Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
ONE DAY YES ZANZIBAR WILL BE FREE FROM MKOLONI MWEUSI ,WACHENI TULANE WENYEWE KWA WENYEWE LAKINI HATUMALIZANI ,

Kumbe tatizo ni weusi wetu? Halafu unajifanya mfuasi wa Robert Nesta Marley?

Yule aliyesema;

Until the philosophy which hold one race superior
And another
Inferior
Is finally
And permanently
Discredited
And abandoned -
Everywhere is war -
Me say war.

That until there no longer
First class and second class citizens of any nation
Until the colour of a man's skin
Is of no more significance than the colour of his eyes -
Me say war.


Unamsikiliza lakini haumuelewi.
 
waache tu, hata wakijitenga hamna shida. kwani sisi tunawang'ang'aniza hawa watu tuwe nao, mbona siku zote nuisence tu kwetu? wanasumbua sana. tukiwaacha wazenji waende na hamsini zao pengine ndo tutasettle. kama wao wanataka sisi twende ne pasport, basi wamewakomesheni nyie mnaopenda kwenda kule. hata ninyi fanyeni wao waje na passport tena na visa, muone wapemba watakapohangaika na majini yao hapa bongo kwenye maduka yao ya kuvukiza uvumba yale.

nijuacho mimi, pengine wanajiandaa kwa uchaguzi, au kuwajua wazenji halisi ni akina nani. na kama bara bado tunasuasua tu kwenye vitambulisho, waacheni wao watupiku tu. toka lini tumesikia vitambulisho kuja bara na hatupati?
 
Kumbe tatizo ni weusi wetu? Halafu unajifanya mfuasi wa Robert Nesta Marley?

Yule aliyesema;

Until the philosophy which hold one race superior
And another
Inferior
Is finally
And permanently
Discredited
And abandoned -
Everywhere is war -
Me say war.

That until there no longer
First class and second class citizens of any nation
Until the colour of a man's skin
Is of no more significance than the colour of his eyes -
Me say war.


Unamsikiliza lakini haumuelewi.



,,,,,,Yap imetulia FM,,,,,jamaa wana hisia za rangi kupita kiasi,wakati kwa bibi yangu huko Igunga(Nata,Choma,Ndekeli,Iborogero,Ndembezi na Ussongo) kuna waarabu wenye minywele mpaka mgongoni manake,lakini Wasukuma haswa na hata Kiswahili hawajui,na wanaji feel ni Watanzania haswa,ukanda huo una julikana kama MUSCAT fisi,wazenji tuache ubaguzi bwana,tujenge nchi yetu hii nzuuuri,yenye Milima na Mabonde,Embu ruka na ndege siku moja ukitokea Zanzibar,halafu uione Tanzania ilivyo nzuri,acheni jamani,tukiweza kuwatimua MAFISADI hawa,tukapata wasimamizi wazuri,mambo yote haya yatakwisha,kwani tuna kila kitu cha kutufikisha paleee pazuri,and the Tanzania Mainland is our Buffer Zone(sijui ka tunajua hili wa znz)
 
Nyerere alisema kweli katika moja ya hotuba zake kwamba shida ya muungano inaanzishwa na viongozi walafi wa madaraka huko visiwani.
Lakini siku tukisema basi kuanzia leo Unguja na Pemba kwendeni kwenu, baada ya siku si nyingi tutasikia wapemba wakiwaambia waunguja kwamba nanyi si wazanzibari.
Poleni wazanzibara kwa kukutana na karaha hii.

Wazanzibara hawana cha kupoteza. nchi hii (Tanganyika) haijui wananchi wake. Watajiita Wazaramo au Wadigo. Kwisha.
 
,,,,,,Yap imetulia FM,,,,,jamaa wana hisia za rangi kupita kiasi,wakati kwa bibi yangu huko Igunga(Nata,Choma,Ndekeli,Iborogero,Ndembezi na Ussongo) kuna waarabu wenye minywele mpaka mgongoni manake,lakini Wasukuma haswa na hata Kiswahili hawajui,na wanaji feel ni Watanzania haswa,ukanda huo una julikana kama MUSCAT fisi,wazenji tuache ubaguzi bwana,tujenge nchi yetu hii nzuuuri,yenye Milima na Mabonde,Embu ruka na ndege siku moja ukitokea Zanzibar,halafu uione Tanzania ilivyo nzuri,acheni jamani,tukiweza kuwatimua MAFISADI hawa,tukapata wasimamizi wazuri,mambo yote haya yatakwisha,kwani tuna kila kitu cha kutufikisha paleee pazuri,and the Tanzania Mainland is our Buffer Zone(sijui ka tunajua hili wa znz)

