kaka yangu unaegemea sana katika ubabe tu. Unafikiri kila siku mtakuwa mnawazonga Wa-zanzibar kwa ubabe tu kwenye vikao vya Dodoma?. Hakuna jipya rudia yale tuliyokubaliana. Kwa mfano tumekubaliana kuwepo kwa SMZ na kuipa jukumu la kuendesha mambo ya Zanzibar kikatiba. Lakini SMZ hiyo tunainyima uwezo kwa kuizuia kukusanya kodi, tunaiingilia kati SMT na kuipora makusanyo ya kodi hizo (TRA na Wizara ya Fedha- ya Mkullo). SMZ tumeiipa jukumu la kushughulikia watu wale wa Zanbzibar- tunainyima fursa ya ku-associate na vyombo vya nje ilikupata nguvu za kuwashuhgulikia watu wale-kwa kisingizio cha Mambo ya Nje ni ya Muungano (ya Benard Membe). Ni mengi- hali iliyopo ni kuwa fursa zinatolewa kikatiba- lakini zinaminywa katika utendaji. Hilo ndio tatizo-Hatuhitaji Serikali tatu wala moja. Mfumo wa sasa urekebishwe-tena marekebisho yenyewe ni kuurudisha katika mstari ili tuutekeleze ipasavyo- Kama tunashindwa hili basi ni kweli tuuvunje Muungano- Majuto ni mjukuu. Kuliko kubabaishana huku tunakofanyiana
 
Jamani punguzeni jazba. ndio nyinyi mnaolifanya hili suala kuwa gumu na kuamsha zile jazba za "retaliation" kutoka upande wa pili mpaka wanasema kama mnaweza basi semeni kule Dodoma mkione. Msaada nusu kwa nusu umeona wapi wewe? kwa vigezo gani ndugu yangu. Kwani yule anayetoa msaada hajui kuwa anaipa Tanzania ambayo Bara ina watu watu milioni 30 na ushei na Zanzibar karibu milioni mbili. Sasa ukidau nusu kwa nusu katika misaada hiyo si wewe ndiye unakuwa mwizi wa hicho mlichopewa na huwafikirii wenzako wa upande wa pili. Punguza jazba unapotosha ukweli.
 

Wishful thinking na ni ule uvivu ninaouzungumzia, jamaa analala mlango wazi!
 
Hii dhana ya Mwiba kuwa kuwa maendeleo visiwani yataletwa kwa misaada (hand outs!), itafanya visiwa hivi kuwa nyuma kiuchumi miaka mingi ijayo!

Chapeni kazi: wakati wa utwana na mtumwa ulishaisha zamani!
 

kwa hiyo kwa mfano utolewe msaada wa $io million, $5 million iende bara kwenye watu millioni 40 na $5million zingine ziende zanzibar kwenye watu 1 million? Sasa hapa nani anakuwa mwizi? Fikirieni kabla ya kuongea. Hela zote zinagawanywa propotionally. Kama mnafuata mfumo huo basi zanzibar ndiyo itakuwa mwizi kwa maana nyie ndiyo mtapata nyingi zaidi in terms of propotion. Think before you talk. Rudi shule ujifunze hisabati.
 
kamakuchapa kazi basi WaTanganyika ndio wachape kazi tena wachapuke kikweli la si hivyo mtakufa njaa japo mmeshaanza kupukutika ingawa ni siri ,lakini ukweli WaTanganyika wanakufa njaa.

Hatutakaa kimya kwa kutona wavivu maana ,kama si ukata milio nao msingetaka kuvamia mafuta ,msingewambia watu warudishe feza kwanza ndio muwapeleke mahakamani ,ila mko taabani ,tena taabani mbaya sana ,tuombe Mwenyezi Mungu aipushe hilo.

Zanzibar inakalishwa na njaa na huu Muungano watu wake wanafariki kwa huu muungano,umewainamia na kuwabamiza kikweli kweli ,mpaka sasa serikali ionashindwa kutoa mishahara kwa mpangilio wa kila mwisho wa mwezi ,kwa sababu jinamizi hili la Muungano linafyonza mapato yote ya Zanzibar ,na huo ndio ukweli.
 
Hii dhana ya Mwiba kuwa kuwa maendeleo visiwani yataletwa kwa misaada (hand outs!), itafanya visiwa hivi kuwa nyuma kiuchumi miaka mingi ijayo!

