Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
ONE DAY YES ZANZIBAR WILL BE FREE FROM MKOLONI MWEUSI ,WACHENI TULANE WENYEWE KWA WENYEWE LAKINI HATUMALIZANI ,
Kumbe tatizo ni weusi wetu? Halafu unajifanya mfuasi wa Robert Nesta Marley?
Yule aliyesema;
Until the philosophy which hold one race superior
And another
Inferior
Is finally
And permanently
Discredited
And abandoned -
Everywhere is war -
Me say war.
That until there no longer
First class and second class citizens of any nation
Until the colour of a man's skin
Is of no more significance than the colour of his eyes -
Me say war.
Unamsikiliza lakini haumuelewi.
Nyerere alisema kweli katika moja ya hotuba zake kwamba shida ya muungano inaanzishwa na viongozi walafi wa madaraka huko visiwani.
Lakini siku tukisema basi kuanzia leo Unguja na Pemba kwendeni kwenu, baada ya siku si nyingi tutasikia wapemba wakiwaambia waunguja kwamba nanyi si wazanzibari.
Poleni wazanzibara kwa kukutana na karaha hii.
,,,,,,Yap imetulia FM,,,,,jamaa wana hisia za rangi kupita kiasi,wakati kwa bibi yangu huko Igunga(Nata,Choma,Ndekeli,Iborogero,Ndembezi na Ussongo) kuna waarabu wenye minywele mpaka mgongoni manake,lakini Wasukuma haswa na hata Kiswahili hawajui,na wanaji feel ni Watanzania haswa,ukanda huo una julikana kama MUSCAT fisi,wazenji tuache ubaguzi bwana,tujenge nchi yetu hii nzuuuri,yenye Milima na Mabonde,Embu ruka na ndege siku moja ukitokea Zanzibar,halafu uione Tanzania ilivyo nzuri,acheni jamani,tukiweza kuwatimua MAFISADI hawa,tukapata wasimamizi wazuri,mambo yote haya yatakwisha,kwani tuna kila kitu cha kutufikisha paleee pazuri,and the Tanzania Mainland is our Buffer Zone(sijui ka tunajua hili wa znz)
ONE DAY YES ZANZIBAR WILL BE FREE FROM MKOLONI MWEUSI ,WACHENI TULANE WENYEWE KWA WENYEWE LAKINI HATUMALIZANI ,ILA NAOGOPA USALAMA WA WATANGANYIKA UMO MIKONONI MWA HUU MUUNGANO SIKU UKISAMBARATIKA NDIPO SIKU TANGANYOKA ITAKAPOTOA WAKIMBIZI ,JAPO HIVI SASA WAPO WANAOKIMBIA Mapigano ya kikabila ila watapatikana wa kitaifa.
GOD BLESS ZANZIBAR , Halafu Muungano mbona ulikwisha kufa zamani imebaki mazishi tu maana bado maiti hajapatikana.
HAPPY X-MASS to everyone out there , Dont panic still the time gap is high .
Hata kama CUF hawatotaka kuuvuruga muungano bado wenye siasa zenye msimamo mkali wataendeleza mapambano ya kuidai Zanzibar ---as marehemu Mtakatifu BOB MARLEY alipoiambia jamii ya kimasikini GET UP STAND UP & STAND UP FOR YOUR RIGHT
,,,,,,,Ndugu yangu tatizo la UMEME ni kubwa sana,na kama unakumbuka wakati ule tuliolala gizani kwa mwezi mmoja tu ilikuaje,naogopa sana kujipiga kifua katika hili suala la nishati,Umeme wa generator za diesel ni balaa,kwa mapato yetu haya kiduchu zenji hapa,sidhani kama tutaweza kuhimili kukimbiza vinu hivyo kwa saa 24/7 kwa wiki,labda tununue toka KENYA au Msumbiji???,mzee unazungumzia $ hapo na sio TSHS,na ujue ikifikia stage hiyo,basi mpaka mbatata, nyanya, kitunguu toka Tabora kule na mchele wa Mbeya itabidi uwe imported kwa $ pia,Haya mambo hayapo rahisi kama mnavyofikiria wazee,tusijidai tupo tayari kufa wakati hata KUZIMIA tu hatuwezi.
Kweli wanasema ukibishana na mmtu asiyejua unapoteza muda wako bure.
Kitu kinachokwamisha nchi nyingi ya afrika ni uongozi kama hujui.
Zanzibar pamoja nakwamba ina import mahitaji mengi lakini ikiwa na viongozi wazuri inaweza kupiga hatua hata kutushinda sisi wa bara ambao tuna tanzanite, dhahabu, mbuga, kilimo, sijui na nini vitu kedekede.
