Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Fundi mchundo naona unashindwa kuelewa kwamba tunaong'ang'ania muungano ni sisi watu wa bara.
Hivi unasoma hata magazeti? Ni mara nyingi viongozi wa visiwani walisema wamechoka na muungano.
Sisi watangayika tukisikia hayo tunaanza kuwashitaki nakusema wanavunja sheria.
Waziri kiongozi wa Zanzibar akiitetea Zanzibar yake basi ni kama Pinda bara.
Wazanzibari wengi hawautaki muungano bali sisi wa bara tumewang'ang'ania kwa kuogopa kwamba watatupita kimaendeleo na wananchi wengi watauliza kwanini Zanzibar iweze sisi tushindwe.
Unawajua mafisadi wangapi kutoka visiwani?
Kwenye bajeti gani wawe mafisadi? Mafisadi wa Zanziba ni hao wafanyabiashara uchwara (wakina Raza n.k.) wanaoshirikiana na wanasiasa.
Ni imani potofu kusema kuwa ni watanganyika wanaowang'ang'ania wazanzibar. Ni viongozi wachache ambao katika kumuenzi baba wa taifa wanaona muungano kuwa ni sacrosant. Ukweli ni kuwa watanganyika wengi wala hawana habari na kinachoendelea Zanzibar. Kuwepo kwake na kutokuwepo kwake hakumsaidii chochote. Tofauti ni kuwa Zanzibar wanapiga kelele wakati wenzao wako kimya. Kuwa kimya kwao si kuwa wanaafiki hali ilivyo. Mara chache wanatokeza watu kama Mchungaji Mtikila wanaotamka bayana kuwa hawana mpango na Muungano.. Lakini unaamini kweli kama itafanyika referendum pande zote mbili, watanganyika watautaka Muungano? Unadhani hizi habari za madeni ya Tanesco, vurugu za unguja na pemba n.k. haziwagusi?
Tatizo ni kuwa kwa kukaa kimya kwao, wenzetu wanachukua fursa kutafuta umaarufu usio na maana kwa kututia vidole machoni! Ukoloni gani wakati wamepewa upendeleo katika Bunge la Muungano? Hivi kama kweli hiyo idadi ya majimbo huko Zanzibar inaendana na hali ilivyo? Chama kilichoshinda Pemba leo ndio kinakuwa Chama kikuu cha upinzani! Uwaziri hata katika wizara ambazo si za Muungano wanapewa wazanzibari bila mtu kulalamika. Watanganyika wanazuiwa kupiga kura Zanzibar wakati wazanzibari ruksa kupiga kura na kukaa kokote katika Tanganyika bila kubughudhiwa na mtu! Wanadai kudhalilishwa kwa Rais wao kwa kutokuwa makamu wa Raisbila kuangalia kuwa kuna Makamu wa Rais (ambaye atamrithi Rais kama jambo lolote likimpata) kutoka Zanzibar! Hawataki kusema kuwa ikiwa Rais wa Zanzibar atakuwa Makamu wa Rais, basi itabidi agharamiwe na serikali ya Muungano! Walidai Mamlaka kwenye bandari zao , wakapewa. wameshindwa kuziendeleza lakini leo wanadai wapewe mgao kwenye Bandari za Tanganyika!
Mchezo wanaofanya viongozi wa Zanzibar ni mbaya. Wao wanaaminim kuwa hata iwaje watanganyika hawawezi kuutema Muungano. Lakini wanasahau uvumilivu una kikomo chake. Na sio wote watakaokuja watakuwa na sentiments za viongozi wa sasa.
Hakuna kiongozi wa Zanzibar anayetamka wazi kuwa muungano uvunjwe. Wanachodai ni marekebisho ambayo yataupelekea kufa. Sasa kwa nini watupatishe taabu kote huko? Waseme tuu, kuwa Muungano hatuhutaki, tuanze mazungumzo ya kugawana mali. Lakini, chonde chonde, yasiwakute yaliowakuta viongozi wa Quebec. Referendum ilipofanywa, na wananchi kufahamu kuwa si masihara tena, canada ndio hio, wakawatosa. Tumeoleana, tumezoeana, msitake kutuharibia!