Chapeni kazi: wakati wa utwana na mtumwa ulishaisha zamani!

Sawa kabisa . Lakini punguzeni kutuwekea vikwazo ili tuweze kuchapa kazi. Tuna Serikali yetu kule, tuna Baraza letu la wawakilishi -katika mambo yetu mkono wenu usiwe mrefu sana na kujifanya -mna-supervise kila kitu na mnataka kutoa ruhsa ya kila kitu kwa jina la kusimamia mambo ya nje na fedha kwa vile ni masuala ya Muungano . Tupeni satuwa.
 
Tatizo unalinganisha Zanzibar na Mtwara ,hapo siwezi kukusaidia ,wewe umesema milioni 10 ,tano ikiwa ipewe Zanzibar ,sasa hukufahamu kuwa ili umuone nani mwizi inakubidi ujue kuwa Zanzibar hapewi hata ndururu ,bila ya shaka hapo utamuona ni nani mwizi.

Hiki kinachozungumzwa sio kuwa kitatokea ni jambo limezoeleka Zanzibar haipewi kitu. wengine mnakuwa mnakurupuka tu na hamjui chanzo cha matatizo na ugonjwa wenyewe hapa hatutafuti kinga ,shida iliyotukumba ni kuwa ugonjwa umekuwa mkubwa na kinga haikuwa applied tokea mwanzo ,hivyo kinachotafutwa ni tiba na inaonekana kuwa ni lazima Tanganyika irudishwe hakuna mbadala wa kutibu zaidi ya huo.
 
Pakacha,

..kuna Zanzibar Revenue Board na Tanzania Revenue Authority. siyo kweli kwamba kila kodi inayokusanywa Zanzibar inachukuliwa na TRA.

..lakini hata kama TRA inakusanya kodi Zanzibar, si bado kuna mgawo toka kwenye hazina ya serikali ya Muungano?

..IMF na WB walipendekeza Zenj ipewe 4.5% toka hazina ya Muungano. je, TRA Zanzibar inakusanya asilimia ngapi ya makusanyo yote ya TRA? je ni zaidi ya 4.5% kiasi kwamba sasa mnalalamika?

..makubaliano 'original' ya Muungano ndiyo yaliyoelekeza tuwe na sera moja ya mambo ya nje. katika msingi wa makubaliano hayo tukaamua kuwa na kiti kimoja Umoja wa Mataifa[UN].

..zaidi ya OIC ni nchi gani ambayo Zanzibar ingependa kuwa na uhusiano nayo lakini mahusiano hayo yakakwazwa na serikali ya Muungano? hivi mmesahau kwamba tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi ili ku-accomodate Zanzibar iliyokuwa na mahusiano na Ujerumani Mashariki?

NB:

..hivi unafikiri ikiundwa serikali ya Tanganyika basi kutakuwa hakuna TRA?

..je, serikali ya Tanganyika ikiundwa kila upande utakuwa na unajitegemea ktk sera ya mambo ya nje, na kuwa na kiti ktk Umoja wa Mataifa?

..je, kila upande utakuwa na hazina,Benki Kuu, na sarafu yake?
 
mbona mwiba umeshinda kutetea kauli yako ya kuwa bara na zenji wote wachukue migao nusu kwa nusu? Or should i take it umeshindwa kutetea hoja yako? Maana naona unachagua cha kujibu ukiona sehemu umeshemsha unai ignore kabisa na kujibu mengine.
 

Haukusema Zanzibar haipewi kitu ulisema hela zigawanywe nusu kwa nusu kati ya sehemu yenye watu 40 million na nyingine yenye watu 1 million au sicho ulichosema wewe? post yako ipo kama ushahidi. na mfano wako wa Mtwara na Zanizbar doesn't even make sense kwa sababu sikuongelea regions niliongelea propotionality kutokana na idadi ya watu au ni hauelewi what proportionality means?
 
1. Ila ukiona wenzetu Visiwani wanvyolalamika, utadhani Bara wanaishi mbinguni na bara wanainyonya Z'bar makusudi tu..ili watu waendelee kuwa maskini! Sijui ni % kubwa kiansi gani wanapinga huu muungano..ila nasema miaka ijayo sioni future ya Muungano wa kweli!

