Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
I really hope for the sake of our nation haya matatizo ya muungano na malumbano hayata zidi hali ilipo fikia sasa.
 
Muungano waibua malumbano makali katika televisheni ya taifaNa Salim Said

MVUTANO mkali umeibuka miongoni mwa wasomi, wanasiasa na serikali katika mjadala kuhusu kero za Muungano uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Katika mjadala huo, baadhi ya washiriki walikua wakinyoosheana vidole na kutuhumiana kuwa, ndio wanaosababisha kukua na usugu wa kero za Muungano wa Tangayika na Zanzibar.

Mjadala huo ambao ulirushwa na Kituo cha Televesheni TBC1 uliwashirikisha baadhi ya wasomi, viongozi wa serikali na wanasiasa..

Waziri wa Nchi katika ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhmmad Seif Khatib alisema muungano umeimarika na kwamba ndoto za waasisi wake, ambao ni mwalimu Julius Nyerere na hayati Abeid Aman Karume zimetimia.

Kauli hiyo pia, iliungwa mkono na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azaveli Lwaitama ambaye alisema muungano umeimarika na kwamba, falsafa ya waasisi imetimia.

“Hata ukimuuliza ndugu yangu Duni hapo, atakwambia yeye ni Mtanzania, kero zinakuzwa na wanasiasa ambao hawajaelewa, yaliyokuwamo katika vichwa vya waasisi wa muungano huu” alisema Dk Lwaitama

Kauli hizo zilionyesha kumkera Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Juma Duni Haji ambaye katika kujibu hoja hiyo alisema, “kama kuimarika kwa muungano ni kuwepo kwa kero nyingi na matatizo, basi umeimarika lakini kama ni utatuzi wa matatizo na kero hizo, basi bado haujaimarika”.

“Katika mambo ambayo siyapendi na yananikera sana ni kuufananisha muungano huu kuwa ni wa mke na mume au mkubwa na mdogo. Huu ni muungano wa nchi mbili. Mimi nikiwa Katibu wa Wizara ya Fedha tuliisaidia serikali ya muungano dola 15 milioni za Marekani kulipa deni la Benki ya Dunia,” alisisitiza Duni.

Jambo hilo, lilimfanya muongoza mjadala huo ambaye ni mtangazaji wa TBC1, kumuomba radhi mwanasiasa huyo na kuruhusu mjadala huo kuendelea.

Duni aliendelea kutoa mifano ya kutoimarika kwa muungano huo kuwa, ni pamoja na kufukuzwa katika chama, kwa Rais mstaafu, Aboud Jumbe na maalim Seif Sharif Hamad, ambaye alikuwa waziri kiongozi wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kutoka na kesi za muungano.

“Muungano lazima ulete faida kwa wananchi kisiasa, kiusalama na kiuchumi lakini Wazanzibari wanahoji kuhusu fedha za misaada na mikopo zinazoingia nchini kwa jina la Tanzania, kwa nini hawapati,” alihoji Duni

Alisema, jambo muhimu ni kushughulikia kero za muungano na si kuwa, mtu akisema aitwe katika vikao vya kamati kuu ya chama na kunyamazishwa au kuadhibiwa.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari, Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (Misa- Tan), Ayoub Rioba alisema, kama kuna mawasiliano yanayoeleweka, baina ya viongozi na wananchi, matatizo ya kero za muungano yatamalizika.

“Kama tutakuwa na mawasiliano imara baina ya pande mbili hizi, tatizo ni dogo sana lakini pia tuthamini michango ya mijadala kama hii, kwa kuwa bado sisi tunayo fursa ya kujadiliana, wenzetu wanatafuta lakini hawapati fursa ya kujadiliana” alisena Rioba.

Katika hilo, Dk Lwaitama alisistiza kuwa, dhamira ya waasisi ilikuwa ni umoja na mshikamano wa Watanzania na Waafrika lakini matatizo na kero ni jambo la kawaida.

Kwa upande wake waziri Khatibu alisisitiza kuwa, uhuru, usalama, amani na uchumi wa Zanzibar unategemea serikali ya muungano iliyopatikana baada ya kuungana kwa Zanzibar na Tanganyika mwaka 1964. “Muungano ni wa binadamu wala si wa malaika, matatizo hayaepukiki lakini tunafanya jitihada mbalimbali za kutatua kero na matatizo hayo” alisema Khatib.