U sound good King Zenj. Pengine ni Bw-mdogo-kiumri- (kama sivyo kumradhi). Lakini usiiiwache Zanzibar ikapoteza identity yake. ikapoteza haki yake kama ni nchi. Imekuwa hivyo toka enzi za enzi- Bw. King. Muungano haugombi lakini sio wa kuifanya Zanzibar kama Sumbawanga. Na W-Tanganyika hawajakatazwa kuhamia Zanzibar. Walioamua si wako huko nawamemkuwa -Intergrated- Ni wazanzibari (wazanzibara sasa) Nenda katembelee huko. Kuna kimtaa kinaitwa Nyarugusu (kule Kizimbani)
 
ONE DAY YES ZANZIBAR WILL BE FREE FROM MKOLONI MWEUSI ,WACHENI TULANE WENYEWE KWA WENYEWE LAKINI HATUMALIZANI ,ILA NAOGOPA USALAMA WA WATANGANYIKA UMO MIKONONI MWA HUU MUUNGANO SIKU UKISAMBARATIKA NDIPO SIKU TANGANYOKA ITAKAPOTOA WAKIMBIZI ,JAPO HIVI SASA WAPO WANAOKIMBIA Mapigano ya kikabila ila watapatikana wa kitaifa.
GOD BLESS ZANZIBAR , Halafu Muungano mbona ulikwisha kufa zamani imebaki mazishi tu maana bado maiti hajapatikana.
HAPPY X-MASS to everyone out there , Dont panic still the time gap is high .
Hata kama CUF hawatotaka kuuvuruga muungano bado wenye siasa zenye msimamo mkali wataendeleza mapambano ya kuidai Zanzibar ---as marehemu Mtakatifu BOB MARLEY alipoiambia jamii ya kimasikini GET UP STAND UP & STAND UP FOR YOUR RIGHT

Mwiba Muungano ukifa Seif anaingia Ikulu kilaini kabisa vichogo hatuji kuiba kura zenu na wala JW hawatakuja mtabaki na JKU na KMKM, hapo ndio kitim tim...
 
Mimi ni mtanganyika na katika nchi zote nilizoishi ugenini watu wana vitu vya kuwatambulisha.

Kwanini Tanzania hatuna. Huu ni upuuzi mkubwa. Kuna watu wanaoishi Tanzania ambao hawana uraia wa Tanzania. Wanatumia haki zote za kiraia za kwenda shule, kuomba mikopo etc bila kuwa raia. Na wapo wanaofanya uharifu.

Mjadala huu inabidi tuanzishe huku Tanganyika pia. Bila kitambulisho na makaratasi mtu asiishi.

Kutaka vitambulisho sio ubaguzi.
 
Vitambulisho vya uraia ni muhimu kwa kila mTZ,lazima tuwe navo
Hapa wazenj wanataka vyao,wapewe,waachwe wafanye wapendayo.
Ikiwezekana wawapige stop waTanganyika kwenda kwao kabisa,yeah.
Wazenj walioko tanganyika wafukuzwe haraka tena sana,majumba na mali zao zinakuwa zetu.yeah!!
 
,,,,,,,Ndugu yangu tatizo la UMEME ni kubwa sana,na kama unakumbuka wakati ule tuliolala gizani kwa mwezi mmoja tu ilikuaje,naogopa sana kujipiga kifua katika hili suala la nishati,Umeme wa generator za diesel ni balaa,kwa mapato yetu haya kiduchu zenji hapa,sidhani kama tutaweza kuhimili kukimbiza vinu hivyo kwa saa 24/7 kwa wiki,labda tununue toka KENYA au Msumbiji???,mzee unazungumzia $ hapo na sio TSHS,na ujue ikifikia stage hiyo,basi mpaka mbatata, nyanya, kitunguu toka Tabora kule na mchele wa Mbeya itabidi uwe imported kwa $ pia,Haya mambo hayapo rahisi kama mnavyofikiria wazee,tusijidai tupo tayari kufa wakati hata KUZIMIA tu hatuwezi.

