Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Nyie wazanzibari na wazanzibara:

Hayo MADINI ya Bara mnayosema hayapo kwenye Muungano, hivi mnataka madini kama MADINI(MINERALS) au JUST AN EQUIVALENT AMOUNT OF MGAWO ulio chini ya makubaliano ya RUZUKU mnayopewa?

Acheni complication. Kama shida ni dau la ruzuku lipande, basi wasilisheni ishu...
Wewe Bwana - tafadhali wafahamu hao watu. hawahitaji ruzuku kutoka kwenu hata siku moja. Wao wana mambo yao na wanayaendesha - kama nyinyi mnatoa au hamtoi - lakini SMZ ipo pale na Zanzibar ipo na wanaendelea, lakini wanahitaji kuishi. Sasa msiwabane katika yale majambo ambayo ni yao. Kinyume cha hivyo- huna Muungano.
 
Hapana,

Hatutaki tafrani hapa jirani..na pia hatutaki wakimbizi wakianza kuchinjana wenyewe kwa wenyewe!

Mapinduzi tu waliuana watu zaidi ya 15,000!

Visiwani ni sehemu ya Jamhuri Kikatiba!


Hivi mapinduzi tuliuana au mulituua?, maana waangalieni uzuri wale waliopindua na utakuta kuwa 90% yao ni Wadanganyika waliolowea tu Zanzibar kwa kazi, hata Okello ni Mganda na huyu ndie alokuwa mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, sasa tuambizane ukweli - Zanzibar wameanza kuuana pale tu walipoanza kugawiwa makundi kutokana na siasa za Pan Africanism ambazo kwa Zanzibar zilimalizikia kuwabagua watu katika makundi ya waafrika, washirazi,waarabu etc. Jee ilitokea tu kuwa Nyerere alikuwa mstari wa mbele kwenye siasa za Zanzibar au alikuwa na lake moyoni tangu mapema?.
 
Mkuu nana kakwambia kuwa kodi inayotozwa Zanzibar inabaki Zanzibar? Kila kitu kinaenda Bara na baadae kurejeshewa hiyo 4%. Pahala kama uwanja wa ndege mapato yote yanakwenda Tanzania aviation na kuacha kiwanja hakina hata pahala pa kufanyia checking wasafiri. Ni aibu juwa na mvua ndio zao wasafiri. Pia kuna wakati maafisa wa TRA wakija Zanzibar kwa Boti asubuhi na kurudi na mapato boti ya kurudi saaa 10.jioni.
Mnapoelezwa kuwa upande mmoja wa Muungano hauna nia njema mnakaidi lakini mambo yanayofanyika huwezi kusadiki unapoambiwa.

Kwani kuna muungano au ukoloni uliogubikwa buibui la muungano?, huu muungano unavyoendeshwa si sawa na wakati muingereza alipokuwa na gavana wake tu, kila kitu kinaamuliwa Uingereza kama sasa ilivyokuwa kila kitu kinaamuliwa Tanganyika, hata raisi wetu anateuliwa Dodoma na uchaguzi ni kuziba macho watu tu.
 
Kisiwa cha Zanzibar ni cha Tanzania kama kuna mtu hapendi aondoke lakini zanzibar haiwezi kutuambia serikali gani tuwenayo wakati sisi ndiyo tumetengeneza hiyo nchi. Je zanzibar wanamchango gani kwenye nchi yetu kiuchumi. Je Watanzania wameijenga Zanzibar kwa miaka mingapi!. Matatizo mengi ya Zanzibar ni watu mfano ndugu zetu wa zanzibar hawaimizi elimu je mtaendeleaje bila elimu? je hili ni tatizo la bara pia, je CCM itabadilisha tabia za wazazi kutojali elimu?