Kingzenj umesoma somo la uchumi? apparently NOT
Unajua kwamba nguo nyingi zinazouzwa ulaya kama Tommy hilfiger, Reply jeans na nguo nyingi tu zenye labels zakufahamika zinatengenezwa Indonesia na nchi nyingine kutoka ulimwengu wa tatu? Kama uko ulaya umeshawahi kununua nguo made in Kenya? na inatamba kwenye fashion.
Jiulize je Indonesia wanapata wapi pamba kama sio kutoka marekani.
Ukinunua Tommy USA basi jua zimetengenezwa Indonesia na nchi nyingi tu ambazo ziko dunia ya tatu. katika kushirikiana na nchi tajiri basi nchi za dunia ya tatu uchumi wao nao unakua kwa kasi.
Zanzibar ikiondokana na sera za CCM inaweza kufanya vizuri mkashangaa.
Unajua kanchi kanakoitwa Singapore?
Nitapoteza muda wangu bure, ila ninachokuomba kama hujasoma uchumi basi japo soma kidogo.
Kweli unajipotezea muda maana unatoa mifano bila hata kuelewa kwa nini iko hivyo! Nadhani umesoma uchumi lakini haukumuelewa mwalimu wako. Au mwalimu alikuwa bomu.
Anzia ilikotokea na si waliko sasa. Wakati wakiwa ni kajibandari kadogo tuu. Ukifanya hivyo utaelewa kwa nini Zanzibar si Singapore!
Mwiba Muungano ukifa Seif anaingia Ikulu kilaini kabisa vichogo hatuji kuiba kura zenu na wala JW hawatakuja mtabaki na JKU na KMKM, hapo ndio kitim tim...
Mtaalamu akabidhi ripoti ya mafuta Zbar
na Mwanne Mashungu, Zanzibar
HATIMAYE Mtaalamu kutoka Kampuni ya AUPEC ya nchini Uingereza, David Reading, amekabidhi ripoti itakayotumika katika mgawo wa mafuta na gesi asilia kati ya pande mbili za Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himidi, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar.
Alisema mtaalamu huyo amekabidhi ripoti hiyo mwezi huu na inatarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Baraza la Mapinduzi mwezi ujao kabla ya Kamati ya kujadili kero za muungano kukutana Januari mwakani chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein.
Rasimu ya ripoti yake inatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Mapinduzi mapema mwezi ujao, kabla ya ripoti hiyo kuwasilishwa katika kikao cha kujadili kero za muungano kitakachokutana Januari mwakani, alisema Waziri Mansour.
Aliyataja maeneo yaliyohusu utafiti kuwa ni mgawanyo wa mapato na gharama za uzalishaji wa mafuta na gesi asilia, katiba, sheria na muundo wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC), lakini alisema mapema kueleza kiwango cha mgawo kilichopendekezwa na mtaalamu huyo kati ya pande hizo za muungano.
Waziri Mansour alisema mshauri huyo elekezi katika ripoti yake ameshauri sheria ya kuundwa kwa TPDC kuangaliwa upya, ili liwe na sura ya muungano badala ya sheria ya sasa kuruhusu shirika hilo kufanya kazi zake upande mmoja wa muungano.
Hata hivyo, alisema suala la mafuta ya Zanzibar kubakia katika orodha ya mambo ya muungano litaamuliwa na wananchi wa Zanzibar baada ya ripoti hiyo kufikishwa katika vikao vya juu kwa vile wajumbe wengi wa Baraza la Wawakilishi kupinga suala hilo kuendelea kubakia katika orodha ya mambo ya muungano.
Mansour, alisema msimamo wa wajumbe wa Barza la Wawakilishi CCM na CUF hadi sasa wanatetea suala la mafuta ya Zanzibar liondolewe katika orodha ya mambo ya muungano kwa vile Zanzibar kwa madai liliingizwa kinyemela na serikali ya awamu ya kwanza chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.
Nyote mmeona wajumbe wa CCM na CUF waliungana kwa kauli moja wakitetea suala la gesi na mafuta yawe ni rasiliamali ya Wazanzibari, ndiyo maana nasema wananchi wenyewe ndio watakaoamua baada ya vikao vya juu kujadili suala la mafuta Zanzibar, alisema.
Hata hivyo, alisema baada ya serikali kumaliza kupitia ripoti hiyo itawekwa hadharani, ili wananchi wapate nafasi ya kufahamu kwa undani mambo ya msingi yaliyopendekezwa na mtaalamu huyo.
Wakati huo huo, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefanikiwa kuokoa sh bilioni 13 kutoka katika mradi wa kuvuta umeme wa gridi ya Taifa kutoka mkoani Tanga hadi kisiwani Pemba.