Kweli wanasema ukibishana na mmtu asiyejua unapoteza muda wako bure.

Kitu kinachokwamisha nchi nyingi ya afrika ni uongozi kama hujui.

Zanzibar pamoja nakwamba ina import mahitaji mengi lakini ikiwa na viongozi wazuri inaweza kupiga hatua hata kutushinda sisi wa bara ambao tuna tanzanite, dhahabu, mbuga, kilimo, sijui na nini vitu kedekede.

Kingzenj umesoma somo la uchumi? apparently NOT

Unajua kwamba nguo nyingi zinazouzwa ulaya kama Tommy hilfiger, Reply jeans na nguo nyingi tu zenye labels zakufahamika zinatengenezwa Indonesia na nchi nyingine kutoka ulimwengu wa tatu? Kama uko ulaya umeshawahi kununua nguo made in Kenya? na inatamba kwenye fashion.

Jiulize je Indonesia wanapata wapi pamba kama sio kutoka marekani.

Ukinunua Tommy USA basi jua zimetengenezwa Indonesia na nchi nyingi tu ambazo ziko dunia ya tatu. katika kushirikiana na nchi tajiri basi nchi za dunia ya tatu uchumi wao nao unakua kwa kasi.

Zanzibar ikiondokana na sera za CCM inaweza kufanya vizuri mkashangaa.

Unajua kanchi kanakoitwa Singapore?

Nitapoteza muda wangu bure, ila ninachokuomba kama hujasoma uchumi basi japo soma kidogo.
 
Kweli wanasema ukibishana na mmtu asiyejua unapoteza muda wako bure.

Kitu kinachokwamisha nchi nyingi ya afrika ni uongozi kama hujui.

Zanzibar pamoja nakwamba ina import mahitaji mengi lakini ikiwa na viongozi wazuri inaweza kupiga hatua hata kutushinda sisi wa bara ambao tuna tanzanite, dhahabu, mbuga, kilimo, sijui na nini vitu kedekede.

Kingzenj umesoma somo la uchumi? apparently NOT

Unajua kwamba nguo nyingi zinazouzwa ulaya kama Tommy hilfiger, Reply jeans na nguo nyingi tu zenye labels zakufahamika zinatengenezwa Indonesia na nchi nyingine kutoka ulimwengu wa tatu? Kama uko ulaya umeshawahi kununua nguo made in Kenya? na inatamba kwenye fashion.

Jiulize je Indonesia wanapata wapi pamba kama sio kutoka marekani.

Ukinunua Tommy USA basi jua zimetengenezwa Indonesia na nchi nyingi tu ambazo ziko dunia ya tatu. katika kushirikiana na nchi tajiri basi nchi za dunia ya tatu uchumi wao nao unakua kwa kasi.

Zanzibar ikiondokana na sera za CCM inaweza kufanya vizuri mkashangaa.

Unajua kanchi kanakoitwa Singapore?

Nitapoteza muda wangu bure, ila ninachokuomba kama hujasoma uchumi basi japo soma kidogo.

Kweli unajipotezea muda maana unatoa mifano bila hata kuelewa kwa nini iko hivyo! Nadhani umesoma uchumi lakini haukumuelewa mwalimu wako. Au mwalimu alikuwa bomu.
 
Kweli unajipotezea muda maana unatoa mifano bila hata kuelewa kwa nini iko hivyo! Nadhani umesoma uchumi lakini haukumuelewa mwalimu wako. Au mwalimu alikuwa bomu.

Lets talk about Singapore shall we!!?



Singapore: A Small Nation With a Big Economy
Singapore's pro-business environment continues to nurture an economy that is poised to become globalized, knowledge-based, and increasingly diversified.

By Michelle Janowitz


Singapore may only be three and a half times the size of Washington, D.C., but this city-state's economic strength and resilience is anything but small. Singapore's strategic location places it in the midst of a Southeast Asian market of 500 million people, and an Asian market of 2.8 billion. Hailed as the gateway to Asia, Singapore is an attractive location for businesses, big and small, seeking to penetrate Asian markets.

After finally gaining independence in 1965, Singapore was faced with a small domestic market and a dearth of natural resources. In response to this, the government adopted an economic policy that was pro-business, pro-foreign investment, and export-oriented. This economic paradigm has proven very successful and still dominates economic policy in Singapore today.