Astaghfirullah - hivi unajua unaongea nini au unaropoka tu?, Zanzibar ni mali ya Zanzibar na wazanzibari wenyewe, hii jeuri ya kuwaambia watu wasiopenda Zanzibar kuwa ni ya Tanzania waondoke sijui imetokea wapi kwa ndugu zetu wadanganyika, nakumbuka miaka ya 1980s Kawawa alienda Pemba na kuwaambia watu kuwa CCM Pemba ni kwao na kama mtu hapendi CCM basi aondoke!!!!!!!. Tanzania haijaijenga Zanzibar bali kuibomoa kama huamini basi kaangalie takwimu za historia za Tanganyika na Zanzibar kabla ya muungano na fananisha kila kitu tangia elimu, uchumi, maendeleo n.k na utaona jinsi gani zanzibar ilivyoanguka katika miaka 45 iliyopita, inawezekana ni matatizo yetu wenyewe lakini kama kweli mulikuwa munaijenga mbona basi imezidi kubomoka. Zanzibar hivi sasa haisaidii kitu kiuchumi Tanzania maana haina tena cha kusaidia imeishafilisika lakini kumbuka tu ni jinsi gani tulikuwa tunasaidia wakati tulipokuwa na uwezo, muwekeni Kawawa kiti moto ataweza kukuambieni ukweli wa mulivyonufaika na mapato ya Zanzibar katika miaka ya 1970s na 1980s.
 
Wanzizibar vilevile ni lazima wajue vifuatavyo.

1. Karume na nyerere wanakufa na hawatarudi tena
2. Poroja ya historia ya muungano hazitasaidia karne hii.
3. Elimu ndiyo Tatizo kubwa la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla na halisababishwi na siasa badi tabia za wananchi.
4. Mtatakiwa kufikiria kutatua matatizo yenu kwa hali mlio nayo na hali halisi badala ya kufikiria kujitenga.
5. Tanzania haitagawanyika na zanzibar haitaweza kujitenga. Hakuna hata nchi moja inayofikiri hili wazo ni zuri mfano comoro bila Tanzania ingekuwa wapi. Hata waarabu hawapendi zanzibar iwe yenyewe kwani wanaangalia investment na si dini tu.
6. Miaka michache ijayo hakutakuwa na zanzibar kwa wananchi wa Tanzania na zanzibar wanabadilika na hawapendi kutegwa na hii italetwa na wanzanzibar wenyewe.
7. Tanzania itakuwa super power miaka 30 ijayo comoro, burundi, rwanda zitakuwa tanzania China, USA, EU, Japan na waarabu wanasapoti hili. EU ikiongozwa na German wamepewa EA Community na wanajenga makao makuu Arusha, China na Japan wamepewa barabara na bandari mfano daraja la kigamboni, reli ya Tazara, barabara mpya ya Tazania-Kenya, Scandinavia wamepewa elimu mfano NANIDA ya denmark, na USA wamepewa kuunganisha nchi mfano wametoa pesa kwa Tanzania kwenda Comoro, wanaongea na rwanda na burundi kufungua border na wanajenga kambi lindi na kusaidia jeshi.


Zanzibar kujitenga ni ndoto za mchana

Duuh - hii ina maana kila kitu tunasubiri nchi nyengine zije kutufanyia?, basi kuna maana gani ya kujitawala? hii ni sawa na kuwa na mke nyumbani halafu anahudumiwa na watu matajiri wa mtaa na wao ndio wanaoamua nani alete mchele au hata kufanya matengenezo ya nyumba - sawa hiyo?, Nyerere must be shaking in his grave.
 
SERIKALI TATU ZANZIBAR NA TANGANYIKA NDIO ZITAONYESHA UPANDE GANI WA MUUNGANO UNA WEZI NA UPI UNA WAADILIFU KWANI MAENDELEO BAADA YA KUANZA HIZO SERIKALI YATAONEKANA KWENYE UPANDE WENYE WAADILIFU.


Tunataka Serikali tatu - Razza

na Martin Malera

MFANYABIASHARA maarufu Zanzibar, Mohammed Razza, amesema kuna mgogoro mzito unaohusu nafasi ya Zanzibar ndani ya Muungano na kupendekeza muundo wa serikali tatu.