Hayaaa - mumenchezea kipole sasa yuaja 🙂
 
Bara tunaungangania na kuendelea kuwagharamia Zanzibar kwa kuwapangia watawala, na kuwapa income support

Zanzibar washatuchoka kwenye hii ndoa of convenience wanaona wao watakuwa bora kuwa kivyao

lakini cha ajabu mikataba ya huu muungano imekuwa siri ya Taifa, watawala wa bara hawapendi kudadisiwa juu yake

na mbaya zaidi after 40 YEARS nadhani its about time tukauvunja kwani HAUKUWEPO, UKAWEPO na UNAWEZA USIWEPO TENA ni contract ambayo inaweza kuvunjwa kama haina faida kwa pande zote mbili

Kwa maoni yangu mimi ama mkataba halali wa huu muungano haupo au kama upo basi kuna vipengele ndani ya mkataba wa muungano ambavyo wakuu hawataki wananchi wavijue, huu muungano ni wa nchi na kila mwananchi ana haki ya kuusoma huu mkataba ili apate kujua nini kimekubaliwa kwa niaba yake kama ambavyo tunavyoisoma katiba ya nchi yetu. Wakuu tuonyesheni na sisi huu mkataba acheni kutuziba macho enzi za kuzibana macho tayari zishapitwa na wakati - au bado mupo kwenye enzi za Chama kushika hatamu?.
 
GT hao wazanzibari unaosema hawautaki muungano ni wazanzibari gani? Maana yake kuna wazanzibari wenye asili ya kiarabu ambao wengi wao ni CUF hawa ni surrogates wa waarabu walioondolewa kwa mapinduzi mwaka 1964; sasa hawa kwa vyovyote vile hawawezi kuupenda muungano na wanatumiwa na jamaa zao waliokonje wafanye chokochoko ili waweze kurudisha utawala wao!!!!. Wale ambao walikuwa wanateswa enzi za Jamshid sidhani kama wangependa muungano uvunjike kwani kwa kufanya hivyo watakuwawanarudi kule walikokuwa wanadhalilishwsa utu wao. Sasa kati ya hawa GT ni wakinanani waliokuambia hawataki muungano na wako wangapi?

Ndugu yangu katika karne hii ambapo mpaka apartheid ya South Africa watu weshaanza kusahau bado unaamini kuna "boogeyman" muarabu anataka kuja kutawala Zanzibar na kunyanyasa watu - acheni kuwatisha watu na siasa zisizo kichwa wala miguu, hivi tuambizane ukweli hivi Aboud Jumbe, Ali Hassan Mwinyi na hata Abeid Amani Karume nani hasa ana asili zaidi ya kizanzibari ukilinganisha na huyo Jamshid?, mimi ni katika generation ambayo hatukumuwahi huyu Sultani na tulikuwa brainwashed kuamini kuwa alikuwa muarabu madevu toka Oman etc etc, nilipoiona picha yake kwa mara ya kwanza nilipigwa na butwaa, hana tofauti yoyote na Mpemba yoyote alioko Ilala au Kariakoo, au hana tofauti na Amani Karume kwa rangi na damu pia. Au bi Fatuma Karume mndengereko nae, mama Shadya jee?.
 
Kutoka mitandaoni
MGOGORO WA KISIASA WA ZANZIBAR
Tarehe 12.01.1964 Chama cha ASP kiliipindua Serikali ya ZNP na ZPPP
26.04.1964 Chama cha TANU kiliipindua Serikali ya ASP Zanzibar
26.04.1964 Serkali ya Tanganyika iliipindua na kuiondoa Nchi ya Zanzibar
ZANZIBAR INATANGAZA KWAMBA KITAIFA NA KIMATAIFA :
ZANZIBAR NI DOLA, TAIFA NA NCHI HURU SAWA NA NCHI YA TANGANYIKA
Rais wa Zanzibar Sh. Amani Abeid Karume ni Rais Sawa na Rais wa Tanganyika Sh. Jakaya Mrisho Kikwete
Waziri Kiongozi wa Zanzibar Sh. Vuai Nahodha ni sawa na Waziri Mkuu wa Tanganyika Sh. Mizegwe Pinda
Serikali ya Zanzibar ina hadhi sawa na serikali ya Tanganyika ijulikanayo kama Serikali ya Muungano
Baraza la Mawaziri la Serikali ya Zanzibar ni sawa na Baraza la Mawaziri la Serikali ya Tanganyika liulikano kama Baraza la Mawaziri la Serikali ya Muungano
Baraza la Wawakailishi la Zanzibar ni sawa na Bunge la Tanganyika lijulikano kama ni Bunge la Muungano
Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ni sawa na Wabunge wa Bunge la Tanganyika wajulikanao kama Wabunge wa Muungano
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ni sawa na Spika wa Bunge la Tanganyika
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ni sawa na Mwanasheria Mkuu wa Tanganyika
Mahakama Kuu ya Zanzibar ni sawa na Makahama Kuu ya Tanganyika
Baraza la Wawakilishi libadilishe Katiba ya Zanzibar na iwe na nguvu sawa na Katiba ya Tanganyika (Muungano)
Serikali ya Zanzibar na BLW wapeleke maombi kwenye Umoja wa Mataifa kukidai Kiti cha Zanzibar katika Umoja wa Mataifa
Zanzibar ijiunge na Mashirika ya Kimataifa kwa maslahi ya Zanzibar
Zanzibar iwe na vyama vyake vya Kisiasa vyenye sifa huru za kitaifa na kimataifa
Serikali ya Zanzibar na Baraza la Wawakilishi wapitishe sheria ya kulinda mali asili yote ya Zanzibar yakiwemo na Mafuta ya Zanzibar yawe chini ya Zanzibar
Serikali na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar waitishe Kura ya Maoni ya Wazanzibari kuwapa Wazanzibari fursa ya kuyakubali au kuyakataa Mapendekezo ya hapo Juu.
 