Embracing globalization and a commitment to a knowledge-based economy, Singapore's government is making strides to establish a growth path for the economy steeped in technology and innovation. One of the primary sources of economic growth in Singapore has been high-tech manufacturing. Electronics and precision engineering currently reign as the strongest forces within this sector, driven by growth in the semiconductor, data storage, and electronic modules and components industries. Just last year Seagate, the U.S.-based disc drive giant, made clear its intentions to invest $500 million over the next five years in its Singapore-based operations.

"Within a changing global economic landscape, Singapore is well-positioned for the next phase of economic development, and the country continues to provide an attractive environment in which to conduct business," says William Watkins, Seagate's president and chief operating officer.

The Economist Intelligence Unit, a provider of country, industry, and management analysis, credited Singapore with having the top business environment in Asia in 2003. In addition to world-recognized accolades, Singapore has many elements set in place to support its pro-business environment. Among these is a government that is stable and highly attuned to the needs of businesses. Singapore's strong legal system, stringent guidelines on intellectual property, and competitive corporate tax rate showcase the government's understanding of the needs of businesses. Singapore's government also aggressively supports free trade and has established a multitude of free trade agreements (FTAs) with many key international markets. The U.S.-Singapore FTA, established in 2003, is the first such agreement between the U.S. and an Asian country. U.S. investment in Singapore is estimated at approximately $23 billion, and this new FTA should further facilitate economic growth from U.S. companies in the region. Singapore is also actively negotiating other FTAs with key trading partners, such as the European Union and China.

Business Facilities -Singapore: A Small Nation With a Big Economy
 
Anzia ilikotokea na si waliko sasa. Wakati wakiwa ni kajibandari kadogo tuu. Ukifanya hivyo utaelewa kwa nini Zanzibar si Singapore!
 
Anzia ilikotokea na si waliko sasa. Wakati wakiwa ni kajibandari kadogo tuu. Ukifanya hivyo utaelewa kwa nini Zanzibar si Singapore!

Na miwani pia unataka ili uone??

After finally gaining independence in 1965, Singapore was faced with a small domestic market and a dearth of natural resources. In response to this, the government adopted an economic policy that was pro-business, pro-foreign investment, and export-oriented. This economic paradigm has proven very successful and still dominates economic policy in Singapore today.
 