Mbali na hilo, Razza alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inapaswa kutangaza mgogoro wa kikatiba, na kupendekeza hatua kadhaa za kuchukua, ikiwemo ya kuwataka marais wastaafu wa pande mbili za Muungano, viongozi na wazee maarufu wakutane haraka ili kuunusuru Muungano ambao alisema Watanzania wengi bado wanaupenda.

Razza ambaye amewahi kuwa Mshauri wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari, katika Ukumbi wa Hoteli ya Starlight, jijini Dar es Salaam.

Akifafanua muundo wa pendekezo lake hilo, Razza alisema kuwe na serikali tatu ikiwemo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, hoja ambayo ilipata kutolewa na wabunge wa kundi maarufu la G55 miaka ya mwanzo ya 1990 na kukataliwa.

Mapendekezo mengine yaliyotolewa na Razza ni pamoja na kutaka iundwe mahakama ya kikatiba ili kuangalia suala hilo, kwa vile hakuna mahakama yoyote inayoweza kutoa uamuzi wa kikatiba kama huu na kusisitiza umuhimu wa kuwaomba marais wastaafu, viongozi na watu maarufu kukaa chini na kulipatia ufumbuzi tatizo hilo ambalo alisema kwa miaka 40 sasa limeshindwa kutatuliwa.

Alisema ameamua kutoa kauli hiyo baada ya kushtushwa na kauli mbili nzito zilizotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma kuwa, Zanzibar si nchi, huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Iddi Pandu Hassan, akipinga kauli ya Pinda na kusisitiza kuwa Zanzibar ni nchi. “Kwenye suala la nchi, sina urafiki na mtu. Bunge la Jamhuri ya Muungano linasema Zanzibar si nchi, Baraza la Wawakilishi linasema Zanzibar ni nchi. Vyote hivyo ni vyombo vya kutunga sheria na viongozi waliotoa kauli hizo ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali zote ni za CCM. Hii ni hatari kubwa, na si jambo la kulifumbia macho hata kidogo,” alisema Razza na kutoa msimamo kwamba Zanzibar ni nchi yenye mamlaka kamili.

“Zanzibar ina rais, ina mahakama kuu, ina baraza la wawakilishi, ina serikali yake, ilishawahi kuwa na mabalozi nje ya nchi, kabla ya Muungano, ina bendera yake, ina wimbo wa taifa, wanapofika viongozi wa nje, wanapigiwa mizinga 21, kwenye sherehe za Muungano na zingine, Rais wa Jamhuri anaingia kabla ili kumpokea Rais wa Zanzibar, bado mnasema si nchi, iitweje?” alihoji Razza.

Alisema ni makosa kuita Zanzibar sehemu ya Jamhuri ya Muungano na kutaja mfano wa baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro, Arusha, Tanga na mingine kuwa nayo ni sehemu ya Jamhuri, lakini haiwezi kufananishwa na Zanzibar, kwa vile ni nchi kwani ina mamlaka na madaraka kamili ya kujiongoza.

Akirejea historia ya kuanzishwa kwa Serikali ya Muungano, Razza alisema wakati waasisi wake, Mwalimu Nyerere na Mzee Amani Abeid Karume walipoamua kuufanya Muungano, nchi zote zilikuwa na hadhi sawa bila kujali kwamba Zanzibar ilikuwa na watu wachache kuliko Tanganyika.

“Turejee kwenye utamaduni, viongozi wetu Nyerere na Karume waliunganisha nchi mbili huru, zilizokuwa sawa, marais wao walikuwa sawa, iweje leo Zanzibar isiwe nchi? Basi kama si nchi basi tuambiwe tuiteje na rais wake aitwe nani?” alisema Razza na kulazimika kunukuu sehemu ya katiba ambayo alidai inasema Zanzibar ni nchi.

