple as that.
 
Well said Kinyamana! Hata mimi binafsi nimechoshwa na swala la Muungano, nakuunga mkono ya kwamba kura za maono zifanyike na nina uhakika kwamba watanzania wengi wata 'vote-against' muungano huu kwani umeshakuwa kero. Wapemba na wazanzibari wanaemiliki mali Tanganyika wawedeclared as 'foreigners' na wafuate taratibu zilizowekwa na immigration juu ya foreign settlement in this country. Sidhani kama Zanzibar itaweza kujimudu bila ya support ya Bara.
 
Mh...kazi ipo!
 
Nani kakwambia ZNZ haiwezi kusimama kwa miguu yake hadi Bara iwasaidie...!!!

Hao unaowaona wafanya biashara they have nothing to lose...Wahindi wangapi leo wapo UK au Dubai na wala si kwao...watafuata tu taratibu...

Kama wanzibar wanataka watu watumie passport kwenda znz, goo, the same wao wakija DSM lazima watumie passport!!!(Sijui kama hili lawezekana kwa sasa on both sides)..

Nionavyo Muungano bado unahitajika, tatizo baadhi ya mambo lazima yawekwe sawa...mambo ya kura za Maoni...hazina Mpango, ni ucheleweshwaji tu wa mambo...
 
Nyerere alisema kweli katika moja ya hotuba zake kwamba shida ya muungano inaanzishwa na viongozi walafi wa madaraka huko visiwani.
Lakini siku tukisema basi kuanzia leo Unguja na Pemba kwendeni kwenu, baada ya siku si nyingi tutasikia wapemba wakiwaambia waunguja kwamba nanyi si wazanzibari.
Poleni wazanzibara kwa kukutana na karaha hii.
 
Tatizo kubwa la hawa wazanzibara ni ubaguzi tu!
wamekuwa wakibaguana sana kwa misingi ya upemba na uunguja mara uCUF na uCCM. Wameona hiyo haitoshi sasa wanataka sisi twende kwao kwa passport???!!!mbona hawasemi na wao waje kwetu kwa passport???wao wanapenda vya bure tu, kweli hawa mdebwedo wameishiwa sasa wanalazimisha mambo.

Wacha kuchanganya mambo. Huo unaouona wewe ubaguzi si ubaguzi bali ni jitihada ya Wazanzibari kujilinda. Matukio yanayotajwa kutokana na kuondoshwa kwa utaratibu wa pasi ni ya kweli. Kama upo utaratibu wa kuzuiya hayo basi changia ili kutatuwa tatizo. Ama hilo la kubaguwana jiulize kuhusu matukio yaliyotokea Tarime pengine utajuwa chanzo .
 
Nyerere alisema kweli katika moja ya hotuba zake kwamba shida ya muungano inaanzishwa na viongozi walafi wa madaraka huko visiwani.
Lakini siku tukisema basi kuanzia leo Unguja na Pemba kwendeni kwenu, baada ya siku si nyingi tutasikia wapemba wakiwaambia waunguja kwamba nanyi si wazanzibari.
Poleni wazanzibara kwa kukutana na karaha hii.

Sijaelewa Karaha gani mojawapo. Ile ya kulazimishwa kukubali kila kitu au ile ya shida ya Muungano kusababishwa na viongozi walafi wa Visiwani? Ikiwa hii ya pili si kweli kwani hao viongozi wanaojipendekeza kwa Muungano ndio walafi wakitegemea kunufaika na hongo za Bara ili kuzidi kuikandamiza Zanzibar.
Kwa nini mnashindwa kuelewa kuwa Wazanzibari wanataka uhuru wa kujiendeleza na iwapo huo Muungano utabadilika na kuwa na mwelekeo huo basi hakutokuwa na tatizo.
 
Mwakilishi wa Magomeni, Bw. Salmin Awadh, alitaka kurudishwa kwa hati za usafiri na kusema kuondoshwa kwake kwa kiasi kikubwa kumesababisha kasi ya ujambazi na uhalifu.

Akutukanae hakutafutii tusi! Watanganyika ni wakoloni, majambazi na wahalifu! Dada zetu wanawapelekea ukahaba!

Vijana wao wanaobwia madawa ya kulevya hawawaoni!

Zirudi hizo pasi lakini safari hii kwa pande zote mbili. Machogo waingie Zanzibar kwa pasi na wao waingie kwetu kwa pasi. Tuanzishe na mpango wa residency permit. Hakuna kukaa nchi ya mwingine bila kibali. Si ndiko tunakoelekea?
 
Mimi nimechoshwa na hizi chokochoko za wazanzibari kuhusiana na muungano.Sifahamu nini tunachoendelea kuung'ang'ania,sioni sababu ya kuridhisha ya kuendelea kuwa nao kama wao ''wazanzibari'' hawataki.

Ipo haja ya kufanya kura za maoni kwa nchi nzima kuona kama tunahitaji kuwa na huu muungano au la.

Na kama hatuihitaji kuwa na muungano,nini hatima ya wapemba na wazanzibari wengine wanaomiliki ardhi,nyumba na biashara huku bara (Tanganyika)?

Yangu macho na masikio!

Hizo si chokochoko bali ni madai halisi yanayotakiwa kutatuliwa. Kwa akili ya kawaida mtu hulalamika paspo maslahi na si busara kumuona mwengine akilalamikia jambo na kumfanya mpuuzi bali ni kutafakari tatizo linalompelekea kulalamika.
Ni tabia ya binaadamu kuona mzigo wa mwenziwe mwepesi na kuona kifurushi alichonacho yeye ndio mzigo. Tumekuwa tukilalama na ufisadi na mikataba mibovu na hata kuwaona viongozi wetu hawana lolote wanalofanya na hatuonani wapuuzi. Wazanzibari wana sababu ya kujitetea na mfumo mbaya wa Muungano. Suluhisho ni marekebisho kinyume cha hivyo.............
 
Jamani mbona jazba? haya ni mawazo ya mtu mmoja tu naona yanachukiwa kama ndio msimamamo wa kila Mzanzibar kupelekea wengine kuanza kunyosha chuki zao siji tumewachoka, wabaguzi, wanachagua hewa nk.

The issue hapa ni kuwa huyu mwakilishi kachemka na kwa kuwa ni mwakilishi kutoka upinzani ( cuf ) one can see the motives as kuvutia wapiga kura na kupata publicity. Huyu ni wa kudharauliwa tuu na kama walivyosema wachangiaji wengine kama wanataka kuanzisha huo mpango wa passport then there should be two way traffic na wao wakija Bara waje na pass na tuende mbele zaidi kuwe na resident permit/work permit vilevile.
 
Back
Top Bottom