Wacheni maneno bana , Zanzibar ikiuza bareli mia tu za mafuta kwa mwezi basi haihitaji uchovu wa dhahabu wala granite au tanzanite ambazo wababe wachache ndio wanaoziiba huko na kuzifanyia dili za kimataifa,tena ikiongeza na kufika ka mapipa mia tano kwa mwezi basi hata wazenji wanaweza wasifanye kazi just wanaenda kupokea hundi na kuziwakilisha benki kwa ajili ya malipo fikiria wazenji hawafiki hata milioni moja na robo ,hivyo wakipanga wastani wa kuuza mapipa ya mafuta na population yao basi ndio hivyo watazidi kuwa weupe ila hivi sasa wamechakaa na kuchakazwa na visa na mikasa ya mkoloni mweusi chini ya utawala wa Tanganyika ndani ya Tanzania ,muungano mazishi matupu na serikali yake imejaa wala rushwa mpaka wengine wanakiri kuwa walarushwa au mafisadi ni watu hatari kuwakamata ....sasa sijui vyombo vya habari tulivyonavyo kama vilimuuza mkulu kwa nini alisema au alifikia kusema hivyo wakati yeye ni kiongozi mkuu wa nchi ,hivi hamuoni kama hakuna haja ya muungano maana utawala umeshawashinda walioko kwenye madaraka ,kwa kauli hizo walikuwa wawe tayari wamewajibika na kuwapisha wenye ubavu.
Mko tayari kufa kuulinda Muungano lakini ni waoga wa kuwakaba makend mafisadi eti mnatafuta ushahidi au ushahidi hautoshi ,hapa hapahitaji ushahidi unatosha au hautoshi ,tume imewakilisha ripoti watu wamejiuzulu hivyo kinagojewa kitu gani ,au ndio huko kuogopana na watu wahusika ni hatari ? Mtikila kamfikisha kigogo mahakamani the probability ,atashinda au atashindwa lakini inaonekana ...iweje serikali inashindwa ,hivi ni nini faida ya serikali kuwa na mawakili kibao nini kazi ya watu hawa ?
Serikali ina vyombo vingi kama njugu Mtikila ni private anategemea sifuri ukilinganisha na serikali katika nguvu na kupata ushahidi Mtikila anatumia nguvu ya uraia wake , Je serikali inahitajia nini ili kuwafikisha mafisadi mahakamani ? Eti ukimfikisha fisadi utaathiri na wengine ? Serikali ya Muungano haifai kwa maslahi ya Tanganyika vipi itafaa kwa maslahi ya Zanzibar ,Kama mafisadi hawa hawakukamatwa kinguvu na nguvu ya Mkuu wa Nchi aliyepo madarakani kutumia ranki yake basi itakuwa haifai kabisa hizi habari za ufisadi si shutuma ni mambo kwa maandiko ,washiriki hata ukisema makampuni hewa ,eti jamani kama ni hewa basi aliyewakilisha hiyo kampuni hewa kupeleka na kupokea makaratasi ndio atakuwa mhusika mkuu ,na kama ulisainishwa makaratasi ya kampuni hewa aliyekusainisha au kukukabidhi makaratasi ndie wa kumbana na kutaja alipata wapi makaratasi hayo kama ni waziri au katibu kata.
Mtalindana mpaka lini ,kunahitajika Raisi asie na usongo na wanaoendesha vyombo vya serikali kwa maslahi yao ,hawa ni lazima wote wakamatwe wataenda kujitetea jela au rumande.
Naweza kusema Raisi anaogopa kutumia madaraka yake hivyo hivyo Mkuu wa Polisi au wa upelelezi Mheshimiwa Kikwete amesikika mara kadhaa akisema ameshatoa wigo wa kufanyiwa kazi ,sasa kurudi kwa Raisi na kumwambia rafiki yako anahusika huko ni kumchonganisha.
Walitakiwa waliopewa nguvu na Raisi kuwakamata watu wahusika mara moja na kama ni Rafiki wa Raisi au waziri Mkuu basi gari ya ikulu itaonekana ikiiingia na kutoka katika vituo vya polisi kwa ajili ya kuwatetea wahusika na hapo ndipo itajulikana kama Raisi ametumia madaraka kuwaachia huru watuhumiwa.
Ila kwenye Muungano tunaona watu wanavyoshughulika wanasheria sijui manani wote kifua mbele kauli nzito nzito kuutetea Muungano usiojulikana faida yake kila siku ni makero juu ya makero ,eti wanajadili ,aibu tupu miaka nenda miaka rudi watu wanajadili kero za Muungano wa ajabu uliofanywa na kuratibiwa na watu wawili , really nonesense!! Ni upotezaji wa fedha za walala hoi tu hakuna kinbachofikiwa hata kimoja kikajulikana kuwa hili au hiki kimepatikana kwa natija ya mazungumzo ya kutatua kero au lipo ? Sawa na mazungumzo ya muwafa CCM/CUF vikao vingapi vimefanyika fedha ngapi zimetumika nani akilipia mazungumzo hayo fedha hiyo jiulizeni imetoka wapi ? Bila ya shaka kuna posho ambayo ni fedha wapi imetoka ? Na nini kimefikiwa kama si ukiritimba wa fedha ambazo hazijulikani ni kiasi gani ? Sasa wanatafuta eti kura waulizwe wananchi hivi hakutahitajika fedha hapo ? Mlo mwengfine huo !
Muungano ni chaka la mafisadi na hakuna faida kwa mwananchi wa kawaida haya ya vitambulisho na pasipoti ni mihimili ya kutafuta njia zingine za kujipatia ulaji ,maana vitu hivi ni kitu ambacho kikatiba ni haki ya kila raia (Passport) ukizaliwa tu unapatiwa ID yako na ukoo mzima utajulikana kutokana na file numberz hivyo ,jambazi mwizi fisadi akikamatwa tu anajulikana ,hata anegongwa na gari ugenini basi atajulikana ni fulani kutoka kijiji fulani ndugu na jamaa zake watajulikana kirahisi as party with finger prints ambazo sasa zinakusanywa katika pasi za kusafiria.
Serikali isiwababaishe watu na mambo ya Muungano na mengine wezi wa ufusadi mkubwa ambao haujawahi kuikumba Tanzania au tuseme ubadhirifu uliogundulika ni lazima ufanyiwe kazi kikamilifu na kuwaliwaza waTz wote wa bara na visiwani.
Kuna dili kibao tu ,tuchukulie ile ya Rada ni kitu open wacha hapa Tz hata Nchi za nje zinaijua sasa ni kitu gani kinachoifanya serikali kuwakalia kimya wahusika ? Usalama wa Taifa hili la Tz uko wapi ?
 