Mfanyabiashara huyo mwenye ushawishi mkubwa wa siasa za Zanzibar, alirejea kesi ya uhaini ya baadhi ya wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) ambao katika utetezi wao waliwasilisha hoja mahakamani kutaka waachiwe huru kwa madai kuwa, wasingeweza kufanya uhaini kwa vile Zanzibar si nchi, na mahakama ilikubali, lakini CCM tulipiga kelele kwa kudai Zanzibar ni nchi.

“Kitu cha ajabu leo, CCM iliyokuwa inatetea kwamba Zanzibar ni nchi, inasema Zanzibar si nchi. Kwa hiyo CUF walikuwa sahihi na CCM ni waongo, hali hiyo si nzuri katika siasa za Zanzibar,” alitahadharisha Razza.

Alisisitiza kuwa endapo mzozo huo utaachiwa, unaweza kuleta athari kubwa hasa visiwani Zanzibar ambako wananchi wamekuwa wakijadili kwa mtazamo tofauti hoja ya ama Zanzibar ni nchi au sehemu tu ya Jamhuri ya Muungano. “Waswahili wanasema kila penye tumbo la shari, huzaa heri. Zanzibar wanaona Muungano ni mzigo, Bara wanaona Muungano ni mzigo.

Tunataka serikali tatu, lakini kama tutaambiwa tuwe na serikali moja, bora mtulipue kwa mizinga, ibaki miti tu,” alisema Razza.

Mjadala wa Zanzibar ni nchi au la, uliibuka na kushika kasi baada ya Pinda kujibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Chwaka, Yahya Kassim Issa (CCM), aliyetaka kujua iwapo Zanzibar ni nchi au la.Issa katika swali lake kwa Pinda, alibainisha kuwa Zanzibar imefikia hatua ya kuwa na rais wake, mihimili yake pamoja na wimbo wake wa taifa, kisha akashangaa Pinda anawezaje kusema Zanzibar si nchi!Mbunge huyo aliuliza swali hilo Juni 26, mwaka huu, siku kadhaa baada ya Pinda kunukuliwa akisema wakati akijumuisha mjadala wa bajeti ya ofisi yake kuwa Zanzibar si nchi.Kauli na majibu hayo ya Pinda yaliibua mjadala mzito ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ambako hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Iddi Pandu Hassan, alisimama na kumpinga Pinda akisisitiza kuwa Zanzibar ni nchi.Mwanasheria huyo alisema Zanzibar, kama zilivyo nchi nyingine, ina mihimili mitatu ya utawala inayojumuisha Serikali, Mahakama na Baraza la Kutunga Sheria hivyo ni nchi.



TUNAOMBA MAWAZO YENU KWENYE HILI.
 
Hili suala alilitolea ufafanuzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndg Jakaya Kikwete na tangu hapo hakukuwa tena na swali la Zanzibar ni nchi au la. Suala la Serikali tatu au mbili ni makubaliano ya pande mbili na vyombo husika vikae kulijadili kuliko kuropoka na kujitafutia umaarufu rahisi kama anavyofanya Raza na kucreate unnecessary conflict. Anachofanya Raza ni kuongeza chuki badala ya kutengeneza amani. Anaposema watanzania bara na wazanzibari wanauona Muungano ni mzigo, huo utafiti aliufanya lini? Atupe basi ripoti ya utafiti wake tuijadili. Otherwise, it's just an unnecessary exaggeration!
 
Sera ya Chama cha Mapinduzi ni Serikali mbili kuelekea kwenye Moja (Kama alivyofafanua Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati ule!) sasa nashangaa vipi Raza anakuwa kada (au mkereketwa) wa CCM wakati anapinga sera za Chama chake?
 
Sera ya Chama cha Mapinduzi ni Serikali mbili kuelekea kwenye Moja (Kama alivyofafanua Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati ule!) sasa nashangaa vipi Raza anakuwa kada (au mkereketwa) wa CCM wakati anapinga sera za Chama chake?
Vipi Raza, bado hajapata wawekezaji pale Changu Soap? Hizi kelele zake mbona zinazidi kadiri inavyokaribia 2010?
 