Boiler linachemsha kweli. Ni wewe Mwiba?

Sasa Watumwa wetu mwatupa kilichochetu? Mhhh, hii kali.

Nafikiri tatizo liko kwingine. Au ndiyo mchecheto wa mafuta huo? Wenzio Wafaransa, USA, German nk wako Bolivia ili kufanya utafiti wa magari yanatumia betri ili kuachana na mafuta na nyie ndiyo mnaamka na mafuta? Mambo sasa hivi ni Bolivia ndugu yangu kwa Moralez na si kwa Chavez tena.
 
Hayo ya betrii yatatufikia baada ya miaka mia,ila habari ndio hiyo ipo ndani ya kasha la habari muhimu huko UN ni muda tu ndio utakao amua wakati wahusika wameshaamua, tuliwaambia hata kikiwa kinibu basi kitatutosheleza.
 
Jana nilikuwa naangalia kipindi cha CNBC. Wakaonyesha jinsi GM walivyo busy katika kuokoa kiwanda chao cha magari. Wahandisi karibu wote sasa hivi wanashughulika na magari Hybrid na magari yanayotumia umeme peke yake. Magari haya yapo tayari na sasa hivi wanachofanya ni kutafuta njia ya kutunza charge kubwa na itakayodumu muda refu kwenye mabetri. Pia utengenezaji wake uwe cheap. Walionyesha hata jamaa mmoja mtaalamu wa magari na akajaribia gari moja ambalo alilisifia na kusema halina sauti na lina kwenda kama gari la kawaida.

Wenzetu wazungu si kama sisi. USA sasa hivi amekuwa kama simba aliyedhurika. Amegundua kuwa wakati anaonyesha ubabe na msuli, kuna vibwana mdogo vimeibuka na kumsogelea sana na au hata kumuacha katika mambo ya technology hasa magari. Wao walikuwa wanatamba na magari yao makubwa kama Hummer na ile mipick-up kama roli na inachoma mafuta kama haina akili, wenzao Ulaya na Japan wakawa wanatengeneza magari madogo yasiyochoma mafuta sana. USA wakidhamiria jambo basi historia inaonyesha kuwa wamekuwa wanafanikiwa.

Kama unafikiri ni baada ya miaka 100, basi utashangaa kuwa hiyo itatokea within 10 years. Ila magari ya hybrid nafikiri itachukuwa miaka 5 yawepo kibao duniani maana hata haya yaliyopo sasa yatakuwa used tayari na Watanzania watumia Mtumba tutaanz kuyanunua na kuwatetemesha majirani zatu kuwa tuna HB.
 