Mwiba Muungano ukifa Seif anaingia Ikulu kilaini kabisa vichogo hatuji kuiba kura zenu na wala JW hawatakuja mtabaki na JKU na KMKM, hapo ndio kitim tim...


umeniua mbavu zangu, yaani kusema wabara ndio wenye vichogo na counterpart ni flat head??!! Kiukweli, huu muungano umeshakufa ni mazishi tu ndio yanasubiriwa.
 
..yetu macho na masikio sasa.

..Mtaalamu aliwahi kudai ZNZ hakuna mafuta.

..sijui ni nini kimo ktk ripoti yake.

..je, ka-inzi ka jamii forums kanaweza kunusu kilichomo kwenye ripoti??

Mtaalamu akabidhi ripoti ya mafuta Z’bar

na Mwanne Mashungu, Zanzibar


HATIMAYE Mtaalamu kutoka Kampuni ya AUPEC ya nchini Uingereza, David Reading, amekabidhi ripoti itakayotumika katika mgawo wa mafuta na gesi asilia kati ya pande mbili za Muungano wa Tanzania.

Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himidi, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar.

Alisema mtaalamu huyo amekabidhi ripoti hiyo mwezi huu na inatarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Baraza la Mapinduzi mwezi ujao kabla ya Kamati ya kujadili kero za muungano kukutana Januari mwakani chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein.

“Rasimu ya ripoti yake inatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Mapinduzi mapema mwezi ujao, kabla ya ripoti hiyo kuwasilishwa katika kikao cha kujadili kero za muungano kitakachokutana Januari mwakani,” alisema Waziri Mansour.

Aliyataja maeneo yaliyohusu utafiti kuwa ni mgawanyo wa mapato na gharama za uzalishaji wa mafuta na gesi asilia, katiba, sheria na muundo wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC), lakini alisema mapema kueleza kiwango cha mgawo kilichopendekezwa na mtaalamu huyo kati ya pande hizo za muungano.

Waziri Mansour alisema mshauri huyo elekezi katika ripoti yake ameshauri sheria ya kuundwa kwa TPDC kuangaliwa upya, ili liwe na sura ya muungano badala ya sheria ya sasa kuruhusu shirika hilo kufanya kazi zake upande mmoja wa muungano.

Hata hivyo, alisema suala la mafuta ya Zanzibar kubakia katika orodha ya mambo ya muungano litaamuliwa na wananchi wa Zanzibar baada ya ripoti hiyo kufikishwa katika vikao vya juu kwa vile wajumbe wengi wa Baraza la Wawakilishi kupinga suala hilo kuendelea kubakia katika orodha ya mambo ya muungano.

Mansour, alisema msimamo wa wajumbe wa Barza la Wawakilishi CCM na CUF hadi sasa wanatetea suala la mafuta ya Zanzibar liondolewe katika orodha ya mambo ya muungano kwa vile Zanzibar kwa madai liliingizwa kinyemela na serikali ya awamu ya kwanza chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

“Nyote mmeona wajumbe wa CCM na CUF waliungana kwa kauli moja wakitetea suala la gesi na mafuta yawe ni rasiliamali ya Wazanzibari, ndiyo maana nasema wananchi wenyewe ndio watakaoamua baada ya vikao vya juu kujadili suala la mafuta Zanzibar,” alisema.

Hata hivyo, alisema baada ya serikali kumaliza kupitia ripoti hiyo itawekwa hadharani, ili wananchi wapate nafasi ya kufahamu kwa undani mambo ya msingi yaliyopendekezwa na mtaalamu huyo.

Wakati huo huo, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefanikiwa kuokoa sh bilioni 13 kutoka katika mradi wa kuvuta umeme wa gridi ya Taifa kutoka mkoani Tanga hadi kisiwani Pemba.
 
Wapeni mafuta yaliyo ndani ya eneo lao. Rasilimali zote za asili na nishati mbalimbali ni bora zikafanywa ziwe aidha za visiwani au bara pekee. Natambua ya kwamba hakuna serikali ya Tanzania bara lakini Tanzania bara si ipo?
 
Back
Top Bottom