Raza kama anataka kugombea 2010 agombee tu, nafasi anayo na sio kuwachanganya wananchi majuukwaani na kufanya kampeni kabla ya wakati. Wakati ukifika basi auze sera zake za Serikali tatu. Kwani kwenye chama si kuna vikao halali? Kwanini wasizungumze kama chama halafu wakawaambia wananchi msimamo wa chama, km. serikali moja, mbili au tatu? Sasa kila mtu kwenye chama hicho hicho anasema la kwake majukwaani...Oh, please, we are fed up with these sentiments.
 
Is Raza sitll a factor? Tusije ttukawa tuna jadili maneno ya mtu anaye tafuta kusika tena kwenye siasa. Na taarifa hii mbona ina elekea ya zamani?
 
Kwani kuna muungano au ukoloni uliogubikwa buibui la muungano?, huu muungano unavyoendeshwa si sawa na wakati muingereza alipokuwa na gavana wake tu, kila kitu kinaamuliwa Uingereza kama sasa ilivyokuwa kila kitu kinaamuliwa Tanganyika, hata raisi wetu anateuliwa Dodoma na uchaguzi ni kuziba macho watu tu.
Kuna ubaya gani maalim! ndo muungano huo atii
mbona huzungumzii kero ya wapemba kuzagaa ovyo bara?
 
zanzibar hawana hela za kujiendesha wenyewe wanaishi kutokana na (kodi na mapato mengine) yatokayo bara.

miaka yote wa bara walikua wanalipia umeme ghali, ili zanzibar watumie bure mbona hawakuwa wanalalamika

kwani hata bara siwanataka hiyo rasilimani mbona ujasema na wao wanaangalia, kutaka iwe yako ni swala jingine na kuangalia ni swala jingingine usichanganye habari.
swala la zanzibar kuangalia rasimali yake sidhani kama ni liatatokea kama wameweza kutoa msamaha wa kodi $19m na wao mapato yao ni $20m.
Mkuu Semilong salam,
Ikiwa maoni yako ni sahihi basi Zanzibar ni mzigo kwa Tanganyika, wakati wenyewe Wazanzibari wanazoza kila kukicha juu ya maswala kadhaa yahusuyo so called MUUNGANO kwanini Wanasiasa wa Tanganyika wanasisitiza KUULINDA muungano huo ambao ni mzigo kwao?????
 
Vipi Raza, bado hajapata wawekezaji pale Changu Soap? Hizi kelele zake mbona zinazidi kadiri inavyokaribia 2010?

Sidhani kama anaweza kupata muekezaji kiwandani pale. Kwani si unajua wewe kuwa Biashara za Raza ni za kimkukumkuku tu na zinategemea kubebwa sasa zikikosa ni balaa, Changu hapana kitu cha kuvutia muwekezaji.
 
habari jamani..

mimi ndo posti yangu ya kwanza hapa JF.. ila sio mgeni kwasababu ninaweza nikasema I have been much of an observer au sideman.. nimekuwa natembelea sana hii JF lakini nimekuwa na prefer sana kuwa nasoma articles (posts) na comeents za watu, mabishano na najifunza mengi sana.. ckuwawahi kushawishika kucomment hapa au kupost hoja yangu… cjui sababu kuu ni nini lakini maybe tu kujiona bado mbichi katika mambo haya yanayo ongelewa humu.. na kuwacha wazee wazima kwenye uwanja.. wakina Blue ray, yo yo, mwanakijiji, nzi, nkruhma na wengine wengi…..