Kutoka mitandaoni
MGOGORO WA KISIASA WA ZANZIBAR
Tarehe 12.01.1964 Chama cha ASP kiliipindua Serikali ya ZNP na ZPPP
26.04.1964 Chama cha TANU kiliipindua Serikali ya ASP Zanzibar
26.04.1964 Serkali ya Tanganyika iliipindua na kuiondoa Nchi ya Zanzibar
ZANZIBAR INATANGAZA KWAMBA KITAIFA NA KIMATAIFA :
ZANZIBAR NI DOLA, TAIFA NA NCHI HURU SAWA NA NCHI YA TANGANYIKA
Rais wa Zanzibar Sh. Amani Abeid Karume ni Rais Sawa na Rais wa Tanganyika Sh. Jakaya Mrisho Kikwete
Waziri Kiongozi wa Zanzibar Sh. Vuai Nahodha ni sawa na Waziri Mkuu wa Tanganyika Sh. Mizegwe Pinda
Serikali ya Zanzibar ina hadhi sawa na serikali ya Tanganyika ijulikanayo kama Serikali ya Muungano
Baraza la Mawaziri la Serikali ya Zanzibar ni sawa na Baraza la Mawaziri la Serikali ya Tanganyika liulikano kama Baraza la Mawaziri la Serikali ya Muungano
Baraza la Wawakailishi la Zanzibar ni sawa na Bunge la Tanganyika lijulikano kama ni Bunge la Muungano
Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ni sawa na Wabunge wa Bunge la Tanganyika wajulikanao kama Wabunge wa Muungano
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ni sawa na Spika wa Bunge la Tanganyika
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ni sawa na Mwanasheria Mkuu wa Tanganyika
Mahakama Kuu ya Zanzibar ni sawa na Makahama Kuu ya Tanganyika
Baraza la Wawakilishi libadilishe Katiba ya Zanzibar na iwe na nguvu sawa na Katiba ya Tanganyika (Muungano)
Serikali ya Zanzibar na BLW wapeleke maombi kwenye Umoja wa Mataifa kukidai Kiti cha Zanzibar katika Umoja wa Mataifa
Zanzibar ijiunge na Mashirika ya Kimataifa kwa maslahi ya Zanzibar
Zanzibar iwe na vyama vyake vya Kisiasa vyenye sifa huru za kitaifa na kimataifa
Serikali ya Zanzibar na Baraza la Wawakilishi wapitishe sheria ya kulinda mali asili yote ya Zanzibar yakiwemo na Mafuta ya Zanzibar yawe chini ya Zanzibar
Serikali na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar waitishe Kura ya Maoni ya Wazanzibari kuwapa Wazanzibari fursa ya kuyakubali au kuyakataa Mapendekezo ya hapo Juu.

hizi hadithi za ndoto. serikali iliyokuwa huru ni ile iliyopinduliwa.

na walioipindua ni akina nyerere na watumwa walio zanzibar na walioletwa kutoka bara kwa mapinduzi.

baada ya hapo kuwekwa asp chama kilichoounganisha

wauaji
watumwa
na wanafiki wachache.
bada ya hapo kwa vile karume alikamatiwa malawi akawa kampambe kuegemea kwa wanafiki kuwadharau wauaji

ndipo wauaji walivyofanya tena mapinduzi kushirikiana na nyerere tena na nyerere kumueka ndugu yake jumbe

ndipo sasa ilipokuja ``mapinduzi daima``

hii ndio maana ya chama cha mapinduzi kilicho sasa tanzania

jina hili (mapinduzi) halikutokana juu ya kuungana vyama vi2 bali ni ukweli watanganyika ndio waliofanya mapinduzi na haya mapinduzi yapo daima.

ndio ukaona zanzibar kila uchaguzi watanganyika wanapelekwa kule pamoja na majeshi.

zanzibar bila ya kuwaandosha wauaji wakarudi kwa bara pamoja na wakuja waliokuja kujaza nchi na makafiri waliokuja kujaza ukafiri basi zanzibar haijawa salama.

visiwa vidogo ambavyo nafasi yake inawatosheleza wazanzibar tu leo imejaa watu kutoka bara. hawa watu wanaishi kama nzi bila ya sheria ila tu ni kujaza kura kwa ccm haya pia ni mapinduzi.

ndio wakatwambia wabara kuwa mapinduzi daima kwa wazanzibar.

kuna wazanzibar na wazanzibara

kaka lakuondoka si la wabara waishio Zanzibar tu bali na ZNZ waishio Bara, sijui patawatosha au wengine itabidi mwende Oman ilikupunguza msongamano.
 
Kisiwa cha Zanzibar ni cha Tanzania kama kuna mtu hapendi aondoke lakini zanzibar haiwezi kutuambia serikali gani tuwenayo wakati sisi ndiyo tumetengeneza hiyo nchi. Je zanzibar wanamchango gani kwenye nchi yetu kiuchumi. Je Watanzania wameijenga Zanzibar kwa miaka mingapi!. Matatizo mengi ya Zanzibar ni watu mfano ndugu zetu wa zanzibar hawaimizi elimu je mtaendeleaje bila elimu? je hili ni tatizo la bara pia, je CCM itabadilisha tabia za wazazi kutojali elimu?
 
Mwiba kila siku Zanzibar ijitoe, Zanzibar, Zanzibar. Lakini huishi kuijiingiza kwenye mijadala ya jeshi letu, EPA, Benki zetu, DPP wetu, Pinda, Kikwete, everything Tanganyika umo. Why care? Jamvi la Kitanganyika, umo.