2. Ni Bora kuachana nao: tuwape chao (kama kipo) na kufiriria EAF yaani kujiunga na Kenya, Uganda, Rwanda n.k

3. Sasa kama watu hawataki: basi!!
 

Ndiyo maana akakwambia mnawanyonya teh teh teh maana Zanzibar ingekuwa inajiwakalisha kama nchi kamili nayo ingepata milion $10 na si m$5 tena,Na wakipata huo msaada na wazanzibar wako wakazi milion moja hivyo kwa wastani wanakuwa wamechuma zaidi kuliko wa bara milion 40 hapo ndipo fenomenani ya wazenji ilipo.

Mie kwa upande wangu wazanzibar wangelikokotoa mahesabu vizuri kabisa wakasema Karafuu kwa mwaka inaingiza milion kadhaa ktk pato la taifa,utalii unaingiza milion kadhaa ktk pato la taifa, mafuta yanaingiza ama yataingiza milion kadhaa ktk pato la taifa yani muungano,wakimaliza hapo wanakokotoa tena kuona kila kichwa cha mzanzibar kinaingiza asilimia ngapi ktk pato la taifa kutokana na mapato hayo ya serikali ya zenji yanayoingizwa ktk muungano.Harafu pia kwa bara wakokotoe vivyo hivyo na waone kila mbara anachangia ngapi na hapo watoe malalamiko.

Kingine kama CUF na CCM wapo pamoja mbona ktk serikali ya mseto CCM zanzibar walitoa machozi?
Hawa watu hawako pamoja wala hawana nia yoyote ila wameshawasoma wazanzibar na hata hao CUF ya kuwa kujipatia umaarufu na hatimaye kuchukuwa hatamu kwa upande wa zenji ni kuongelea Muungano.

CCM zanzibar wameteka hoja za CUF na CUF wamekubali kutekwa kwa mantiki hiyo 2010 CUF hawana sera ya kuuiza kwa wazanzabar .
 
 
Mwiba,

..ni mara chache sana wafadhili kutoa msaada fedha bila kuelekeza mradi ambao fedha zao zitakwenda kusaidia. mfano mzuri ni msaada uliotoka UAE kusaidia hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar ni kwa maelekezo ya mfadhili mwenyewe.

..lakini kama kuna malalamiko labda ungetuletea hesabu ya fedha zote za misaada, halafu tugawanye kwa idadi ya watu, tuone kama per head, wa-Tanganyika wanapata zaidi ya wa-Zanzibari.

..mgogoro wa Zanzibar na Tanganyika kuhusu mgawanyo wa misaada na mapato ya muungano ulisuluhishwa na IMF na WB. hao ndiyo waliokuja na kile kifungu kwamba Zenj mpewe 4.5% ya mapato ya Muungano. sasa hata hao utasema wanawaonea kwasababu hawakuwapa 50% ya mapato ya Muungano?
 

Well said. Ndiyo hiyo per head niliyo kua najaribu kumueleza mwiba lakini akashindwa kuelewa. I think your post summarises everything about hizo pesa. kama kuna mtu atashindwa kuelewa basi ni uelewa waki tu ni finyu na wana lack comon sense. Haihitaji utaalamu wala elimu ya chuo kuelewa mambo mengine jamani.
 
 
wabara ndio wanaoungangania huu muungano Zanzibar hawautaki

Wazanzibar ndio wanaong'ang'ania huu Muungano. WaTanganyika HATUUTAKI! Iwepo Serikali MOJA TU, au Serikali TATU, au TUTENGANE KABISA.
Tukitungana itakuwepo nchi ya Tanganyika na nchi jirani ya Zanzibar. Uchaguzi utakaofuata huko Zanzibar utakuwa wa HURU na HAKI hivyo CUF watachaguliwa na kuongoza nchi yao, halafu wazenji wasiopenda demokrasia ya kweli (na matokeo ya kweli) watakimbilia Tanganyika.

Mtoto akililia wembe mpe!!!!1
 

Huu hapa!
Ila simuoni Karume akishiriki, LOL
Naona JKN alikua anachanganya mwenyewe

 
Anaeweza kuvunja Muungano ni Zanzibar anytime wakiamua tu ,ila wanawaonea huruma waTanganyika ,hivyo wanachojaribu ni Kuirudisha Tanganyika ,ili WaTanganyika wasije wakawalaumu hapo baadae mlichukua Zanzibar yenu mkatuwacha na mafisadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…