lakini leo nimeamua na mimi nichangie kidogo baada ya kuguswa na mjadala na maoni ya hapa..
nimesoma comment karibia zote za mpaka sasa…

kitu kimoja nimegundua ni kuna kutupiana sana lawama hapa kati ya pande mbili… pande ya watanzania bara na Tanzania visiwani… kuanzia wanaochangia humu JF hadi viongozi wa siasa.. hii Blame game imechukua sura kubwa… serikali,bunge la pande zote wote wanatupiana lawama.. ILA bado cjajua nikitu gani haswa wanachotupiana lawama… sijajua tatizo haswa nini??? Nahili ndo swali ambalo watu wa humu JF nadhanni ingekuwa vizuri wangejiuliza kabla ya kuanza kushutumiana na kutupiana lawama… tatizo ni nini haswa??? Tukianza na hili swala nadhani tunaweza hata kufikia kijua nani mwenye tatizo.. kwasababu kama kunatatizo lazima kutakuwa na aliyesababishia kama si kilichosababisha..

Nimejaribu kujiuliza sana na mimi hilo swali?? Tatizo nini?? Well cjapata jibu hadi sasa hivi kwasababu kuna sababu nyingi sana ambazo sito zi horodhesha sasa hivi kwasababu nahitaji kuzifanyia uchunguzi.. ila ohja ya haraka haraka tu ninaweza kusema.. nimegundua moja ya tatizo ni VIONGOZI waliopo serikalini na Waliopokea madraka kutoka kwa wale walioanzisha huu muungano..

Na hao hao viongozi wamelifanya tatizo liwe lakisiasa zaidi na kuwapeleka wananchi wa nchi hizi mbili katika matatizo..

Sidhani kama mwanachi wakaida ukimuuliza kwanini unataka muungano atakupa sababu kama ‘muhimu ki uchumi, ulinzi' …

Mimi ukiniuliza kwanini nataka muungano nitakumbia kwasababu Zanzibar is Tanganyika na Tanganyika is Zanzibar…hiyo haina ubishi.. hizi nchi mbili zina hadhina kubwa ya Mila na tamaduni.. they have so much in common and shared a lot in culture.. Ukizungumzia historia ya Tanganyika, Zanzibar imo na imecheza pati kubwa sana.. ukizungumzia Zanzibar, Tanganyika imo na imecheza pati kubwa sana..

Kwa miaka zaidi ya 100 sasa watu wamekuwa waki move na kuzaliana kati ya hizi inchi mbili kama ni miji miwili… watu wamezaliana na kuanzisha makazi from Tanganyika to ZNZ na from ZNZ to Tanganyika…

Sasa unafikiri hawa watu (wananchi) wanataka kuvunja muungano kweli….?????
 
Mimi ukiniuliza kwanini nataka muungano nitakumbia kwasababu Zanzibar is Tanganyika na Tanganyika is Zanzibar…hiyo haina ubishi.. hizi nchi mbili zina hadhina kubwa ya Mila na tamaduni.. they have so much in common and shared a lot in culture.. Ukizungumzia historia ya Tanganyika, Zanzibar imo na imecheza pati kubwa sana.. ukizungumzia Zanzibar, Tanganyika imo na imecheza pati kubwa sana..
Kwa miaka zaidi ya 100 sasa watu wamekuwa waki move na kuzaliana kati ya hizi inchi mbili kama ni miji miwili… watu wamezaliana na kuanzisha makazi from Tanganyika to ZNZ na from ZNZ to Tanganyika…

Sasa unafikiri hawa watu(wananchi) wanataka kuvunja muungano kweli….?????

Unayozungumza hasa katika sehemu hii mimi kwa mawazo yangu nafikiri ni sahihi. Na nafikiri umefika wakati Katika Katiba na sheria zetu tukasema bayana kuwa Nchi yetu ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na inabakikia kuwa hivyo daima na milele. sasa hapo hakuna tena nafasi ya kulumbuna kama Muungano upo au la.

Kuna mfano wa Marekani wamesema hivyo kikatiba na iko hivyo. Na kule hakuna aliye hodari tena wa kuleta hoja ya kuhoji kwa nini kumekuwepo na United States of America. Kuhusu ni namna gani Muungano wetu uwe nafikiri tusingekuwa tunatawaliwa na hamasa za kutaka uwe kama vile tunavyotamani uwe.