Sitaki nataka type.
 
Wanzizibar vilevile ni lazima wajue vifuatavyo.

1. Karume na nyerere wanakufa na hawatarudi tena
2. Poroja ya historia ya muungano hazitasaidia karne hii.
3. Elimu ndiyo Tatizo kubwa la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla na halisababishwi na siasa badi tabia za wananchi.
4. Mtatakiwa kufikiria kutatua matatizo yenu kwa hali mlio nayo na hali halisi badala ya kufikiria kujitenga.
5. Tanzania haitagawanyika na zanzibar haitaweza kujitenga. Hakuna hata nchi moja inayofikiri hili wazo ni zuri mfano comoro bila Tanzania ingekuwa wapi. Hata waarabu hawapendi zanzibar iwe yenyewe kwani wanaangalia investment na si dini tu.
6. Miaka michache ijayo hakutakuwa na zanzibar kwa wananchi wa Tanzania na zanzibar wanabadilika na hawapendi kutegwa na hii italetwa na wanzanzibar wenyewe.
7. Tanzania itakuwa super power miaka 30 ijayo comoro, burundi, rwanda zitakuwa tanzania China, USA, EU, Japan na waarabu wanasapoti hili. EU ikiongozwa na German wamepewa EA Community na wanajenga makao makuu Arusha, China na Japan wamepewa barabara na bandari mfano daraja la kigamboni, reli ya Tazara, barabara mpya ya Tazania-Kenya, Scandinavia wamepewa elimu mfano NANIDA ya denmark, na USA wamepewa kuunganisha nchi mfano wametoa pesa kwa Tanzania kwenda Comoro, wanaongea na rwanda na burundi kufungua border na wanajenga kambi lindi na kusaidia jeshi.

Zanzibar kujitenga ni ndoto za mchana
 
nimesahau Waarabu wamewa kilimo na usafiri. Russia na India wamepewa afya na wanasomesha madaktari wengi sasa. South Korea wameomba wapewe teknologia lakini wa
 
Hongera vijana wa Zanzibar kwakuwa aware na na rasilimali zenu. endeleeni kutetea mambo ya msingi. Unafiki hauwezi kamwe kuisaidia Tanzania.
 
Mwiba kila siku Zanzibar ijitoe, Zanzibar, Zanzibar. Lakini huishi kuijiingiza kwenye mijadala ya jeshi letu, EPA, Benki zetu, DPP wetu, Pinda, Kikwete, everything Tanganyika umo. Why care? Jamvi la Kitanganyika, umo.

Sitaki nataka type.

Hata vita ya Uganda nilikwenda nikiwa katika kikosi cha mawasiliano nakumbuka nilijibanza juu ya mti mkubwa katika misitu na wajeshi wa nduli wakikatiza chini ,na baada ya hapo kuwasilisha ripoti kwenye kituo cha mawasiliano na kutoa data za wapi wanajeshi wa nduli wameelekea ,dogo kusema kweli hapo nilimuona yule malaika anaetoa roho kanikazia macho ile mbaya na mimi sikubadilisha nilitazamana nae mpaka akaondoka ndio nikajua kuwa nipo salama na kuwasilisha ,halafu nyie waTanganyika hamkogi ,maana kuna jamaa mmoja ambae alinihadithia alikuwa ni mwalimu katika shule ya Murutunguru kule ukerewe Mwanza ,huyu jamaa toka vita inaanza mpaka inamaliza hakuwahi kukoga wala kuchana nywele ,aliingia vitani kama askari wa kujitolea ,unajua siku zile sijui ilikuwa kulazimishwa au kujitolea lakini ,wale majeshi haswa tunaowaona wapo kambini hawakuwa mstari wa mbele waliwatomeza wale wa kujitolea baada ya kuwapa mafunzo ya kufyatua risasi na amaelekezo kidogo tu,lakini data ambazo tukiwapa kituo kikuu ziliwasaidia sana maana mizinga ilienda sawa na hesabu zetu na kuwasambaratisha waganda ,unajua kama si wazenji vita ile Tanzania isingeshinda 😀
 
Nyie wazanzibari na wazanzibara:

Hayo MADINI ya Bara mnayosema hayapo kwenye Muungano, hivi mnataka madini kama MADINI(MINERALS) au JUST AN EQUIVALENT AMOUNT OF MGAWO ulio chini ya makubaliano ya RUZUKU mnayopewa?

Acheni complication. Kama shida ni dau la ruzuku lipande, basi wasilisheni ishu...
 
Back
Top Bottom