Lakini tungeuwacha ukaendelea kuchukuliwa na mkondo asilia- ukanyumburuka kwa minajil ya hali ya maisha na mazingira yanavyokwenda.

Mathalan hivi sasa ni vigumu kusema kuwa unataka Serikali moja na uongozi wa himaya moja. Hili ni jambo linaloweza kuja wenyewe kwa kufuata mnyumburuko asilia, huko mbele, si la kulichukulia nguvu kama tunavyotamani iwe.

Unapolitaka kwa nguvu ndipo pale inapotokea nguvu ya pili (counter forces) ya kuvutia kwa nyuma na kutoa kauli ya kutaka kujitenga.
 
*Wadai Pinda, Nohodha hawana mamlaka kujadili kero
*Wataka mkataba wake sasa ujadiliwe bungeni
*Wahoji kufutwa Serikali ya Tanganyika
*Serikali yasema wenye Tanganyika walishakufa
*Spika Sitta amtimua John Cheyo bungeni

Na John Daniel, Dodoma

KATIKA hali isiyotarajiwa wabunge wote wa Zanzibar (wa Chama Cha Mapinduzi -CCM na Chama cha Wananchi-CUF),jana waliungana kuushambulia Muungano huku wakidai kuwa Waziri Mkuu Bw.Mizengo Pinda na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) Bw. Shamsi Vuia Nahodha hawana mamlaka kujadili kero za Muungano huo.

Akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais iliyowasilishwa bungeni jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Batilda Burian, Mbunge wa Chwaka Bw. Yahya Kassim Issa (CCM), alisema Tanzania Bara inawanyonya na kuwarudisha nyuma Wazanzibar katika nyanja mbalimbai ikiwemo elimu na biashara.

“Wenzetu (Watanzania Bara) mnatuwekea vikwazo, bandari ya Zanzibar imekufa, watu walikuwa wanachukua vitu kwenda na kurudi lakini sasa hakuna, vikwazo wanavyowekewa ni matatizo, leteni vitu vya kiuchumi vitakavyosaidia Zanzibar ,hatutaki kusikia hadithi.

“Mafuta ni haki ya Zanzibar, sisi hatujaomba, sisi tulikuwa nchi kamili kama ilivyokuwa Tanzania Bara, mtu akikukanyaga ukanyamaza hatajua amekukanyaga, sisi Wazanzibari tunashindwa kujizuia kuhusu mambo ya Muungano,” alisema Bw. Issa na kusisitiza kuwa mwaka 2011 watakaporudi bungeni, hawataelewa mambo yakienda mrama.

Kwa upande wake msemaji wa Kambi ya Upinzani katika masuala ya Muungano Mbunge wa Viti Maalum Bi. Riziki Omar Juma, (CUF), alilitaka Bunge kuiagiza Serikali kuvunja haraka mazungunzo kati ya Waziri Mkuu, Bw. Pinda na Waziri Kiongozi Bw. Nahodha na kuwasilisha Mkataba wa Muungano bungeni ili ujadiliwe kwa lengo la kumaliza matatizo yaliyopo.

“Hatuoni kwamba vikao hivi vya pamoja (Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano na waziri Kiongozi wa SMZ ) vinakuja na suluhisho la tatizo la Muungano, vyenyewe ni sehemu ya tatizo, ili kutimiza wajibu wetu kama Bunge la watu lenye jukumu la kusimamia matumizi ya fedha za walipa kodi, liitake Serikali ya Muungano isitishe mara moja vikao hivi, badala yake Mkataba wa Muungano uletwe hapa bungeni kama nukta kuu ya mjadala, hapo ndipo tuanzie na tumalizie kero za Muungano.

“Ofisi ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi hazina uwezo wa kujadili Muungano, hapa ni kizungumkuti kinachofanyika. Katika Mkataba wa Muungano, hakuna sehemu inayosema kufutwa kwa Serikali ya Tanganyika,”alisema Bi. Juma.

Alisema Kambi ya Upinzania inaona kazi inayofanywa sasa na Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi kujadili Muungano, ni kama sehemu ya kuongeza kero kwa kuwa ajenda kuu wanayoina ni ukiukwaji wa Mkataba wa Muungano hivyo kero zinazojadiliwa ni matokeo ya tatizo na si tatizo lenyewe.

“Watanznzania waniwie radhi kusema kwamba wakubwa wetu wameufanya Muungano huu ushabihiane sana na kile kisa cha Mfalme Jeta aliyemo kwenye riwaya ya Kusadikika akiwa amekaa katika eneo ambapo mto uliokuwa unakokozoa kila kitu, mawe, magogo, majengo, unatiririka kinywani na kuishia tumboni, lakini mara alisikika akilia 'njaa !njaa!' kiu!kiu!”alisema Bi. Juma.

Alisema katika suala la Muungano hakuna mkubwa wala mdogo na kusisitiza kuwa nchi zilizoungana zilikuwa nchi kamili na suala la udongo halipaswi kuwepo na kuongeza kwamba Serikali ya Muungano ndio inayopaswa kubeba lawama kuhusu Muungano.

Alidai kuwa mazungumzo yanayofanywa kati ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi ni sawa na watu wanaokutana kunywa kahawa au chai na si kufanya jambo la maana.

Naye Mbunge wa Mkanyageni, Bw. Mohamed Habib Mnyaa (CUF),alisema timu ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi hazitoshi kujadili suala la Muungano kwani linawagusa Watanzania wengi hivyo lilipaswa kushirikisha nyanja mbalimbali.

Bw. Mnyaa alikwenda mbali zaidi na kutoa mfano wa swali la mwanawe kuhoji uhalali wa kiongozi mmoja (marehemu Mwalimu Julius Nyerere) kuonekana akichanganya udongo peke yake,jambo linalotia dosari kwenye misingi ya Muungano humo.

Bw.Mnyaa alisema tangu mwaka 1990 hadi 2000 zimeundwa tume 12 kushughulikia matatizo ya Muungano lakini hadi sasa hakuna muafaka uliopatikana.

Hivi karibuni Serikali iliweka wazi mambo matatu yaliyopatikana kupitia mazungumo kati Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi kuwa ni pamoja na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Uvuvi katika bahari kuu na shughuli za biashara ya meli.

Katika Hotuba yake, Dkt. Burian alisema Serikali imepiga hatua katika mazungumzo kati ya viongozi hao wawili na kueleza kwamba vikao hivyo vitaendelea kwa kasi zaidi ili kuboresha Muungano.

Akijibu hoja hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw.Muhammed Seif Khatib alisema suala la Serikali ya Tanganyika kwa sasa halina nafasi kwani wenye Tanganyika walishakufa.

Alisema wakati wa Muungano Tanzania ilikuwa na watu milioni 10 tu na sasa wapo zaidi ya milioni 40.

Alisisitiza kuwa Waziri Mkuu na Waziri kiongozi wana uhalali kujadili kero za Muungano kwani mwenyekiti suala hilo ni Makamu wa Rais.

Source:
Majira
 
ukweli mficha maradhi kifo kitamuumbua huu ni wakati muafaka kuweka kila kitu wazi

au mnasubiri mpaka waasisi wote wafariki halafu wajukuu zetu watumbuane macho?

nnaamini upeo na uelewa watanzania uko juu wajuulishwe na wafahamishwe nn kilitokea na washirikishwe ktk maamuzi hapana cha kuogopwa juu ya hilo
 
Hakika shoka haliwezi kuwa shoka mpaka liwekwe kipande cha mti (Mpini).

Kwani shoka litakata miti yoote mara baada a kuweka kipande cha mti (Mpini)
 
Ukitaka kujua kama wanauwezo wa kweli wa kuwa wamoja subiri 2010 kwenye uchaguzi. Ndio utajua kama ni wakweli au uzugaji tu.
 
Back
Top Bottom